Wasifu (CV) ya Dr. John Pombe Magufuli

he is typically a teacher. Bt he is doing good, he shows patriotic bt as teachers are, he ended up impregnating a geology student udsm.
University students are in an age that allows them to make free decisions unlike those in primaries.Talking of that is just another shit.
 
FRIDAY, JULY 22, 2016
WASIFU WA DKT. JOHN POMBE JOSEPH MAGUFULI



WASIFU WA DKT. JOHN POMBE JOSEPH MAGUFULI


1.0. MAISHA YAKE

Ndugu John Pombe Joseph Magufuli alizaliwa Oktoba 29, mwaka 1959 katika kijiji cha Chato, Wilayani Biharamulo katika Mkoa wa Kagera. Hivi sasa Chato ni Wilaya katika Mkoa wa Geita. Ndugu Magufuli ni Daktari wa Falsafa (PhD) ya Kemia. Ana mke na watoto saba. Alichaguliwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mwezi Oktoba, 2015 kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (C.C.M). Aliapishwa na kuanza rasmi majukumu yake ya kuiongoza Tanzania tarehe 5 Novemba, 2015.

Tangu ameingia madarakani, Rais Dkt. Magufuli, ameonesha kuwa ana sifa zote muhimu za uongozi. Ana dira, maono na malengo kuhusu anakotaka Taifa liende. Ana mikakati ya kutekeleza dira na maono yake. Haogopi kufanya maamuzi makini. Ana kiu ya kuona Taifa linapata maendeleo. Amejipambanua kuwa yeye ni mtetezi wa wanyonge na dhamira yake kubwa ni kuona wananchi wanapata huduma bora za jamii na kero zao zinaondoka.

2.0. ELIMU NA MAFUNZO

Rais Dkt. Magufuli alianza elimu ya msingi katika Shule ya msingi Chato mwaka 1967 na kumaliza mwaka 1974. Mwaka 1975 alianza masomo ya sekondari katika Shule ya Seminari ya Katoke Mkoani Kagera. Mwaka 1977 alihamia shule ya sekondari ya Lake iliyopo Mkoani Mwanza na kuhitimu kidato cha Nne mwaka 1978. Kuanzia mwaka 1979 hadi 1981 alifanya masomo ya kidato cha Tano na Sita katika shule ya Sekondari ya Mkwawa Mkoa wa Iringa .

Mwaka 1981 hadi 1982 alisoma Chuo cha Ualimu Mkwawa na kuhitimu Stashahada ya Ualimu ya Masomo ya Kemia na Hisabati. Mwezi Julai hadi Disemba mwaka 1983, Dkt. Magufuli alipata mafunzo ya kijeshi katika Jeshi la kujenga Taifa kikosi cha Makutupora mkoa wa Dodoma. Mwezi Januari hadi Machi 1984 alihamishiwa kikosi cha mafunzo Jeshi la Kujenga Taifa Makuyuni, Arusha. Mwezi huo wa Machi alihamia kikosi cha Jeshi la Kujenga Taifa Mpwapwa Dodoma na kumaliza mafunzo mwezi Juni 1984.

Mwaka 1985 alijiunga na Chuo Kikuu cha Dar es salaam kusoma Shahada ya kwanza ya Sayansi na Ualimu akijikita katika masomo ya Kemia na Hisabati. Alitunukiwa Shahada hiyo mwaka 1988. Mwaka 1991 hadi 1994 alisoma na kutunukiwa Shahada ya Uzamili katika fani ya Kemia iliyotolewa na Chuo Kikuu cha Dar es salaam na Chuo Kikuu cha Salford cha Uingereza. Mwaka 2006 alijiunga na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwa ajili ya Shahada ya Uzamivu katika Fani ya Kemia na kufanikiwa kuhitimu mwaka 2009.

