Elections 2010 Wasifu wa Dr. Slaa: Download, SAMBAZA!

Status
Not open for further replies.
Naiombea CHADEMA sana kama inaweza kuhakikisha inapata wabunge wa kutosha.... Mungu Ibariki Tanzania.
 
huu ni ujumbe ambao umetoka kwa dr. Slaa, endapo utaupenda basi usambaze kadiri unavyoweza.

kila sehemu na mambo yake , haya angeyafanya michuzi kwa ccm watu wangelimnanga na kumtoa thamani hadi basi, angeambiwa blog ameifanya ccm na yeye anatumika kwa ccm

ama kwa huku kwa ulilolifanya ndugu yetu sio dhambi na thanks za kufa mtu, umehabarisha umeleta habari njema na wala hujalalia upande mwengine. Si watasema ccm na cuf na wengine hawajakutafuta nakukupa mbona ungepewa ungebandika na kuwaachia wasomaji wachangie

mmh usinaban swahiba wangu maana mcha maago hanyele huenda akawiya papo
 
mmh usinaban swahiba wangu maana mcha maago hanyele huenda akawiya papo
=========

watani wamepagawa, sasa wanatapatapa

CHADEMA wameteua, Dakta slaa ulingoni,
CCM kuwatungua, kuwatoa mjengoni,
Uteuzi ulotulia, kama maji mtungini
Watani wamepagawa, sasa wanatapatapa

Slaa chaguo poa, tutakavyo kutimia,
Hakuna wa kutania, wala pua kuitia,
Kazi kwetu kuamua, Oktoba yakaribia,
Kura zote kwa SLAA, ili tupate raha.

Kura zote kwa Slaa, ili tupate raha,
Nchi kaipigania, bila kuwa na staha,
Na mengi katuambia, hakujali majeraha
SLAA chaguo la leo, kwa faida ya milele.

Kumbukeni wajameni, ni yeye alisimama,
Macho yenu fungueni, mwembe yanga kalalama
Yanachotwa mabenkini, mambo huko si salama,
Bila yeye kukemea, mapesa karibu kwisha

Akaenda migodini, akazipiga kelele
Tuachieni madini, msiyapigie misele
Mgawo uwe makini , hatutapiga kelele
Serikali ikabaini,asemacho ni bayana
.

Kama tukipiga kura , SLAA kumkubali,
Tutapata barabara, shule na maji kweli
Yeye atatupa kula, kusaza ugali na wali,
Tumchague Slaa, kama twahitaji raha.
 
Slaa kumfananisha na Nyerere ni upeo mdogo, unaokufanya ufikiri Nyerere alikuwa kiongozi bora ni kipi ? Ni wakati wa utawala wake Ufisadi kila kona au ulikuwa unaishi nchi gani

Kwa taarifa yako Nyerere akiamua kugombea tena uraisi CCM hatopata, kwa sababu watz wanajua wametoka wapi, na kama Mchungaji Slaa unamuona ni sawa na Nyerere umeishiwa na hoja

Kumchagua Mchungaji Slaa kuongoza ni kuirudisha nyuma nchi, Slaa hana sifa ya uongozi, kashindwa kuleta democrasia, utawala bora, kashindwa kuondoa sera za kidini na ukabila ndani ya chadema.

Kwa usalama wa National security, kupewa nchi Slaa ni kuisaliti TZ kwa sababu kawaida ya wakatoliki maamuzi yao yanatolewa toka Vatican.

Slaa atapewa kura na shemeji zake na kabila lake kama anavyoendelea kuomba kura kwa msimamo huo
 
Is one of few people I admire to hear talking about this country's problems and how we can solve them.
He is one of few leaders who was ready to join us here and get our views and tell the public through parliament.
He is a great leader

I too think the same way. It's revolutionary Tanzanians who can see it, and after realizing that make a decision to vote him inn for Presidency.
 
Mkuu hii lugha ya Kichina si ya kimataifa. Sema inazungumzwa na watu wengi walio wachina wenyewe na watu wa Taiwani. Lugha hii ni ngumu sana kujifunza kwa maana haina gramma ya kueleweka. Wako watu wengi wamejaribu kujifunza wakashindwa. Wachina wenyewe sasa wameweka kipaumbele kujifunza kiingereza.

