gfsonwin nakubaliana na wewe kabisa. Nilipofunga ndoa nilisema sitasimamia ndoa zaidi ya tatu na mpaka leo zimebaki hizo hizo na namuomba Mungu sana asitokee mwingine kutaka tena nimsimamie ndoa yake maana najiulizaga mambo mengi sana kabla sijakubaliana na suala zima la kusimamia ndoa ya mtu. Ni lazima nimjue mhusika back ground yake nijue wazazi wake na aina ya ndoa ya wazazi wake na na kama ni zile ndoa ambazo kila kukicha ni mgogoro baina ya wazazi hata mimi itanipaa shida sana kusimamia ndoa ya mhusikakaka yangu Mr Rocky usimamizi wa ndoa sio jambo la matani hata kidogo. Tena kwa wale wanaojua maana yake huwa wanakaa na kuanza kusali ili wapate msimamizi wa kuwalea kiriho. Kwangu mimi msimamzi wa ndoa nisawa na baba ama mama wa ubatizo.
Mpaka leo hii sijawah kukubali kumsimamia mtu ndoa kwasababu kila mimi na mwenzangu tukikaa tunaona bado hatuna ule utakatifu Mungu alioukusudia ndani yetu hadi tuweze kumsimamia mtu ndoa.
Baada ya muda sana tuliamua kubadili aina ya maisha yetu na kuona kwamba inabidi tutoke kwenye ukristo wa jina na kwenda kwenye ukristo wa kimatendo, na hapo ndipo siku moja mchungaji alipotufundisha jinsi ambavyo ndoa nyingi zimepita kwenye magumu kisa wasmamizi wao niliogopa sana. Hta hivyo nilimshukuru sana Mungu kwamba sijawah kusimamia ndoa.
ukimchagua msimamizi kisa mnalandana kimo, uzuri shepu imekula kwenu. Zmanai RC walikuwa wanagoma kama wasimamizi sio wanandoa, siku hizi naona wanachakachua kimtindo
Suala la usimamizi wa ndoa kama nilivyosema limebaki fashion mnakutana washkaji hata wengine kwa kuwa wamesikia tuu una ndoa na wao wanakuja kuomba usimamie ndoa zao bila hata kukujua au kujua kama wewe ndoa yako imesimama au imeshikiliwa na uzi wa sindano
Ndo maana hata wale wanandoa wakitofautiana hawawezi kwenda kwa wasimamizi wao wa ndoa maana wanajua kuwa kule ni majanga tuu na kwenyewe
Na ndo maana unakutana na malalamiko kwenye mitandao ya mambo ambayo wasimamizi wa ndoa wangeyamaliza bila kuwafanya wanandoa wajianike kwenye mitandao au vyombo vya habari. Kama umesimamia ndoa zaidi ya kumi huwezi niambia eti unawajua wanandoa wako wote na kuwa ndoa zao zote ni imara na hazina matatizo.
Last edited by a moderator: