Wasomi kukosa ajira ilaumiwe Serikali 100%

Samiaagain2025

JF-Expert Member
Joined
Dec 2, 2020
Posts
4,796
Reaction score
5,278
Wakati akilihutubia bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania,rais Samia Suluhu Hassan alisema serikali itaanza kutoa elimu ya itakayomuwezesha msomi kujiajiri.

Maswali haya yafuatayo yatadhibitisha kuwa serikali ni chanzo Cha tatizo hili 100%:

1. Serikali ilikubalije kutumika kwa mtaala huu mashuleni na vyuoni,usiowafanya wasomi wajiajiri?

2. Je,Hawa waaomi ambao tayari wamehitimu ktk mtaala huu ambao una matatizo (hauwafanyi wasomi wajiajiri),wanasaidiwaje?

3. Kuna baadhi ya kozi vyuoni( especially vyuo vikuu), wasomi wanadhaminiwa kwa asilimia mia,je,
Unatoaje udhamini wa asilimia mia huku ukijua msomi huyu akihitimu humpi au hapati ajira?

4. Bado siamini,hivi mfano mtu umesomea kozi zifuatazo,utaweza vipi kujiajiri?

Ualimu, Utawala,Mipango, maendeleo ya jamii,sayansi ya siasa.

Laaa! Mungu aseme na viongozi wetu,
La sivyo
Tutaendelea kuomba ili Mungu atende tena.
 
Serikali iwekeze zaidi katika kutoa mikopo rafiki na kuboresha mazingira ya watu kujiajiri. Hata hizo kozi unazohisi hawawezi kujiajiari wataweza.
 
Ukweli na usemwe... sio Tz tu ajira hakuna...sema sasa Serikali uweke mazingira mazuri ya wahitimu waweze kujiajiri...kusiwe na longolongo

Yaani mambo yabkufanya yapo mengi sana. Hizo kada zote ulizotaja mitaani kuna mishe mob za kufanya .ishu tunataka kufika mapema..hatupendi kuteseka
 
Mtu umesomea political science,unaambiwa eti "ujiajiri"!

Hizi ni akili gani hizi?
 
Serikali itoe udhamin kwa kozi na idadi chache tu inayoimudu, iwapo mafunzo bora
Wengine waelekezwe VETA....au wachague kutembea na fundi
 
Wakati akilihutubia bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania,rais Samia Suluhu Hassan alisema serikali itaanza kutoa elimu ya itakayomuwezesha msomi kujiajiri.

Maswali haya yafuatayo yatadhibitisha kuwa serikali ni chanzo Cha tatizo hili 100%:

1.Serikali ilikubalije kutumika kwa mtaala huu mashuleni na vyuoni,usiowafanya wasomi wajiajiri?

2.Je,Hawa waaomi ambao tayari wamehitimu ktk mtaala huu ambao una matatizo (hauwafanyi wasomi wajiajiri),wanasaidiwaje?

3. Kuna baadhi ya kozi vyuoni( especially vyuo vikuu), wasomi wanadhaminiwa kwa asilimia mia,je,
Unatoaje udhamini wa asilimia mia huku ukijua msomi huyu akihitimu humpi au hapati ajira?

4. Bado siamini,hivi mfano mtu umesomea kozi zifuatazo,utaweza vipi kujiajiri?
Ualimu, Utawala,Mipango, maendeleo ya jamii,sayansi ya siasa.

