Wasioamini katika uchawi na ushirikina wana hoja lakini...

Wasioamini katika uchawi na ushirikina wana hoja lakini...

Sasa wewe uliye mkubwa ndo ilikubidi kufafanua siye tulio watoto tukaelewa badala ya kukomea kushangaa tu.!

Anaetaka kueleweshwa haandiki kama ulivyoandika....Usipinge kitu ambacho huna uhakika nacho kama hujaibiwa usiseme hakuna wezi na kama hujarogwa usibishe kuwa hakuna uchawi
 
Hebu tupe darasa kuhusu vibwengo
Vinyama fulani Kama binadamu lakini vifupi sana jamii ya vinyamkera havina madhara bali hupenda kufanya vitimbwi na kutisha watu nyakati za usiku na hasa sehemu za misitu mito mabwawa na sehemu zilizo kimya
 
Anaetaka kueleweshwa haandiki kama ulivyoandika....Usipinge kitu ambacho huna uhakika nacho kama hujaibiwa usiseme hakuna wezi na kama hujarogwa usibishe kuwa hakuna uchawi
Tuliza nafsi,punguza "emotions" tueleweshane vizuri,sijapinga hivyo ulivyovitaja.Tupe kidogo "experience" yako kuhusu hii imani ili tuelewe wote,kuna watu wazima siyo watoto kama udhaniavyo lakini hawana ufahamu na hawajakumbwa na imani hii,kwa hiyo usidhani kila anayeuliza ni mtoto na ameuliza kwa kejeli.!

Umesababisha hata mtoa Uzi aone nimeuliza kwa kejeli wakati nilimaanisha na nilipouliza alinijibu vizuri tu.!
 
Last edited:
Vinyama fulani Kama binadamu lakini vifupi sana jamii ya vinyamkera havina madhara bali hupenda kufanya vitimbwi na kutisha watu nyakati za usiku na hasa sehemu za misitu mito mabwawa na sehemu zilizo kimya
Mkuu hz co hadith za kusadikika
 
Kumuaminisha mtu asiyeamini katika uchawi na ushirikina ni sawa na kumwambia mpagani kuna Mungu halafu usipate upinzani wowote toka kwake lakini wakati huo huo akitumia jina na mambo mengi ya kiimani
 
Uchawi wa kawaida hutumia madawa madawa wakati uchawi wa mapepo na majini mara nyingi hutumia maandishi wanaita uchawi wa kitabu lakini vyovyote iwavyo uchawi una mahusiano na roho mapepo na majini
Mkuu, hivi hayo madawa yapoje? Ni mitishamba au ni vitu gani? Na huwa mechanism yake ipoje kuanzia uandaaji wake hadi kwenye matumizi..naomba ufafanuzi kidogo mkuu...
 
Mkuu, hivi hayo madawa yapoje? Ni mitishamba au ni vitu gani? Na huwa mechanism yake ipoje kuanzia uandaaji wake hadi kwenye matumizi..naomba ufafanuzi kidogo mkuu...
Nipe muda nitarejea nikisahau nikumbushe
 
Shukrani mkuu..uje kabisa na uzi juu ya hilo litatoa mwangaza kwa wengi
Kuna baadhi ya mimea hutumiwa sana na waganga na wachawi mmojawapo ni mkafiri na mandrake plant ngoja nikutafutie picha zake
 
Mkuu, hivi hayo madawa yapoje? Ni mitishamba au ni vitu gani? Na huwa mechanism yake ipoje kuanzia uandaaji wake hadi kwenye matumizi..naomba ufafanuzi kidogo mkuu...
1453750778358.jpg
Hapo kuna ushanga kukuwafu na nazi zilizovunjwa
1453750820170.jpg
angalia katika hivyo kuna mkuki
1453750873458.jpg
fisi hutumiwa sana kama chombo cha usafiri ukiacha ungo fisi ni usafiri wa ardhini kama bus nk wakati ungo ni ndege
1453750954305.jpg
mimea maarufu inayotumiwa sana kwenye ishu za ushirikina
1453750987759.jpg
 
Inakuaje mtu anajilinda dhidi ya Uchawi kupitia Uchawi(Kwa Waganga wa kienyeji)? Je,uchawi kwa uchawi unaweza kupingana,yaani upande mwingine umtakie kheri mawanadamu na upande mwingine umtakie Shari?
Uchawi ni kama majeshi tu ya kawaida Kuna kuzidiana ufundi zana mbinu ujuzi na mikakati
 
Kitu ambacho wengi hatukifahamu ni kwmb, Shetani alipotupwa Ulimwenguni aliachiwa uwezo wake na ilipewa pia mamlaka ya kumchezea mwanadamu ikiwemo kumjaribu.

Ukisoma kitabu cha Ayubu pale mwanzoni utakutana na kisanga cha Shetani kumjaribu Ayubu na alitumia njia za kichawi.

Hata leo wapo wanajiita manabii wanatumia njia za kichawi kufanya miujiza ikiwemo kuponya na kutajirisha. Zote hizi ni kaz ya Shetani.

Pia ningependa kuwajuza jambo jema ambalo mtoa uzi kaligusa.
Ukiwa shabiki wa Simba wa ukweli lazma utawajua wachezaji wa Yanga na mbinu wanazozitumia kuwafunga ninyi, vivyo hivyo kinyume chake.

Ukiegemea kwa Mungu utayajua ya Shetani na ukiegemea kwa Shetani utayajua ya Mungu.
Kujua jambo la upande wa pili si lazma ulifanye lakn linakupa njia na ari ya kupambananalo na kulishinda kama ilivyo kwa Mungu na Shetani kutwa hufanya kampeni.

Huu uzi ni mzuri sana na unaeleweka lakn tu kwa watu wenye uzoefu na maisha kwa maana ya wale walopitia matatizo mengi ya kimaisha.

Kujua mambo ya kichawi ni elimu pia japo inaweza kuwa si rasmi maana haina cheti wala waziri wetu haitambui hi kitu hahahahahaha, lakn nimependa hii mada.

Msojua mtajua tu siku yakiwakuta.
 
Back
Top Bottom