Mkuu chinese (Mandarin) ndo lugha inayozungumzwa na watu wengi duniani kuliko lugha yoyote, just do ur reseach utafahamu hilo. But sio muhimu sana kwa Dr Slaa kujifunza kichina kwani wakalimani tupo
 
mwambie KINANA alete cv ya JK uone kama invisible hataiweka visible hapa jamvini....kama umechukia vile? mbona makampuni yote ya matangazo hapa dar yametoa mabango yote kwa JK na watu tunavumilia tu though yanachefua....hasa ukipita bonde la jangwani! inauma sana PAYE yangu nina wasiwasi imekamata bango moja kubwa sasa hivi..by the way JK hajulikani hadi awe na mabango mengi vile.??wizara zinatundika picha zake kila kona lakini bado hamridhiki tuu?

Kaka fisadi tangu lini akaridhika! fisadi anatamani hata hicho kidogo chako kiwe chake ndo tabia za mabazazi kama CCM, Hawana haya mchana kweupe, aisee!
 
Imeelezwa kuwa mchumba wa Dk Slaa, Josephine Mkatunzi Mushumbusi alifunga ndoa kanisa la KKKT Usharika wa Kijitonyama jijini Dar es Salaam Februari 7, 2002 na Aminiel Chediel ambaye ni mfanyakazi wa Mamlaka ya Bandari (TPA).

KUMBE NI MKE WA MTU.....!
+++++

The difference between Dr. Slaa and Jk is aparent through various way. Even looking at people who support each of them, the difference is crystal clear. Look at the above quote and many others who supports JK! Utadhani wao ndio wake wa JK kwa vile wao sio wake za watu!
 
Ni nani wa kumlaumu, ni Dr Slaa aliyempenda Josephine au Josephine aliyeficha ndoa yake kama ni kweli. Lakini ukianza kuangalia maisha binafsi ya mtu badala ya alichokifanyia jamii unakuwa na wewe umepotea. Kuna nani sasa hivi akawa mtanzania, a nationalist kuliko Slaa katika nchi yetu sasa? Hio haitoshi tu!
 
Slaa kumfananisha na Nyerere ni upeo mdogo, unaokufanya ufikiri Nyerere alikuwa kiongozi bora ni kipi ? Ni wakati wa utawala wake Ufisadi kila kona au ulikuwa unaishi nchi gani

Kwa taarifa yako Nyerere akiamua kugombea tena uraisi CCM hatopata, kwa sababu watz wanajua wametoka wapi, na kama Mchungaji Slaa unamuona ni sawa na Nyerere umeishiwa na hoja

Kumchagua Mchungaji Slaa kuongoza ni kuirudisha nyuma nchi, Slaa hana sifa ya uongozi, kashindwa kuleta democrasia, utawala bora, kashindwa kuondoa sera za kidini na ukabila ndani ya chadema.

Kwa usalama wa National security, kupewa nchi Slaa ni kuisaliti TZ kwa sababu kawaida ya wakatoliki maamuzi yao yanatolewa toka Vatican.

Slaa atapewa kura na shemeji zake na kabila lake kama anavyoendelea kuomba kura kwa msimamo huo

Kumbe wewe ni mdini wa kutupwa! Ulikuwepo kweli wakati wa utawala wa Nyerere? Unafikiri kwa nini pamoja na matatizo yale makubwa ya uchumi bado Nyerere anakumbuka na wala sio hapa bali Duniani? Alikuwa na principles ambazo hakuzipinda, alikuwa na mwelekeo na itikadi ambayo aliamini licha ya maadui wengi wa nchi za magharibi kuupinga, alifanikisha mambo mengi na kuhakikisha raslimali yetu inalindwa kwa vizazi vyetu, na ndio leo hii mimi na wewe tunataka yale madini yetu yachimbwe kwa mkataba wa kutunufaisha. Kwa maneno yake wakati ule anafuta mfumo wa kuhoji ardhi kwa njia ya kikabwela (freehold titles), alisema angeruhusu hayo, watanzania wengi wangefanywa watumwa/vitwana kwenye ardhi yake. Na tumeona ukweli huo.....angalia yanayofanywa na wanaotaka kulima jatropha kule Kisarawe!

Kwa nini napoteza muda wangu kukuelewesha najua hutapenda kujifunza maana umekwishaingiwa na dudu baya IMANI!
 