3.0. UZOEFU WA NDANI YA SERIKALI

Baada ya kuhitimu masomo yake ya Stashahada ya Ualimu, mwaka 1982 hadi 1983 Dkt. Magufuli alikuwa Mwalimu katika shule ya Sekondari ya Sengerema iliyopo Mkoani Mwanza akifundisha masomo ya Kemia na Hisabati. Mwaka 1989 alijiunga na Chama Cha Ushirika cha Nyanza Mkoani Mwanza, ambapo alifanya kazi kama Mkemia Mkuu hadi mwaka 1995.

Mwaka 1995 alichaguliwa kuwa Mbunge wa Jimbo la Biharamulo Mashariki Mkoa wa Kagera. Baada ya Uchaguzi, Rais wa Awamu ya Tatu, Mheshimiwa Benjamin William Mkapa alimteua kuwa Naibu Waziri wa Wizara ya Ujenzi nafasi ambayo aliitumikia hadi mwaka 2000. Mwaka 2000 alichaguliwa kwa mara ya pili kuwa Mbunge wa Jimbo la Biharamulo Mashariki lakini mara hii akipita bila kupingwa. Mwaka huo huo aliteuliwa kuwa Waziri kamili wa Wizara ya Ujenzi hadi mwaka 2005.

Mwaka 2005 Rais Dkt. Magufuli alichaguliwa kwa mara ya tatu kuwa mbunge wa jimbo la Biharamulo Mashariki, kwa mara nyingine akipita bila kupingwa. Baada ya uchaguzi, Rais wa Awamu ya Nne, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete alimteua kuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kuanzia mwaka 2005 hadi mwaka 2008 ambapo alihamishiwa Wizara ya Mifugo na Maendeleo ya Uvuvi hadi hadi mwaka 2010.

Mwaka 2010 Dkt. Magufuli alichaguliwa kwa mara ya nne kuwa Mbunge lakini, kufuatia mgawanyo wa majimbo uliofanyika, mara hii katika Jimbo jipya la Chato. Baada ya uchaguzi, aliteuliwa kuwa Waziri wa Ujenzi kuanzia mwaka 2010 hadi mwaka 2015.

Wakati akiwa Mbunge na Waziri, Dkt. Magufuli amefanya shughuli na kushika nyadhifa kadhaa ndani na nje ya nchi. Mwaka 2014, Dkt. Magufuli alishiriki katika Bunge Maalum la Kutunga Katiba Mpya akiwa ni Mjumbe wa Bunge hilo. Aidha, wakati akiwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi aliweza kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti Mwenza (Co-Chair) wa Mkutano wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo ya Makazi (UN-Habitat).

Tarehe 25 Oktoba, 2015 Dkt. John Pombe Joseph Magufuli alichaguliwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na tarehe 5 Novemba, 2015 aliapishwa kushika rasmi wadhifa huo.

4.0. UZOEFU WA UONGOZI NDANI YA CHAMA

Rais Dkt. Magufuli alijiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM) mwaka 1977. Amekuwa Mwanachama mwaminifu na ameshika nafasi mbalimbali za uongozi ndani ya Chama. Nafasi alizowahi kushika ni pamoja na kuwa Mjumbe wa Kamati ya Siasa ya Wilaya, Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya, Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Wilaya, Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Mkoa, Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Mkoa na Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Taifa.

Sambamba na kushika nafasi mbalimbali za uongozi, Dkt. Magufuli mara zote alijitoa kukitetea Chama na kuhakikisha kinapata ushindi. Alishiriki kikamilifu kuwafanyia kampeni wagombea wa CCM katika Chaguzi Ndogo zilizofayika katika majimbo ya Busanda, Biharamulo Magharibi na Igunga na kupata ushindi. Katika Mkutano Mkuu wa CCM wa tarehe 11 – 12 Novemba mwaka 2012, Dkt. Magufuli alikuwa miongoni mwa Mawaziri wachache waliopata fursa ya kuelezea mafanikio ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama ya Mwaka 2010 – 2015. Alielezea mafanikio ya utekelezaji wa Ilani, hususan katika sekta ya miundombinu.

