GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 56,571
- 108,926
Tokea mchana baada kukamilika kwa mazungumzo na Wazungu wa Madini wa Barrick na kupelekea utiaji saini wa makubaliano mapya ya usimamizi na malipo stahiki nimekuwa nikipitia Social Platforms nyingi ( JF ikiwemo ) na kugundua kwamba Watu wengi wamekuwa wakimshutumu na hadi kumdhihaki Mbunge Mheshimiwa Tundu Lissu kwa kumuambia kwamba ' ameshindwa ' na mambo mengine mengi.
Ama hakika leo ndiyo niweza kujua kwamba kumbe Watanzania wengi uwezo wao wa ' Kufikiri ' ni mdogo sana na kwamba bado tuna safari ndefu mno ya kuweza kukimbizana na wana Jumuia Afrika Mashariki wenzetu hasa Wanyarwanda, Wakenya na Waganda ambao kiukweli IQ zao zipo juu mno na pengine ndiyo maana wametuacha Kimaendeleo.
Yaani Watanzania badala ya kuchambua hili jambo vizuri tena Kisomi kabisa ili kuonyesha kwamba huko Vyuo Vikuu hatukuenda kupoteza muda au kukua tu wengi wetu tumeacha kujikita katika ' Hoja ' Kuu na ya Msingi na badala yake tumetanguliza mbele itikadi zetu za Kisiasa ( hapa namaanisha UCCM na UCHADEMA ) katika jambo ambalo pengine halihitaji zaidi Siasa ila linahitaji zaidi mjadala mpana.
Kwa wale ' Critics ' wote wa Mheshimiwa Mbunge Tundu Lissu labda niwaambieni tu kwamba mnaweza leo mkamcheka na kumdhihaki Lissu kwa kila aina ya maneno na kashfa ila tambueni kwamba yale ' makelele ' yake au ule ' uropokaji ' wake ambao Mimi nimeubatiza rasmi kwa majina ya ' makelele tija ' au ' uropokaji tija ' ndiyo umepelekea leo hii tumekuwa na haya matokeo ' chanya ' ya mazungumzo marefu na Watu wa Barrick na nadhani Watanzania tulipashwa ' Kumpongeza ' Lissu badala ya kumdhaki hivi.
Hivi mnadhani bila makelele yale / uropokaji ule wa Tundu Lissu Serikali yetu ingejipanga vyema kuandaa Timu yake iliyokuwa chini ya Waziri Profesa Kabudi ili waweze kufanya mazungumzo makini ambaye yangeinufaisha leo hii nchi yetu Kimapato kama hivi ilivyotokea? Siyo kila Mtu anayekupinga au kukusema vibaya ' anakuchukia ' tena kwa Mimi ninavyojua ni kwamba yule Mtu anayekusema au kukukosoa ndiyo mwenye ' mapenzi ' mema na ya kweli nawe kuliko yule ambaye kila mara anakuchekea na kukusifu halafu siku ukija ' kuharibikiwa ' ndiyo anakudharau zaidi.
Ingekuwa ni nchi zingine ambazo zina Watu wenye IQ za kweli na ambazo zinawatosha sawasawa nadhani baada ya haya mazungumzo yaliyozaa ' tija ' na Barrick leo basi tungempongeza na hata kumpa ' Tuzo ' Mheshimiwa Tundu Lissu kwani yale ' makelele tija ' yake ' uropokaji tija ' wake ndiyo umesaidia ' kuchochea ' kuwepo kwa umakini wa mazungumzo na hawa Wazungu wa Barrick lakini bahati mbaya mno Watanzania wengi wenye akili fupi na za hovyo hovyo leo kutwa nzima wanachokifanya ni kumsema vibaya Tundu Lissu na kumdhihaki.
Nikiwa kama Mtanzania ( GENTAMYCINE ) niseme tu kwamba nimefurahi sana kuona kwamba leo kumekuwa na mafanikio ya Tume iliyoundwa na Mheshimiwa Rais wa Tanzania Dkt. Magufuli ambayo pia imeleta mafanikio makubwa hivyo angalau sasa Tanzania itakuwa inapata kile inachostahili kutoka katika Rasilimali zake za madini ila nadhani pia hata Mheshimiwa Mbunge Tundu Lissu nae anahitaji kupongezwa kwani sidhani kama bila ' makelele tija ' yake / ' uropokaji tija ' wake leo Tanzania ingefikia hapa ilipofika.
Namuunga sana mkono Mheshimiwa Rais Dkt. Magufuli katika harakati zake za kuiletea Maendeleo Tanzania lakini pia namuunga mno Mheshimiwa Mbunge Tundu Lissu katika harakati zake za kuishtua na kuiamsha Serikali juu ya mambo ambayo ama hawayajui au wanayajua lakini wanataka kuyapeleka ndivyo sivyo. Nilidhani leo kutakuwa na ' mijadala ' yenye ' tija ' badala yake kila nikipita mitaani ' Vijiweni ' na nikitembelea mitandao yetu hii nashuhudia tu akili zile zile ' fupi ' na za ' hovyo hovyo ' kutoka kwa Watanzania ambao bahati nzuri kutwa wanajiita ' Wasomi ' au ' Great Thinkers '.
Watanzania tubadilike Kifikra na Kimtizamo kama kweli tunataka kukimbia Kimaendeleo na Kidemokrasia.
Nawasilisha.