ibanezafrica
JF-Expert Member
- Oct 23, 2014
- 7,261
- 6,556
Najiuliza mamlaka zinazohusika na barabara hawalioni hili?mbona ni hatari?askari wetu wa usalama barabarani hawalioni hili wakaliripoti kwa Tanroads au Tarura?
Sehemu nyingi hapa Dar hasa city centre kuna matundu pembezoni mwa barabara yaliyosababishwa na either kuondolewa mifuniko au kubomoka lakini yameachwa hivyo hivyo bila hatua zozote kuchukuliwa kwa muda mrefu.
Kila niyaonapo mashimo haya mimi husimama na kuwaza hivi inakuwaje hawa bodaboda walivyozagaa mjini au hata watembea kwa miguu kwa kutoliona shimo hili inakuwaje pale atakapojikuta katumbukia kwa ghafla?na sina hakika hadi sasa kama hakuna wahanga wa mashimo haya,kwa binadamu au uharibifu kwa vyombo vya moto.
Tuombe mamlaka ikiwa ni Tanroads,au Tarura hebu liangalieni jambo hili na kulitafutia ufumbuzi kwa barabara nyingi katikati ya jiji la Dar na pengine miji mingine.
Hapa nimeweka mfano wa shimo lililopo pembezoni mwa kituo cha mwendokasi shekilango,sasa kuna mengine ni makubwa kiasi cha mtu mzima kuingia na kuzama kabisa,mfano kuna moja au mawili nakumbuka yapo sokoine drive kati ya station na posta ya zamani.
Nawasilisha.
Sent from my SM-A205F using JamiiForums mobile app