Tarehe 11 mwezi Julai, 2015 Mkutano Mkuu wa Taifa wa CCM ulimchagua na kumteua Dkt. Magufuli kuwa mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Aliinadi vyema Ilani ya uchaguzi ya CCM (2015) na kukiwezesha Chama kupata ushindi mkubwa. Tarehe 25 Oktoba, 2015 alichaguliwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Nafasi hiyo imemwezesha kuwa Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa.

5.0. UFANISI KATIKA UONGOZI

Dkt. Magufuli ni kiongozi mnyenyekevu, aliye na hofu ya Mungu, mkweli, mtekelezaji wa ahadi, mwadilifu, shupavu, mahiri, mbunifu, mtafiti, mchapakazi na mtetezi wa wanyonge. Ni kiongozi mpenda haki na mchukia dhuluma, rushwa, ufisadi na ubaguzi wa aina yoyote ile. Ni kiongozi mwenye msimamo na mtetezi wa yale anayoyaamini.

Katika nyadhifa zote alizopata kutumikia alifanya kazi kwa uadilifu na umahiri mkubwa. Amejidhihirisha na kujipambanua kuwa ni mfuatiliaji na msimamizi wa sheria. Akiwa Mwalimu Sengerema Sekondari aliwezesha wanafunzi wote wa darasa lake kufaulu masomo ya Hesabu na Kemia aliyokuwa akiyafundisha. Akiwa Mkemia Mkuu wa Chama cha Ushirika cha Nyanza alisimamia vyema ubora wa uzalishaji wa mafuta ya Pamba na kuifanya Kampuni ya Nyanza kuwa mzalishaji mzuri wa mafuta ya Pamba.

Akiwa Waziri wa Ujenzi anakumbukwa kwa kubuni na kusanifu miradi ya ujenzi wa barabara, kusimamia vizuri matumizi ya fedha na kuhakikisha miradi hiyo inatekelezwa kwa viwango na kwa wakati uliopangwa. Uwezo wake katika kubuni na kusanifu miradi ya barabara uliigwa na nchi majirani, ikiwemo Kenya. Ameondoka Wizara ya Ujenzi akiwa amesimamia ujenzi wa zaidi ya Kilometa 17,000 za barabara za lami, madaraja makubwa zaidi ya 14 na madaraja madogo madogo zaidi ya 7,000 na vivuko. Aidha, alisimamia vizuri taasisi mbalimbali za Makandarasi, Wahandisi, Wabunifu na Wakadiriaji Majengo.

Dkt. Magufuli pia anasifika kwa uwezo wake mkubwa wa kuweka kumbukumbu ya kazi zake. Akiwa Wizara ya Ujenzi aliweza kutaja majina ya barabara zilizojengwa au zilizokuwa katika hatua za ujenzi, urefu wake, majina ya wakandarasi pamoja na gharama za ujenzi bila kusoma mahali popote. Wakati wa Rais Mstaafu Benjamini William Mkapa alimwita “Askari wa Mwavuli”.

Akiwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi alisimamia upimaji wa ardhi za vijiji na viwanja vya makazi, na kushughulikia migogoro mingi ya ardhi iliyowahusu wananchi wa maisha ya chini. Wakati akiwa Waziri wa Wizara ya Mifugo na Maendeleo ya Uvuvi alikuwa maarufu wa kutambua na kutaja idadi ya mifugo, kama vile samaki, ngómbe, mbuzi, kondoo, kuku, mbwa n.k. Kitendo cha kukamata meli ya kichina iliyokuwa ikivua samaki kwa wizi ndani ya Bahari Kuu ya Hindi eneo la Tanzania kilidhihirisha uzalendo kwa Taifa lake. Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Dkt. Kikwete alimpachika jina maarufu la “Tingatinga”.

