Wasichana /Wanawake wenzangu

Wasichana /Wanawake wenzangu

Wanawake wenzangu!
Natamani sana sote humu tuwe wake wema kwa wame zetu au mahusiano yetu kiujumla. Hivo naomba kushea kitu hapa. Hii nimeona mahali nikabarikiwa nayo kuleta kwenu wapendwa.

BUSARA KWA WANAWAKE.

1. Degree yako ya fist class uliyoipata chuo kikuu haiwezi kukufanya uwe mke first class katika ndoa yako bali ni heshima yako na uthubutu wako.

2. Mwanamke anaemuheshimu mumewe ni mwanamke bora ambae kila mwanaume angetamani kuwa nae.

3. Tabia yako na misimamo yako ndio itakayomfanya mumeo ajute au afurahie kukuoa wewe.

4. Kuwa mke bora inakubidi uwe vizuri katika maarifa ya kutawala hasira zako na sio kuwa mtu wa kulipiza visasi.

5. Kuwa kiongozi huko kazini kwako lakini kuwa mtu wa kunyenyekea nyumbani kwako kwa mumeo. Hiyo ni busara.

6. Usiweke mashindano na mumeo, mpe hongea na mtie moyo kwa kila hatua anayopiga katika maisha.

7. Kuwa na ubinadamu, sio kosa dogo tu mumeo amefanya ukatamani kulipiza kisasi. It won't help u!

8. Kuwa mkarimu, kila mwanaume anamuheshimu mwanamke mkarimu na mwenye msimamo.

9. Usijaribu kumpa adhabu mumeo ya kumnyima chakula cha usiku kitandani, hii itamlazimu kutafuta chakula nje ya ndoa.

10. Hakuna kitu kibaya kama utakubali kuwa ulikosea kama kweli ulikosea. Kuwa mrahisi kukubali kama kweli ulikosea. Na omba radhi pale inapobidi.

11. Jiandae kumsamehe mumeo pale anapokosea kwa maana mke atoae msamaha kwa mumewe ni mke mwema tofauti na yule aliejaa visasi.

12. Tengeneza maamuzi ya kuwa mke mwema, pasina kuwa na hofu yoyote na Mungu atakubariki.

13. La mwisho na la muhimu tambua kwamba mwanamke aliejaliwa umbo zuri na sura nzuri pasina maarifa kichwani anafaa kwa usiku mmoja, lakin yule mwenye maarifa na ufahamu yeya afaa kwa maisha yote!

Akhsanteni na weekend njema

Mmmmh haya shostie naona leo umekuja na style ya ukweli that's good
 
Ukikutana na wahivi katoe posa haraka. Yaani ukizubaa tu washabeba. Maana dada zetu ma role model wao ni kina sepenga. Wamesahau mwanaume anaweza kukupenda au kukutamani
 
Kama yupo mwanamke mwenye vigezo hivyo hapo juu, Naomba ajitokeze tukamuweke Kwenye MAKUMBUSHO YA TAIFA kwasababu atakuwa ni hazina kubwa sana iliyobaki
hahahahaha a hahahahaha mkuu mbona unatudhihaki wanawake
 
Ukikutana na wahivi katoe posa haraka. Yaani ukizubaa tu washabeba. Maana dada zetu ma role model wao ni kina sepenga. Wamesahau mwanaume anaweza kukupenda au kukutamani
Mbona mmekufa mioyo nasisi w wanawake jamani??? Kwanini lakini???
 
Hasa hapo kwa chakula cha usiku wajitafakari vizuri maana wakibana tu ndipo mwanzo wa kujitengenezea uke wenza utakaowagharimu sononeko la moyoni
 
Back
Top Bottom