Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 280,836
- 730,307
Mungu ni mwema hata ametuwezesha kuuona mwaka 2016, tuombeane heri katika mwaka huu. Hii ni topic yangu ya kwanza mwaka huu, naomba twende pamoja
Kwenye hizi mada za uchawi ushirikina kumekuwa na upinzani mkubwa sana kuhusu uwepo wa uchawi ushirikina uwepo wake na nguvu yake, wao hawajawahi kuona uchawi na wanasema wako tayari kurogwa ili waweze kuamini
Kwanza uchawi haufanyi kazi kihivyo, uchawi ni kitu cha siri uchawi ni roho ni nguvu isiyoonekana ni kitu kisicho na ithibati za kisayansi au kama sayansi ,lakini hii haiondoi ukweli kama uchawi haupo, kutokuamini katika jambo fulani haukuondoi uhalisia wa uwepo wa jambo husika
Ningekubaliana nao kama wangesema hawaamini katika uwepo wa waganga wa kienyeji na wachawi. Mtu ambaye anaweza kusema haamini katika uchawi na akawa na hoja ni mpagani peke yake, lakini kama wewe unaamini katika Mungu lakini huamini katika uchawi huku ni kujichanganya kulikopitiliza, au hujui unachokiamini na hata maandiko kwenye misahafu huyasomi ukayaelewa
Nilishaulizwa hapa jamvini kuwa hebu nionyeshe uchawi ukoje? Duu..! Nikabaki kinywa wazi
Hivi leo hii ukimuuliza mtu JAMII FORUM ikoje? Hayo majibu utakayoyapata unaweza kubaki na kwikwi, sasa hii ni JF kitu cha wazi kabisa.... Tuna mengi ya kuhoji kabla ya kufikia kuhoji uwepo wa uchawi
Kwahiyo wale wote wasioamini katika uchawi na ushirikina wana hoja lakini wanajichanganya na hawajui jinsi ya kuitetea, warudi wakajipange upya

Last edited by a moderator: