Muganyizi Jackson
Member
- Aug 11, 2016
- 13
- 3
Mkuu wa wilaya Majula kasika , mkurugenzi Marcelin Ndimbwa na Engineer, Maimuna makutika wa wilaya ya Malinyi wakutana na wahitimu wa vyuo vikuu Dar es Salaam Leo 13
.8.2016
Katika kuhakikisha vijana wanajiari kupitia kilimo, mkurugenzi na mkuu wa wilaya ya Malinyi iliyopo mkoani Morogoro Leo wamefanya kikao kifupi na Viongozi wa kikundi cha Mtaji Ardhi cha vijana wahitimu wa Elimu ya juu kilichopo hapa Dar es Salaam, pamoja na mambo mengine Viongozi hao wamewakalibisha vijana Kwenda kulima wilayani Malinyi ambapo wamewahidi kuwapatia eneo la kulima bure, mbegu bure na kuwalimia bure kwa msimu wa kwanza wa mradi. Viongozi wa halmashauri ya Malinyi wamefurahishwa na kitendo cha vijana wasomi tena wa Elimu ya juu kuamua kujikita kwenye kilimo, mkurugenzi ameandaa mbili zaidi na kusema " sisi kama halmashauri tunawakaribisha mno na tunategemea mtaweza kubadilisha jamii yetu ya Malinyi na wao kujikita kwenye kilimo". Kwa upande wa engineer ametuhakikishia kuwa ardhi inafaha kwa mazao yote na hali ya hewa ni nzuri mnoooo. Kwa upande wa mkuu wa wilaya hiyo anasema lengo la serikali ya Rais Magufuli ni kuhakikisha vijana wanajiari wenyewe na serikali ya halmashauri kuwauunga mkono vijana na watu wote waliotayari kujiajiri, pia halmashauri hiyo imeunda vikundi zaidi ya 25 vyenye watu 150 na kuviwezesha pembejeo za kilimo bure na halmashauri, pia Halmashauri inampango wa kujenga ghara kubwa la kuhifadhi mazao ya wakulima wakati wa mavuno na kujenga kiwanda cha kuongeza mazao ya wakulima thamani.
Kwa ujumla wetu tumefurahishwa na juhudi za wasaidizi wa Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania za kutekeleza maagizo ya Rais kwa matendo na kuanza kuitafsiri Ilani ya CCM 2015 kwa vitendo. Tunatoa wito kwa Viongozi wengine kwenye halmashauri zote nchini kuinga utaratibu huu na kuuanzisha katika maeneo yao kwani unalenga kuwainua wananchi hasa vijana kiuchimi na haya ndio mabadiliko ya kweli kwa kila mtanzania na kufikia maisha bora kwa kila mtu hasa mnyonge.
Tunatoa wito pia kwa vijana wengine hasa wahitimu kwenye vyuo vya Elimu ya juu kote nchini kujiunga kwenye vikundi na kufuatilia fursa hasa za kilimo cha kibiashara na kuachana kulalama kila leo na kutegemea ajira za maofisini tu.
Imetolewa kwenu na
Jasper Jackson Muganyizi
Mwenyekiti
Kikundi cha Mtaji Ardhi
Dar es Salaam, Tanzania
0784097173
"ukitaka mali utaipata shambani"