kazurikazuri
JF-Expert Member
- Aug 9, 2014
- 237
- 70
Siku hizi tunaangalia tunaoendana nao rangi urefu ili sherehe inoge
Teh teh
Siku hizi tunaangalia tunaoendana nao rangi urefu ili sherehe inoge
ndoa ya jide na Gardner mwana fa ndio alikuwa best man
ukiwa unataka kuoa unatafuta mskmamizi mwenye maadili. ambaye unadhani atakushauri na kukemea uovu wako. tatizo watu wa namna hii hawapo na ukimpata anakua mzee sana au kama ni kijana mwenzio anakwanbia hawezi.
hili tatizo ni supply oriented. hao wasimamizi wenye maadili don't exist kwenye orodha ya watu wa karibu.
Miaka ya nyuma kidogo nilikuwa naona wasimamizi wa ndoa walikuwa wadau muhimu sana katika kurejesha amani ndoani pale kunapokuwa na tatizo
Ila sasa nahisi mambo yamebadilika sana hasa huku mijini. Watu wanachagua wasimamizi washkaji zao na mara nyingi ushkaji huu huwa hadi kwenye issues kama "uchepukaji". Yani unakuta mtu na msimamizi wake ndio wanapeana dili za michepuko mitaani.
Mbaya zaidi baadhi ya wasimamizi wanachepuka na wanandoa wale wale waliosimamia...!!!
Yani hapa hata sijui niulize swali gani...
Changia tu chochote
Mmmmmmmh!
Tuko maana nzima ya mdhamini wa ndoa haipo imeishia kuwa fashion
Maana kuna ndoa nyingine wanaosimamia wenyewe hawana ndoa wamechaguana washkaji wanaofahamiana na yeye mshkaji anaenda kumtafuta mchepuko wake wanasimamia ndoa
Sasa hapo unategemea nini kama sio majanga
Wengine wanachaguana kwa kuwa walisoma wote au ni marafiki kwenye deal wanasimamia ndoa bila kujua maana nzima ya usimamizi wa ndoa
Na kuna wengine ni kama anaona ni jambo la kawaida kusimamia ndoa so unamkuta mtu amesimamia ndoa zaidi ya 20 na unamuuliza hivi katika ndoa zote ulizosimamia unajua wanandoa wako wanaendeleaje au unazikumbuka zote na familia zao wanaendeleaje.
Dhana nzima ya usimamizi wa ndoa imepoteza maana kutokana na hata wasimamizi wenyewe kuwa wahusika kwenye kuongeza idadi ya michepuko au kuchepuka pamoja au kushirikiana katika kutafutiana michepuko
cc gfsonwin, BAK, Tized
Tuliwahi kuombwa na mama mmoja jirani tusimamie ndoa ya mwanae kisa tu eti tunaendana na hao maharusi, tulikataa mpaka tukaletewa wazee kutubembeleza ikabidi tukubali, maharusi wenyewe hatuwajui hawatujui, harusi imeisha kila mtu kivyake, miaka 3 imepita hata hatujui nani yuko wapi na wapi.
Siku hizi haya mambo ni fasheni, tena unakuta bibi harusi anachagua mtu ambaye hatamfunika uzuri, msimazi akiwa mzuri zaidi ya bibi harusi inabidi saluni wasimlembe eti. Vinginenvyo bibi harusi ananuna mpaka harusi inaisha na mikanda ya harusi hakuna kuiangalia.
Haya ndio tunayosema Kanigini yaani mtu anakuambia simamia harusi yangu kwa kuwa mnaendana na maharusi bila kujali au kuelewa dhana nzima ya wasimamizi wa ndoa
Suala limekuwa ni namna mikanda ya video itakavyotokana namna mtakavyopendeza mkisimama pamoja bila kujali kama huyo msimamizi ni mtu haswa anayefaa kuwa msimamizi
Wengine wanakuja kwako bila kujua kama ndoa yako imeshikiliwa kwa uzi inakaribia kukatika au bila kujua kama mna ndoa iliyofungwa au mnaishi kama mke na mume tuu
Sasa hebu fikiria miaka mitatu hamjawahi waona wanandoa mliowasimamia wala hawajawahi kurudi kutoa salam au hata kuwakumbuka wasimamizi wao
Miaka ya nyuma kidogo nilikuwa naona wasimamizi wa ndoa walikuwa wadau muhimu sana katika kurejesha amani ndoani pale kunapokuwa na tatizo
Ila sasa nahisi mambo yamebadilika sana hasa huku mijini. Watu wanachagua wasimamizi washkaji zao na mara nyingi ushkaji huu huwa hadi kwenye issues kama "uchepukaji". Yani unakuta mtu na msimamizi wake ndio wanapeana dili za michepuko mitaani.
Mbaya zaidi baadhi ya wasimamizi wanachepuka na wanandoa wale wale waliosimamia...!!!
Yani hapa hata sijui niulize swali gani...
Changia tu chochote
Kweli kabisa mkuuNdiyo utandawazi wetu, ndiyo maana kila kukicha humu watu wanaleta malalamiko ya ndoa ambayo hayakutakiwa kujadiriwa humu, kama wangeanza na wasimamizi mambo yangemalizika vizuri, lakini utaona JF imekuwa kama ndiyo wasimamizi na washauri wa ndoa.