Bila Nyerere hata Kikwete asingesoma na hata leo Kikwete anaweza kukebehi mengine siyo Nyerere, japo pia tunajua anamsanifu maana siku hizi naye kalambishwa unga wa ufisadi.

Kwa taarifa yako Bull, hata nchi za Magharibi zinatumia sera zile zile za Nyerere kuufanya ubepari wao uheshimike, ndo maana kuna food stamps, kuna free housing kwa maskini, kuna elimu bure kwa maskini, medicare, medicaid, n.k. Huo wote ni ujamaa wa Nyerere wa kuwajali watu maskini.

Kama Slaa anaongozwa na Wakatoliki, basi, huyo unayemshabikia ataongozwa kutoka misikitini na mifano tunayo.
 
Asante sana kujua kama wakati wa Nyerere tulikuwa na hali mbaya ya Maisha,

nakama unazungumzia sifa ya Nyerere kwa sababu watu wanamkumbuka, nakuomba ufahamu kitu kimoja kuwa, mtu anaweza kukumbukwa kwa ubaya pia, kama vile hitla na N.K. kweli alikuwa na pricipal ambazo hazukuwa na maslai na nchi bali kwa yeye mwenyewe.
Nyerere alikuwa kiongozi asieambilika hata kutoka kwa wataalam na ndio maana aliifikisha nchi alipoifikisha mwishowe akaikimbia.

Nyerere alikuwa kwenye position zuri ya ku-negotiate jinsi ya kuzitumia rasilimali zetu vizuri, lakini kwa sababu hakuwa anaambilika kaiacha nchi maskikini

Je, viongozi wote waliopita waseme tuachie rasilimali zetu kwa vizazi vijavyo, tungeendelea hivyo mpakalini ?
someone must make decisition now ilitufaidike na raslmali zetu, hatuwezi kusubiri vizazi vijavyo, huu ni moja ya udhaifu aliokuwa nao Nyerere.

Mimi na- analys issues politicaly na econmcly, Kwenye mambo ya udini nakuachia mwenyewe.
 
Ni Dr Slaa anayeweza kuwapa elimu ya bure watoto wetu pale mlimani.

Waulize mpango wao ccm kama si kuwapa wahindi wanaoleta mabehewa ambayo mababu zetu walitumia wakati wa ukoloni. Sasa wahindi wanabaki kutudanganya na bajaji wakati vyuma chakavu vya reli sasa vinatumika kujenga vyoo.

Uchumi unadidimia kwa kasi. Ahadi nyingine za uongo lukuki zinatolewa tena, wakati zile tulizoahidiwa mwaka 2005, hata moja haijatekelezwa.

Si tumeona mnazi mmoja alivyowataja mafisadi wote!

Angalizo:

Ahadi ya Dr. Slaa na CHADEMA ni Elimu bure hadi kidato cha Sita na si Chuo Kikuu (Mlimani). Free hadi Mlimani ni CUF.

Kutaja "Wahindi" sounds ubaguzi. Simply say wawekezaji wabovu wasio na uwezo. wako wengi hawa: Wazungu, Waasia, na hata Waafrika.

Si kweli ahadi za 2005 za CCM hazijatekelezwa, baadhi zimetekelezwa. Ila Maisha Bora kwa kila Mtanzania haijatimia.

Mafisadi 11 hawakutajwa Mnazi Mmoja, ilikuwa Mwembe Yanga Temeke.

Hayo machache ni kuweka records sawa tu. Mengine yako poa.
 
Bila Nyerere hata Kikwete asingesoma na hata leo Kikwete anaweza kukebehi mengine siyo Nyerere, japo pia tunajua anamsanifu maana siku hizi naye kalambishwa unga wa ufisadi.

Kwa taarifa yako Bull, hata nchi za Magharibi zinatumia sera zile zile za Nyerere kuufanya ubepari wao uheshimike, ndo maana kuna food stamps, kuna free housing kwa maskini, kuna elimu bure kwa maskini, medicare, medicaid, n.k. Huo wote ni ujamaa wa Nyerere wa kuwajali watu maskini.

Kama Slaa anaongozwa na Wakatoliki, basi, huyo unayemshabikia ataongozwa kutoka misikitini na mifano tunayo.

Mbona kuna watu wengi tu walisoma kabla ya Nyerere? na kabla ya Nyerere yeye mwenyewe Nyerere alisoma wapi, hizi zako zinafanana na hoja za Makamba!!