Sifa hizi nzuri ameendelea nazo hata baada ya kuchaguliwa kuwa Rais. Katika miezi michache ya uongozi wake amethibitisha anatekeleza ahadi. Aliahidi kutoa elimu bila malipo na kuanzisha Mahakama ya Mafisadi. Ameweza kusimamia nidhamu kwenye utumishi wa umma kwa kuondoa watumishi hewa na kuchukua hatua dhidi ya watumishi wa umma wasio waaminifu, wala rushwa, wazembe na wanaoshindwa kutekeleza majukumu yao ipasavyo. Ameweza kudhibiti matumizi mabaya ya fedha za umma na kuongeza ukusanyaji wa mapato ya Serikali. Kwa hakika Dkt. Magufuli anaakisi uongozi bora unaopaswa kuigwa na viongozi wengi Barani Afrika na Dunia.

6.0. DHIMA YA UONGOZI WA SERIKALI YA AWAMU YA TANO 2015 – 2020) NA MALENGO YAKE MAHSUSI

Ilani ya uchaguzi ya CCM ya Mwaka 2015 – 2020 inazielekeza serikali zake kutumia nguvu zake zote kuendelea kupambana na changamoto kubwa nne;- Kwanza kuondoa umaskini, Pili, kupunguza tatizo la ukosefu wa ajira hasa kwa vijana, Tatu, kuendeleza vita dhidi ya adui rushwa na ubadhirifu wa mali ya umma, na Nne, kuendelea kudumisha amani, ulinzi na usalama wa maisha ya Watanzania na mali zao.

Sambamba na kutekeleza mambo hayo makubwa manne, kipindi cha Kampeni na wakati akizindua Bunge la 11 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tarehe 20 Novemba, 2015 Rais Dkt. Magufuli alitaja malengo mahsusi ya Serikali ya Awamu ya Tano. Malengo hayo ni haya yafuatayo:

· Kudumisha Muungano, Amani na Umoja wa Tanzania. Serikali haitamwonea aibu mtu mwenye nia ya kuvunja Muungano na kuvuruga amani na mshikamano katika nchi. Hili alilidhihirisha vizuri wakati wa uchaguzi wa marudio huko Zanzibar, kwani Uchaguzi ulifanyika kwa amani na utulivu.

· Kujenga Uchumi wa Viwanda ili kufikia azma ya kuwa nchi ya uchumi wa kati kulingana na malengo ya Dira ya Maendeleo ya Taifa 2025. Viwanda vinalengwa ni vyenye kutumia nguvu kazi kubwa, malighafi za ndani ya nchi, kuzalisha bidhaa kwa ajili ya soko la ndani na nje ya nchi. Nia ni kukabiliana na tatizo la ajira na umasikini;

· Kuongeza kasi ya ujenzi wa miundombinu ya kiuchumi, hususan miundombinu ya usafiri na nishati;

· Kuimarisha huduma za jamii, hususan elimu, Afya na Maji. Lengo ni kuhakikisha huduma hizo zinapatakana sio tu kwa urahisi bali pia kwa ubora unaostahili ili kukabiliana na maadui ujinga, umaskini na maradhi;

· Kusimamia uwajibikaji wa utumishi wa umma na kuondoa urasimu ndani ya Serikali. Lengo ni kuhakikisha watumishi wa umma wanafanya kazi kwa ueledi, uadilifu na kujituma ili kuwawezesha wananchi kupata huduma kwa wakati;

· Kuimarisha usimamizi wa rasilimali za nchi, ikiwemo kuhifadhi mazingira na kuzidisha vita dhidi ya ujangili. Lengo ni kuhakikisha rasilimali za nchi zinawanufaisha watu wote wa kizazi cha sasa na kijacho. Aidha, ukusanyaji wa mapato ya Serikali na udhibiti wa matumizi ya Serikali nao utaimarishwa;

· Kusimamia utawala bora unaozingatia sheria na haki za binadamu. Jitihada za makusudi zitaelekezwa katika kuzidisha mapambano dhidi ya rushwa, ufisadi, dhuluma na uonevu wa aina yoyote. Aidha, maslahi ya makundi mbalimbali katika jamii, ikiwemo wanawake, wazee, watu wenye ulemavu na watoto yatalindwa. Kwa upande mwingine, wananchi watahimizwa kuheshimu na kufuata sheria za nchi;

· Kulinda usalama wa raia na mali zao kwa kupambana na uhalifu, ikiwemo wizi, ujambazi, tatizo la dawa za kulevya n.k.

