Wasimamizi wa barabara za mjini liangalieni hili

ZINDAGI

JF-Expert Member
Dec 5, 2015
1,117
1,424
Inashangaza na kuhuzunisha kuona watu waliopewa dhamana ya kuzitunza na kuziangalia barabara zetu hawatendei haki majukumu yao, hii inasababisha matatizo makubwa kwa wateja wao ambao ni sisi sote watumiaji wa barabara hizo.

Utakuta watu wanachimba barabara kuziba viraka au kuchimba mashimo kuziba pipe za maji yanayovuja, kitakocheendelea hapo ni kuachwa kwa mashimo hayo kutokuzibwa na kuletea kuwa mahandaki makubwa au kufinya barabara kunakoletea kuharibu barabara kwa pembeni.

Mfano ni hili shimo lilipo hapa maungano ya barabara ya kutoka Alaf kuingia Nyerere Road, ni wiki ya tatu sasa limechimbwa shimo na kuachwa hivyo hivyo, hali inayoletea usumbufu kwa watumiaji wa barabara hiyo.

Tunawaomba(Ingawa ni wajibu wenu) mje mtuzibie hili shimo, au tunasubiri mkandarasi achaguliwe kuja kuziba shimo moja!!!

Shimo.PNG
 
Back
Top Bottom