Nadhani huzielewi vizuri sera za magharibi, ndo maana unazifananisha na za Nyerere zilizo mshinda, kumbuka wao walimshauri Nyerere kuachana na sera zake alizoshindwa kuzisimamia, kwa hiyo kumbuka zilikuwa sera mbili tafauti na wakati huo wanamshauri pia nchi zao hao wazungu walikuwa wanatoa free Schoo, medical, benefit, etc

Wakatoliki wanaasili ya Centralised command ambayo misikini hakuna, tuliwaona viongozi wengi walivyoongozwa toka Vartican, kwa hiyo nchi yetu kamwe ahtutoisaliti kwa Slaa na Network yake,,,,Asante,,,
 
Angalizo:
Si kweli ahadi za 2005 za CCM hazijatekelezwa, baadhi zimetekelezwa. Ila Maisha Bora kwa kila Mtanzania haijatimia.

.
Mtanzania wa kweli atatafuta maisha bora mwenyewe, badala ya kusubiri kuletewa maisha hayo nyumbani kwake
 
ça c'est bon CV, Allez-y Docteur pour conduire notre pays.

Hapo vipi?
 
Ok dr padri slaa amelelewa vema na kanisa katoliki elimu yake yote ameipata seminari na rome makao ya papa mpaka amefikia kuwa padri... Laiti kama shejkh mussa kundecha angegombea basi mchuano ndio ungekuwa nguvu sawa padri v/ sheikh....lakini kikwete ni mwana siasa hawezi kushindana nae....katika masuala ya kuongoza nchi yenye makundi mawili yasio aminiana hata kidogo..huu ndio ukweli

wana jf muelewe kitu kimoja si rahisi upande mwengine wa jamii ya watanzania kumwamini na kumchagua kiongozi wa dini au hata kama alikua kiongozi wa dini kuwa rais wa nchi hii....sio rahisi....na si rahisi kutenda haki kwa makundi yote.....mkapa na kikwete wote walichaguliwa kwa kura nyingi sana kwa sababu wao ni wana siasa .hata sheikh ama padri akiwa mfano mbunge bado uamuzi wake unakuwa unaegemea upande wake....
Bado hamuja chelewa.... 2015 chagueni vema...pangeni safu yenu ionekane ya kitaifa zaidi....muwe na uongozi ulo jikita kila sehemu....na sio ionekane kila mkoa viongozi wanatoka sehemu moja ya nchi.....pia tuhuma zilizo andikwa kwenye kitabu cha wangwe kwamba viongozi wengi ni waku toka sehemu moja ila mbinu imetumika ya kuficha majina ili kuficha ukweli ..hii haileti picha nzuri...watanzania si wajinga ni werevu wa siasa .....
Tumieni nguve zenu kupata wabunge wengi.....urais kwa ukweli mume fulia na kufanya ya kosa la kimkakati..
 
Ni nani wa kumlaumu, ni Dr Slaa aliyempenda Josephine au Josephine aliyeficha ndoa yake kama ni kweli. Lakini ukianza kuangalia maisha binafsi ya mtu badala ya alichokifanyia jamii unakuwa na wewe umepotea. Kuna nani sasa hivi akawa mtanzania, a nationalist kuliko Slaa katika nchi yetu sasa? Hio haitoshi tu!

sisi unationalist tu hata udini kampita PAULO, huyu safi tungekuwa tunachagua papa angetufaaa, hata hilo la kuchukua mke wa mtu tungemsamehe.
 
Huu ni ujumbe ambao umetoka kwa Dr. Slaa, endapo utaupenda basi usambaze kadiri unavyoweza.

5. Vitabu alivyoandika
 Utimilifu wa Msichana (1977)
 Utimilifu wa Mvulana (1977)
 Expediency and exigency Liturgical Legislation (1981)

Mwandishi wa kweli anaandika kile anachokiamini na kukichukia na ndipo inapoonekana taswira ya ndani ya mwandishi! Wapigania uhuru wengi waliandika vitabu kuhusu harakati za ukombozi na mambo mengine kama hayo! Nchi hii ufisadi haujaanza leo, na Dokta Slaa anajipambanua kama mpinga vita ufisadi!! Inakuwaje hana andiko katika kitu anachokichukia?
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom