Elections 2010 Wasifu wa Dr. Slaa: Download, SAMBAZA!

Status
Not open for further replies.
Is one of few people I admire to hear talking about this country's problems and how we can solve them.
He is one of few leaders who was ready to join us here and get our views and tell the public through parliament.
He is a great leader
 
Watu mliosoma madrasa mnastmbua sana.utapataje PhD bila degre za BA na MA? Pia mjue hakuna kitu kinaitwa degree za kanisa.ila degree zimetolewa ktk vyuo vinavyomilikiwa na kanisa.vinatambulika na vinaheshimika kote duniani.vyuo kama st.johns university USA,chuo kkuu cha bologna italy nk. Hata chuo kikuu maarufu kuliko vyote duniani cha Havard ni cha walutheri,degree wanazotoa ni za vyuo siyo makanisa.
 
Vyama venye ufa kama CHADEMA,hatuwezi kuvipa kura ya kuongoza nchi kwa sababu kama tukivipa kura na vikapata ushindi, kazi yoa ya kwanza itakuwa ni kutatua matatizo na migogoro yao badala ya kutatua matatizo ya wananchi (wapiga kura)

Childish!
 
Kibs, Kibs, Kibs.... Hiyo ni sifa bana. Kutokubaliana kisha kung'atuka kutoka kwenye mfumo hiyo ni positive endeavour, haswa kwenye siasa!
Maelezo yake katika ulingo wa siasa yana walakini. Ilimpasa kuitaja CCM ambako ndipo alipoanzia siasa. Kusema kwamba yupo kwenye siasa kwa muda wa miaka 15, ni uongo.
 
Asante mkuu tayari nimeshasambaza kwa watu wangu wa karibu watano, ila nimeshangaa kwenye ufasaha wa lugha ni kipaji au kitu gani tena amesahau lugha ya tisa ya Ki-Mbulu.



9. Kimbulu
katika dunia ya sasa huwezi taja lugha ya kimataifa uache Kichina..........Je ni muhimu Dr. ajifunze????????
 
umoja wa mataifa wakiipata hii CV watatushangaa watanzania tukishindwa kumuingiza ikulu kwa wingi wa kura
 
Katika mambo ya kuyapa kipaumbele katika serikali yake amesahau mambo kadhaa muhimu sana kwa mfano kuwapa watanzania umeme wa uhakika utakaoharakisha maendeleo ya nchi. Kutangua mikataba mibovu inayoinyonya TANESCO na kufanya bei ya umeme kuwa juu, kuendeleza jitihada za Mkapa za ujenzi wa barabara katika mikoa ambayo haina barabra nzuri, kuhakikisha rasilimali zetu e.g madini na vivutio vya utalii (mbuga za wanyama, Mlima Kilimanjrao n.k) vinatumika ipasavyo katika kukuza uchumi wa nchi n.k.
Naomba kutoa hoja.
 
katika dunia ya sasa huwezi taja lugha ya kimataifa uache Kichina..........Je ni muhimu Dr. ajifunze????????

Mkuu hii lugha ya Kichina si ya kimataifa. Sema inazungumzwa na watu wengi walio wachina wenyewe na watu wa Taiwani. Lugha hii ni ngumu sana kujifunza kwa maana haina gramma ya kueleweka. Wako watu wengi wamejaribu kujifunza wakashindwa. Wachina wenyewe sasa wameweka kipaumbele kujifunza kiingereza.
 
Kwenye uzoefu wake kiasiasa, kasahau kuandika alivyopigwa chini na CCM hadi kuamia chadema
kuinuliwa
labda kama unatania....lakini kama uko serious inawezekana huna CV au hujawahi kuandika CV na inawezekana hujui kazi yake.....au ndo nyie manao vuna sasa hivi mzitumia mpaka uchaguzi ujao?...kwenye CV huwezi ukaandika failure point zako simply bCoz failure zingine in turn zinakuuplift so unashikilia kule kuinuliwa na sio kule ulikojaribu kuangukia...angechaguliwa na CHICHIEM wakati ule angekuwa na mawazo mgando kama madk na maprof mlionao huko CHICHIEM...prof mzima anaongoza wizara itundike bango kumsifia JK kuwa anajali watoto kwa kuwapakata na kuwa anajali walemavu kwa kuchungulia ulemavu wao....so sad unajua...mabango ya wizara moja yamejaa mjini hapa yananikera mimi...nwayz our days r coming soon or later we'll c changes in ourbongoland.
 
Katika mambo ya kuyapa kipaumbele katika serikali yake amesahau mambo kadhaa muhimu sana kwa mfano kuwapa watanzania umeme wa uhakika utakaoharakisha maendeleo ya nchi. Kutangua mikataba mibovu inayoinyonya TANESCO na kufanya bei ya umeme kuwa juu, kuendeleza jitihada za Mkapa za ujenzi wa barabara katika mikoa ambayo haina barabra nzuri, kuhakikisha rasilimali zetu e.g madini na vivutio vya utalii (mbuga za wanyama, Mlima Kilimanjrao n.k) vinatumika ipasavyo katika kukuza uchumi wa nchi n.k.
Naomba kutoa hoja.
maadili, uadilifu, umakini na uwajibikaji......kwenye haya maneno kila kitu kiko covered bro/sisy.
ukichambua kimojakimoja hapo unaweza kupata page40 na zaidi.....kwa kifupi hana sababu ya kuongea sana ukishawabana hawa mafiSadi Tz ina kila kitu...maendeleo kwenye nyanja zote ni veri posibo.....ungana nasi kwa pamoja tutashinda.
 
Mimi nimetumiwa tu katika e-mail yangu, nimependa kuwashirikisha mambo haya kama kawaida yetu wana JF. Karibuni!

Mtanzania yeyote Mzalendo wa kweli, mwenye akili timamu, asiye na mtindio wa ubongo, wala mtumwa wa hila chafu, wala udumavu wa kiakili, tena asiye na utando wa buibui wala tongotongo za ufisadi machoni, wala asiye mzembe wa kufikiri, anaalikwa asome kwa uangalifu na azingatie makala hii na awashirikishe ndugu, jamaa na marafiki zake popote pale walipo..

Dr Slaa yes we can! Huyu ni mtanzania wa pili baada ya Nyerere kuchukia ufisadi kwa vitendo. Ni mtanzania wa pili kuchukia umaskini wa watanzania kwa vitendo. Ni Dr. Slaa aliyesimama na kutaja majina ya wala rushwa na mafisadi. Akataka wale wanaopinga wampeleke mahakamani. Hakuna aliyethubutu kujitokeza kumpeleka mahakamani.

Ni Dr. Slaa aliyesimama bungeni kuomba posho za wabunge kupungzwa kuzielekeza zaidi kwa watanzania maskini. Ni Dr Slaa aliyesimama bila woga kunyosha vidole kwa matumizi mabaya ya ofisi za umma. Ni Dr Slaa amekuwa mtanzania baada ya Nyerere kutoa hoja za nguvu zinazomlenga kumkomboa mtanzania maskini. Maisha bora kwa kila mtanzania yako wapi? Ajira milioni moja ziko wapi? Hebu mwenye mbavu za kujibu swali hili ajibu bila unafiki!

Ni Dr Slaa anayeweza kudhibiti matumizi mabaya ya ofisi za umma. Ni Dr Slaa anayeweza kuwapa elimu ya bure watoto wetu pale mlimani. Achana na longolongo za CCM kuwatoza ushuru watoto. Waulizeni majukwaani wao Nyerere aliwatoza ada? Kama si kutaka watanzania waendelee kuwa mambumbumbu ni nini? kama si kutaka watanzania tuendeleee kuwa watumwa ni nini?

Ni Dr. Slaa anayeongelea treni ya umeme kwenda Kigoma, Dodoma, Tabora, na Mwanza. Waulize mpango wao ccm kama si kuwapa wahindi wanaoleta mabehewa ambayo mababu zetu walitumia wakati wa ukoloni. Sasa wahindi wanabaki kutudanganya na bajaji wakati vyuma chakavu vya reli sasa vinatumika kujenga vyoo. Hawa hawatutakii mema. Hawana tofauti na akina Carl Peters.

Ni Dr Slaa anayeongelea mfumko wa bei -nani hajajua dola leo hii ni sawa na tsh 1500. Uchumi unadidimia kwa kasi. Ahadi nyingine za uongo lukuki zinatolewa tena, wakati zile tulizoahidiwa mwaka 2005, hata moja haijatekelezwa. Watanzania walio wengi na hasa wa vijijini, wamelala usingizi. Wanafumbuliwa macho, lakini wamesinzia bado! Wanatabasamu, wanachekelea na kuridhika na vitisheti vya kijani na vikofia za njano. Wamekwishazoea shida kiasi kwamba wanadhani ni sehemu ya maisha yao. Ee mwenyezi Mungu, tunusuru na hili balaa..

Ni Dr.Slaa anaweza kuzuia wizi wa matrilion ya pesa kutoka migodi yetu ya Buzwagi, Geita, Bulyankulu, Buhemba, Nyamongo, Tulawaka, Nzega na Tanzanite. CCM wameshindwa kwa sababu ni washirka wakubwa na wameruhusu wizi huo. Ni Dr Slaa anaeweza kuwalipa wafanyakazi zaidi ya shilingi 350.000 achana na CCM ambayo imeshindwa kusimamia maliasili ambazo zingeliwapa wafanyakazi kima cha chini kinachokidhi mahitaji yao.