Laaa! Mungu aseme na viongozi wetu,
La sivyo
Tutaendelea kuomba ili Mungu atende tena.
Mkuu ina maana wote waliojiajiri hawakusoma kwa kutumia hiyo mitaala, mitaala ni kama nyenzo tu kujiajiri ni uthubutu wa mtu, duniani kote hakuna nchi ambayo haina tatizo la ajira hata hao wenye mitaala unayofikiria wewe, kujiajiri siolazima ufuate kozi uliyosomea, huyo atakuwa sio msomi,msomi yeyote lazima atumia akili na maarifa yake kufikiria nje ya box, sababu naamini msomi ni msomi tu hata kama anashinda akivuta bangi , tatizo la wasomi wa Tanzania wanatakiwa waletewe kila kwetu kwenye hotpot mezani wao wapakue tu. Tanzania pana fursa nyingi sana sio lazima mtu akuajiri, kama wasomi mnaweza kuunda vikundi, mkaandika mpango biashara/kazi na mkapata mikopo au mkajichangisha vijisenti kidogo mkaanza kufanya shughuli zenu,tumeona baadhi ya vijana waliosomea kwa mfano uhasibu wakianzisha kampuni za uhasibu na ukaguzi na wanaendelea vizuri ,wao wameona kuna pengo kati ya wafanyabiashara na mambo ya kodi au ukaguzi wa vitabu kutokana na sheria kwamba kwa biashara yoyote lazima uwe na vitabu vya mahesabu ndio ukadiriwe TRA au upate tenda kwenye mashirika, waliosomea uganga au maabara wanaweza kuanzisha maabara zao za uchunguzi wa magonjwa na kutokona na hali ya aisha siku hizi watu wa maabara wanapiga pesa ndefukutokana na kazi zao. Tatizo tunataka serikali iwe mwaajiri wakati ni jambo lisilowezekana na kujiajiri serikali imeweka mazingira bora ya kila mtu afanye kazi,imetengeza miundo mbinu, imerahisisha usajiri wa kampuni na hata sasa inafanya maboresho kwenye mambo ya ukusanyaji mapato hivyo ndio serikali inasaidia.Fanyeni kazi ,ajira zisizo rasmi zipo nyingi ,lima hata bustani utapata pesa, nendeni nje mkabebe box sio mnakaa tu ,wenzetu Wakenya wana uthubutu wa kutoka nje na kujiamini kwenda kutafuta au kufanya kazi, hiyo ni njia nyingine ya ajira.
 
Mtu umesomea political science,unaambiwa eti "ujiajiri"!

Hizi ni akili gani hizi?
Nani kakwambiaaliyesoma political science hawezi kujiajiri? labda awe kihiyo, kwanini asianzishe kampuni ya ushauri wa mambo ya kisiasa,si umeona kuna NGOs nyingi na watu binafsi wanaishi kwa ajili ya kuwa washauri wa mambo ya siasa? pia unaweza kuajiriwa na Chadema/CCM/TLP/ACT etc ukawa mshauri wao. Tatizo la vijana wetu wanashindwa kujiamini kila msomi anataka aajiriwe BOT, TRA ,Serikalini au kwenye wakala wa serikali, makampuni ya simu.
 
Wakati akilihutubia bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania,rais Samia Suluhu Hassan alisema serikali itaanza kutoa elimu ya itakayomuwezesha msomi kujiajiri.

Maswali haya yafuatayo yatadhibitisha kuwa serikali ni chanzo Cha tatizo hili 100%:

1.Serikali ilikubalije kutumika kwa mtaala huu mashuleni na vyuoni,usiowafanya wasomi wajiajiri?

2.Je,Hawa waaomi ambao tayari wamehitimu ktk mtaala huu ambao una matatizo (hauwafanyi wasomi wajiajiri),wanasaidiwaje?

3. Kuna baadhi ya kozi vyuoni( especially vyuo vikuu), wasomi wanadhaminiwa kwa asilimia mia,je,
Unatoaje udhamini wa asilimia mia huku ukijua msomi huyu akihitimu humpi au hapati ajira?

4. Bado siamini,hivi mfano mtu umesomea kozi zifuatazo,utaweza vipi kujiajiri?
Ualimu, Utawala,Mipango, maendeleo ya jamii,sayansi ya siasa.

Laaa! Mungu aseme na viongozi wetu,
La sivyo
Tutaendelea kuomba ili Mungu atende tena.
Chanzo cha serikali ni wewe. Kama huwezi kuleta mabadiliko kwa elimu uliyo ipata serikali haihusaidi. Elimu ya Chuo huwa inapanua uwezo wako wa kufikiri na utayari wa kutenda, Chuo Kikuu hakifundishi Mafundi Mchundo, ni vyuo vya katikati ndio kazi yake.

