Mkulima wa Kuku
JF-Expert Member
- Jan 13, 2011
- 1,270
- 534
Nimefuatilia suala la daraja hili kwa uchache na kugundua kuwa ni restrictive kwa matumizi. Sina hakika iwapo ni kiwango kikubwa cha tozo ya ushuru wa barabara (road toll) au kama kuna sababu nyingine.
Ila nimegundua kuwa ni magari machache sana yanayotumia daraja hili:
1. Ubovu wa barabara -pande zote mbil. Nakumbuka ahadi ya mkuu wa nchi alipokuwa analizindua daraja hili akaahidi itajengwa barabara walau ya upande wa Kigamboni kwa kiwango cha lami kwa dharura. Mpaka leo sioni dalili zozote za ujenzi wa barabara hii kwa udharura uliotajwa. Aidha ukishavuka barabara upande wa kuelekea mjini kuna mashimo makubwa na ya kutisha kwenye barabara ya shimo la udongo. Sina hakika kama serikali inayaona haya au inamuhitaji mheshimiwa Rais kushughulika na mambo haya.
2. Toll inayotozwa bado naona ni kubwa mno ukilinganisha na uwezo wa watumiaji wake. Hakuna daladala yenye uwezo wa kulipia road toll 7,000 au zaidi ili kupitisha gari mara moja wakati wa kurudi unalipa kiasi hichohicho. Aidha kama kumbukumbu zangu ziko sawa nakumbuka malori makubwa yanavuka hadi kwa shs. 100,000/= hivi. Kwa biashara gani itakayomfanya mtu apate fedha hizo zote? Naomba wizara husika isijitoe ufahamu kwenye jambo hili na irudi kwenye uhalisia wa maisha na sababu za uwepo wa daraja.
Nakumbuka daraja liliwekwa ili kupunguza kero kwa wavukaji wa panton zetu. kama bado hiyo ni sababu, basi iko haja kwa serikali kuliangalia suala hili. Ikumbukwe kuwa Tanzania si nchi ya kwanza kulipia ushuru wa barabara kwa hiyo kuwa na viwango vya ajabuajabu kwenye tozo la ushuru wa barabara, ila pia isionekane kuwa kuna nia madhubuti ya kurudisha fedha yote ya ujenzi kwa kipindi kifupi kama nia ilikuwa ni kurekebisha kasoro zilizokuwepo.
Naamini wakubwa wanapitia humu na niwaombe wachukulie serious jambo hili. Chondechonde tuokoleeni maisha yetu watumiaji wa Panton ili na sisi tusijisikie kana kwamba ni wapiga mbizi