Ni Dr.Slaa anayeweza kusimamia mashirika ya umma kuleta tija achana na CCM wanaofyonza michango yetu kule, kwani haya mashirika yameshindwa nini kuwajengea nyumba wanachama wake? Mbona kwingine yameweza? Ni Dr.Slaa anayeweza kuongoza nchi bila woga, kwa utawala wa kweli wa sheria bila kuwaonea watu wala bila kulipiza visasi.

Ni Dr. Slaa ambaye amepanga kubadili katiba ili Rais afuate matakwa ya walio mwajiri ambao ni wananchi. Waulize CCM hata kama mtu kaiba anapewa mda arudishe pesa. Hivi inaingia akilini kweli? Utawala wa sheria uko wapi? Naomba niwape heko ITV kwa kuturejeshe kwenye hotuba za mwalimu. Katika hotuba yake moja alisema waziri mmoja kule uingereza aliandikwa kidogo tu gazetini juu ya kashfa, yule waziri alijiuzulu na waziri mkuu hata hakumjibu bali aliteua mtu mwingine.

CCM hawawezi hayo? Eti wanataka ushahidi. Nani kawambia rushwa tule wawili harafu tutoe vielelezo? Tunaiona rushwa kwa matokeo yake. Matengenezo ya barabara ya bilion 200, baada ya siku mbili imeharibika. Kwanini usimfukuze waziri na katibu wake wa wizara kwanza? CCM hawawezi! eti wanataka vielelezo!

Ni Dr Slaa anayeweza kufanya hayo. Si tumeona mnazi mmoja alivyowataja mafisadi wote! hapo akiwa ni mbunge tu! Je akiwa rais si watakimbia nchi? Jamani nawambia tumpe miaka mitano tu awakurupushe muone moto utakavyowaka.. Tutapata dawa, tutapata shule za bure, tutapata madawati. Jamani hivi kweli karne ya leo watoto wanasoma wamekaa chini? we must be serious! Hivi kweli dunia ya leo watu wanavuliwa nguo njiani kwenda Mwanza, Shinyanaga, Tabora, Kigoma, Mbeya, Lindi na Mtwara kwa sababu ya usafiri wa malori?

Nani asiye jua madaktari wetu wengi bingwa wapo botswana kwa sababu ya maisha duni Tanzania na hivi kwenda kutafuta maisha bora wakati hapa kwetu wananchi maskini wanakufa bila madawa? Nani asiyejua matatizo ya umeme, maji, makazi, maradhi, yanavyotutesa? Nani asiyejua wakulima wetu wasivyokuwa na masoko ya mazao yao? Nani asiejua asilimia 85 ya watanzania wanatumia vibatari au makoroboi kama mwanga? nani asiejua tunavyonyonywa na hawa wakoloni waliokuja kuchukua kila kitu??

Jamani wafanyakazi, wakulima, na wanafunzi, kwa nini mnalala usingizi? Kwa nini mnapiga miayo ya njaa wakati maghala yetu yamejaa nafaka? Ni akili gani hii? Nchi yetu inazo raslimali za kututosha, lakini wanaozifaidi ni vibaka wachache. Mtalala hadi lini?

Ni Dr Slaa mzalendo wa kweli, na sio kwa ajili ya sifa, anaweza kutuvusha tulipo. Nchi hii ni maskini na umaskini wenyewe ni wa kujitakia. Tanzania ni tajiri tuna kila kitu - mito, maziwa, national parks, migodi, mazao ya misitu, na kila aina ya utajiri. Lakini tuko maskini wa kutupwa! Naona huruma na umaskini wa kifikra wa watanzania.

Hivi kuna mtu hajui mapolisi wanalala kwenye vibanda vya mabati? Hivi kuna ambao hawajui mapolisi watendaji wanalipwa laki moja? Wamekosa nini hawa? Ni ajabu! pamoja na laki yao moja utakuta bado wanatumika kuwanyanyasa watetezi wao. Hata maaskari amkeni hiyo laki moja yenu haina tija hadi mrubuniwe kuwanyanyasa wapinzani ambao kimsingi wanawatetea ninyi! Hivi maaskari mnayo macho ya kuona? Jamani tuache woga inawezekana! Mbona Kenya wameweza? Mbona malawi wameweza?Mbona zimbabwe wameweza? Mbona Ghana wameweza? Kufanya mabadiliko sahihi, inawezakana na nafasi ni hii tuitumie.