Muono wa mahitaji na mabadiliko ya kiutendaji kazi ni wewe.

Mwaka 1980, Chuo Kikuu cha Dar es salaam, hawa wote nitakao wateja ambao kwa sasa tunawaita Deputy Vice Chancellors ni wasomi waliomaliza Darasa la nane hawakupata nafasi yakuendelea moja kwa moja Sekondari, lakini walijiendeleza na kupata kiwango cha juu kabisa cha Elimu, DVC Academic Prof. Kimambo, DVC Administration Dr. Kinunda, DVC Finance Mr. Jamieson, DVC reseach and Library services Mr Mvaa..

Kina Kishimba, Musukuma, Maji Marefu, Shigongo na maelfu ambao walipata elimu ya Darasa la Sabá lakini sasa hivi ni Mabilionea, au wamejiendeleza na kuwa Ma professor na kufanikiwa katika nyanja zingine, Je utaipongeza serikali.

Mabadiliko ya maisha baada ya kupata elimu hata iwe ndogo sana ni wewe mwenyewe unavyo weza kuitumia hiyo Elimu ndogo kwa manufaa na kuongezea pato au elimu hiyo hiyo kuziba penye upungufu.
 
Wakati akilihutubia bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania,rais Samia Suluhu Hassan alisema serikali itaanza kutoa elimu ya itakayomuwezesha msomi kujiajiri.

Maswali haya yafuatayo yatadhibitisha kuwa serikali ni chanzo Cha tatizo hili 100%:

1. Serikali ilikubalije kutumika kwa mtaala huu mashuleni na vyuoni,usiowafanya wasomi wajiajiri?

2. Je,Hawa waaomi ambao tayari wamehitimu ktk mtaala huu ambao una matatizo (hauwafanyi wasomi wajiajiri),wanasaidiwaje?

3. Kuna baadhi ya kozi vyuoni( especially vyuo vikuu), wasomi wanadhaminiwa kwa asilimia mia,je,
Unatoaje udhamini wa asilimia mia huku ukijua msomi huyu akihitimu humpi au hapati ajira?

4. Bado siamini,hivi mfano mtu umesomea kozi zifuatazo,utaweza vipi kujiajiri?

Ualimu, Utawala,Mipango, maendeleo ya jamii,sayansi ya siasa.

Laaa! Mungu aseme na viongozi wetu,
La sivyo
Tutaendelea kuomba ili Mungu atende tena.
Kama mtu amehitimu chuo kikuu halafu hawezi kujiajiri basi huyo siyo msomi bali anaitwa " Aliyekariri"
 
Wakati akilihutubia bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania,rais Samia Suluhu Hassan alisema serikali itaanza kutoa elimu ya itakayomuwezesha msomi kujiajiri.

Maswali haya yafuatayo yatadhibitisha kuwa serikali ni chanzo Cha tatizo hili 100%:

1. Serikali ilikubalije kutumika kwa mtaala huu mashuleni na vyuoni,usiowafanya wasomi wajiajiri?

2. Je,Hawa waaomi ambao tayari wamehitimu ktk mtaala huu ambao una matatizo (hauwafanyi wasomi wajiajiri),wanasaidiwaje?

3. Kuna baadhi ya kozi vyuoni( especially vyuo vikuu), wasomi wanadhaminiwa kwa asilimia mia,je,
Unatoaje udhamini wa asilimia mia huku ukijua msomi huyu akihitimu humpi au hapati ajira?

4. Bado siamini,hivi mfano mtu umesomea kozi zifuatazo,utaweza vipi kujiajiri?

Ualimu, Utawala,Mipango, maendeleo ya jamii,sayansi ya siasa.

Laaa! Mungu aseme na viongozi wetu,
La sivyo
Tutaendelea kuomba ili Mungu atende tena.
Serikali hipi Duniani umewahi kusikia ilimaliza tatizo la ajira likawa 0%?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hawajafunguka tu ufahamu...sasa hv wanavyuo wasifikirie kuajiriwa....
Tatizo ninaloliona mie kwa mitazamo ya wasomi wajiajiri ni kwamba tunakuwa solution za kufuta kuganga njaa baadala ya kuwa na solution za kuleta maendeleo.

Inapelekea wasomi wafanye vitu nje kabisa na taaluma zao. Mfona yule dada ana masters alafu anasifiwa kwa kujiajiri kuendesha bajaj.

Kama kwwli tina nia ya dhati ya kuwa donor country basi hizi fikra zinatakiwa zibadilike lah sivyo tutaendelea kuwa wapokeaji tuu.
 
Ukweli na usemwe... sio Tz tu ajira hakuna...sema sasa Serikali uweke mazingira mazuri ya wahitimu waweze kujiajiri...kusiwe na longolongo

Yaani mambo yabkufanya yapo mengi sana. Hizo kada zote ulizotaja mitaani kuna mishe mob za kufanya .ishu tunataka kufika mapema..hatupendi kuteseka
Mfano kada ya ualimu mishe mob ni zipi ambazo zitamfanya huyu mwalimu ajiajiri???
 
Wakati akilihutubia bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania,rais Samia Suluhu Hassan alisema serikali itaanza kutoa elimu ya itakayomuwezesha msomi kujiajiri.

Maswali haya yafuatayo yatadhibitisha kuwa serikali ni chanzo Cha tatizo hili 100%:

1. Serikali ilikubalije kutumika kwa mtaala huu mashuleni na vyuoni,usiowafanya wasomi wajiajiri?

2. Je,Hawa waaomi ambao tayari wamehitimu ktk mtaala huu ambao una matatizo (hauwafanyi wasomi wajiajiri),wanasaidiwaje?

3. Kuna baadhi ya kozi vyuoni( especially vyuo vikuu), wasomi wanadhaminiwa kwa asilimia mia,je,
Unatoaje udhamini wa asilimia mia huku ukijua msomi huyu akihitimu humpi au hapati ajira?

4. Bado siamini,hivi mfano mtu umesomea kozi zifuatazo,utaweza vipi kujiajiri?

Ualimu, Utawala,Mipango, maendeleo ya jamii,sayansi ya siasa.

Laaa! Mungu aseme na viongozi wetu,
La sivyo
Tutaendelea kuomba ili Mungu atende tena.
He he heee Umofia kwenu
 
Tatizo ninaloliona mie kwa mitazamo ya wasomi wajiajiri ni kwamba tunakuwa solution za kufuta kuganga njaa baadala ya kuwa na solution za kuleta maendeleo.

Inapelekea wasomi wafanye vitu nje kabisa na taaluma zao. Mfona yule dada ana masters alafu anasifiwa kwa kujiajiri kuendesha bajaj.

Kama kwwli tina nia ya dhati ya kuwa donor country basi hizi fikra zinatakiwa zibadilike lah sivyo tutaendelea kuwa wapokeaji tuu.
Ndo hiyo nasemea serikali isaidie wenye maono ya mbali....tusiishie wote kuendesha bajaj...! Mie naona mambo ya kufanya ni mengi ila tu ukiritimba uliopo serikalini unaboa....
 
Jamani tatizo la yote haya ni kupungua uwekezaji kwenye sekta binafsi, jambo ambalo limekuwa kubwa sana kipindi cha mwendazake....rais awe makini sana kwenye kuweka mkwamo kukua kwa sekta binafsi na kujikuta serikali nayo inapumulia mashine kwa kuchukua gawio kutoka kwenye taasisi zake ambazo kimsingi zinatakiwa kutoa huduma zaidi na siyo kufanya biashara. Sekta binafsi kwenye mataifa tajiri yote duniani ndo injini ya uchumi wa nchi na ndo inatoa asilimia kubwa ya ajira......unakuta watu wanaofanya serikalini ni kwa kujitolea zaidi maana sekta binafsi ina maslahi makubwa zaidi...
 
Back
Top Bottom