· Kudumisha na kuendeleza ujirani mwema, mahusiano mema na Mataifa mengine duniani pamoja na Mashirika ya Kimataifa na Kikanda;

· Kuendeleza na kusimamia vizuri shughuli za michezo, sanaa, burudani na utamaduni, ikiwemo kukuza lugha ya Kiswahili.

HITIMISHO
Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Dkt. John Pombe Joseph Magufuli imedhamiria kuongeza kasi ya ukuaji wa maendeleo ya kiuchumi na kuwataka watanzania washiriki kufanya kazi kwa bidii na maarifa ndani ya falsafa ya HAPA KAZI TU. Dhamira hii inakusudia kuwezesha Taifa letu kufikia Uchumi wa Kati uaoongozwa na Viwanda ili kutimiza malengo ya Dira ya Maendeleo ya Taifa ya mwaka 2025.

Chanzo: Michuzi Blog
 
MWENYEKITI wa Taifa wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais mstaafu Jakaya Kikwete, amekata mzizi wa fitna kwa kutangaza rasmi kuwa Mkutano Mkuu Maalumu wa CCM, utakaofanyika mjini hapa kesho utafanya kazi moja tu ya kumchagua Rais John Magufuli kuwa Mwenyekiti mpya wa chama hicho.

Kikwete alisema hayo alipofungua kikao cha Kamati Kuu ya CCM kwenye ukumbi wa White House, makao makuu ya CCM, mjini hapa jana. Kauli hiyo ya Kikwete inamaliza minong’ono ya muda kuwa hapangekuwa na kupokezana kijiti katika mkutano huo.

Pia kauli hiyo imezima madai kwamba kungekuwa na mchujo katika uchaguzi wa Mwenyekiti, ambapo majina hadi matano yangependekezwa na Kamati Kuu na kupelekwa katika Halmashauri Kuu ambayo ingekata mawili na kupeleka matatu kwenye Mkutano Mkuu Maalumu, ili yapigiwe kura kumchagua Mwenyekiti.

“Ajenda yetu kubwa leo (jana) ni moja tu; nayo ni kupendekeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ili nayo Halmashauri Kuu ya Taifa ipendekeze kwa Mkutano Mkuu wa CCM ili achaguliwe kuwa Mwenyekiti wa CCM,” alisema Kikwete kwenye ufunguzi huo wa Kamati Kuu, akitumia dakika tano tu, kisha wajumbe wakaendelea na ajenda. Rais Magufuli alichaguliwa kuongoza Tanzania Oktoba mwaka jana.

Katika hotuba yake hiyo ya jana, Kikwete aliwajia juu ‘wafitini’ walioombea chama hicho kife katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana.

Alisema “Wapo watu walidhani CCM ingekufa na walishajiandaa na salamu za rambirambi. Walidhani wataibuka. Hawakuibuka na hawataibuka kamwe.” Kikwete aliwaeleza wajumbe wa kikao hicho kuwa kilikuwa kikao chake cha mwisho cha Kamati Kuu, kauli iliyobainisha wazi kuwa anang’atuka kumwachia kijiti Rais Magufuli kuongoza chama.

Alisema amekuwa Mwenyekiti wa Chama kwa miaka 10, hivyo aliwashukuru wajumbe wa Kamati Kuu kwa kumsaidia katika kipindi chote hicho huku akisisitiza; “Bila msaada wenu CCM isingekuwa imara kama ilivyo hivi leo.” Wakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana, Rais Magufuli alikuwa akifahamika kama Tingatinga na kwenye mikutano kadhaa, Rais mstaafu Kikwete aliweza kumuita kwa jina hilo.

Wakati huo huo Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete jana alikagua ukumbi wa mikutano wa CCM na kuoneshwa sehemu mbalimbali ambapo alisema ameridhika na maandalizi ya mkutano kwamba yanaenda vyema.

Maeneo mengine aliyotembelea ni mabanda ya mama na baba lishe, sehemu za kutolea huduma za Benki na mabanda ya maonesho ya wajasiriamali.

Katika ziara hiyo aliambatana na Katibu Mkuu Abdulrahman Kinana, makamu Mwenyekiti Bara, Phillip Mangula, waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo Nape Nnauye, msemaji wa CCM Christopher Ole sendeka, naibu katibu mkuu wa CCM Bara Rajab Luhwavi na wajumbe wa Kamati Kuu Pindi Chana na Mohamed Seif Khatib. Wajumbe wa mkutano Mkuu maalum wa CCm walianza kuwasili jana na wengine wengi wanatarajiwa leo.

Kutoka Arusha, Mwandishi Veronica Mheta anaripoti kwamba CCM mkoani humo imejipanga kumpatia kura zote za ndiyo Rais Magufuli kuhakikisha anapata kura za kishindo ili kumthibitisha kuwa Mwenyekiti mpya wa CCM Taifa kutoka kwa mtangulizi wake Rais mstaafu Kikwete.

Katibu wa Siasa na Uenezi Mkoa wa Arusha, Shaaban Mdoe aliyasema hayo mjini hapa jana alipozungumza na waandishi wa habari. Waandishi hao walitaka kujua msimamo wa wajumbe wa mkoa huo kutokana na kuwa mmoja wa mikoa iliyoathiriwa na vuguvugu la baadhi ya viongozi na wanachama kusaliti na kukihama chama hicho siku chache kabla ya kufanyika kwa Uchaguzi Mkuu.

Mdoe aliondoa hofu kuhusu wajumbe wa Mkoa wa Arusha na kusema kwa ujumla wajumbe wote wamekubaliana kwa kauli moja kumpatia Rais Magufuli kura za ndiyo kwa kuwa hakutakuwa na maana yoyote ya kupiga kura za maruhani na kuelekeza kwa kivuli kwa kuwa mgombea ni yeye pekee.

Alisema wajumbe hao wamefikia hatua hata ya kudiriki kupendekeza kura watakazopiga kuwa za wazi ili kuondoa uwezekano wa kuwepo kwa kura hizo za maruhani kwani wana imani kubwa na utendaji mzuri wa Rais Magufuli ndani ya chama kutokana na kazi nzuri aliyoifanya kwa kipindi kifupi cha urais wake.

Mdoe alisema kwa sasa hali ya kisiasa ndani ya chama hicho mkoani Arusha ni nzuri kutokana na kila mwanachama na kiongozi kutambua siasa zilishapita wakati wa kupatikana kwa mgombea wa urais ndani ya chama.

Wasifu wa Magufuli

Dk John Pombe Joseph Magufuli alizaliwa Oktoba 29, 1959 wilayani Chato mkoani Kagera (sasa mkoa mpya wa Geita). Alianza elimu ya msingi katika shule ya msingi Chato wilayani Chato mwaka 1967 na alihitimu mwaka 1974.

Alijiunga na Shule ya Seminari Katoke wilayani Biharamulo, ambako alisoma Kidato cha Kwanza na cha Pili mwaka 1975 – 1977. Alihamishiwa shule ya sekondari Lake mkoani Mwanza, ambako alisoma Kidato cha Tatu na Nne mwaka 1977 - 1978. Masomo ya Kidato cha Tano na Sita aliyapata shule ya sekondari Mkwawa mkoani Iringa kati ya mwaka 1979 na 1981.

Alirudi Chuo cha Ualimu Mkwawa kusomea Stashahada ya Elimu ya Sayansi katika masomo ya Kemia, Hisabati na Elimu. Alisoma hapo mwaka 1981 – 1982. Baada ya kuhitimu hapo, alianza kazi ya ualimu katika shule ya sekondari Sengerema mkoani Geita, akifundisha masomo ya Kemia na Hisabati kati ya mwaka 1982 na 1983.

Baadaye alijiunga na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) kwa mujibu wa sheria akianzia Makutupora, Dodoma (Julai - Desemba 1983), kisha kambi ya Makuyuni mkoani Arusha (Januari hadi Machi 1984) na kumalizia kambi ya Mpwapwa mkoani Dodoma (Machi – Juni 1984).

Mwaka 1985 alijiunga Chuo Kikuu cha Dar es Salaam akisomea Shahada ya Sayansi ya Elimu akibobea kwenye masomo ya Kemia na Hisabati na alihitimu mwaka 1988. Mwaka 1989 - 1995 alifanya kazi katika Kiwanda cha Nyanza Cooperative Union (Ltd.), akiwa Mkemia na wakati huohuo alianza masomo ya Shahada ya Uzamili ya Sayansi katika Chuo Kikuu cha Salford nchini Uingereza, kikishirikiana na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ambako alisoma kati ya mwaka 1991 na 1994.

Magufuli aliendelea na elimu ya juu zaidi kwa maana ya Shahada ya Uzamivu ya Kemia kuanzia mwaka 2000 hadi 2009, ambayo alihitimu katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na kuwa mhitimu wa Shahada ya Udaktari. Dk Magufuli ana mke na watoto.

Alichaguliwa kuwa Mbunge wa Chato mwaka 1995 na aliposhinda Rais wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa alimteua kuwa Naibu Waziri wa Wizara ya Miundombinu. Katika uchaguzi wa mwaka 2000, Dk Magufuli aligombea na kushinda kwa mara ya pili. Rais Mkapa alimteua kuwa Waziri wa Miundombinu.

Mwaka 2005 alichaguliwa kuwa mbunge kwa kipindi cha tatu na Rais Jakaya Kikwete alimteua kuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi hadi mwaka 2008, alipohamishiwa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, ambayo aliiongoza hadi mwaka 2010.

Mwaka 2010 alifanikiwa kuchaguliwa kuwa Mbunge kwa mara ya nne na Rais Kikwete alimrudisha katika Wizara ya Ujenzi, ambayo aliiongoza hadi 2015. Mwezi Oktoba mwaka 2015 alichaguliwa kuwa Rais wa Awamu ya Tano. Wasifu wa Jakaya Kikwete Kuzaliwa – Msoga, Bagamoyo mkoani Pwani Oktoba 7, 1950.

Elimu ya Msingi – Lugoba wilayani Bagamoyo 1956-1965. Kidato cha Nne na Sita - 1966-1971, Tanga Sekondari na Kibaha. Chuo Kikuu Dar es Salaam - Shahada ya Uchumi 1972-1975. Naibu Waziri Nishati na Madini – 1998 -2000. Waziri wa Maji, Nishati na Madini – 1990 -1994.

Waziri wa Fedha - 1994 -1995. Mbunge wa Kuteuliwa – 1988 – 1990. Mbunge wa Chalinze – 1990 -2005. Uzoefu, Utumishi na Uongozi CCM – miaka 40 Tanu hadi CCM Mjumbe wa Kamati Kuu – miaka 20. Mjumbe wa NEC - miaka 33. Ajira ya mara kwanza CCM – Aprili 3, 1975 Katibu Msaidizi Singida. Mwenyekiti wa CCM – Tangu 2006 hadi sasa.

Habari Leo
 
Back
Top Bottom