Tumtume Dr Slaa atukurupushie wezi wote na atuwekee katiba sawa. Huo ndio msingi wa yote. Ni Dr. Slaa asiyeogopa kuwepo na mgombea binafsi. CCM hili hawaliwezi. Wamelipinga hadi mahakamani. Wanataka wao tu ndio waendelee kututawala na kutunyonya.

Jamani 2010 hakuna kudanganyika! enough is enough. Acheni kudanganyika. Wakati ndio huu. Watanzania msipoamua sasa, mtamlaumu nani tena? Nawatamani watu wa kule Mara -hakuna kura inaibiwa. Zote zinasimamiwa. Tukibadilika inawezekana, tena ni rahisi. Peleke ujumbe huu kwa marafiki, ndugu, jamaa, babu na bibi yako kule kijiji ambako wanadhani bado Nyerere ndiye rais wa nchi hii. Peleka ujumbe huu haraka kwa simu kama ipo, au kwa njia ya posta, mradi tu wale jamaa waliochoka kuishi wasiikwapue barua wakidhani ni hela..

======= M W I S H O ==========

NB: Comment yangu mimi 'poster': Kuhusu ITV, siwaungi mkono moja kwa moja kwani nao ni wazungukaji, wanatuzunguka katika baadhi ya habari, si waungwana.
 
JF/CHADEMA @ WORK........mkiambiwa mnakataa......!
jmiiforums ni mtanda wa CHADEMA..........(?)
 
kuinuliwa
labda kama unatania....lakini kama uko serious inawezekana huna CV au hujawahi kuandika CV na inawezekana hujui kazi yake.....au ndo nyie manao vuna sasa hivi mzitumia mpaka uchaguzi ujao?...kwenye CV huwezi ukaandika failure point zako simply bCoz failure zingine in turn zinakuuplift so unashikilia kule kuinuliwa na sio kule ulikojaribu kuangukia...angechaguliwa na CHICHIEM wakati ule angekuwa na mawazo mgando kama madk na maprof mlionao huko CHICHIEM...prof mzima anaongoza wizara itundike bango kumsifia JK kuwa anajali watoto kwa kuwapakata na kuwa anajali walemavu kwa kuchungulia ulemavu wao....so sad unajua...mabango ya wizara moja yamejaa mjini hapa yananikera mimi...nwayz our days r coming soon or later we'll c changes in ourbongoland.
Ainisha uzoefu wa slaa kwenye siasa... sio blah blah zisizokuwa na mwanzo wala mwisho.

Kwa slaa kusema yupo kwenye siasa kwa miaka 15, ni uongo ulio wazi
 
Huyu ameamua kumwaga radhi kwa kusema ukweli mtu. Nimwongezee sumuni:
-Ni Dr. Slaa tu aliyesema mishahara ya wabunge ni mikubwa kulinganisha na umaskini wa watanzania, sawa na Nyerere alivyopunguza mishahara akianza na wa kwake mwaka 1966, akijibu maandamano ya wanafunzi wa chuo kikuu, waliokuwa wanagoma kwenda JKT.
 
JF/CHADEMA @ WORK........mkiambiwa mnakataa......!
jmiiforums ni mtanda wa CHADEMA..........(?)
mwambie KINANA alete cv ya JK uone kama invisible hataiweka visible hapa jamvini....kama umechukia vile? mbona makampuni yote ya matangazo hapa dar yametoa mabango yote kwa JK na watu tunavumilia tu though yanachefua....hasa ukipita bonde la jangwani! inauma sana PAYE yangu nina wasiwasi imekamata bango moja kubwa sasa hivi..by the way JK hajulikani hadi awe na mabango mengi vile.??wizara zinatundika picha zake kila kona lakini bado hamridhiki tuu?
 
mwambie KINANA alete cv ya JK uone kama invisible hataiweka visible hapa jamvini....kama umechukia vile? mbona makampuni yote ya matangazo hapa dar yametoa mabango yote kwa JK na watu tunavumilia tu though yanachefua....hasa ukipita bonde la jangwani! inauma sana PAYE yangu nina wasiwasi imekamata bango moja kubwa sasa hivi..by the way JK hajulikani hadi awe na mabango mengi vile.??wizara zinatundika picha zake kila kona lakini bado hamridhiki tuu?
Cv ya JK mbona ipo kitambo sana hapa JF, hayo mabango ndio kampeni mkuu...! Zaidi ya mabango kampeni ya mwaka huu kwa CCM ni nyumba kwa nyumba. Mabalozi wa nyumba kumi kumi wapo kazini tena.
 
Umeshafika na utaendelea kuwafikia walengwa wwengine ambao ni watanzania wote.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom