Wachina wana ubaguzi wa hali ya juu na wapo kimaslahi zaidi, huwa nashindwa kuelewa hadi sasa kwa nini serikali yetu huwa inataka kuwaaminisha Watanzania kuwa watu hao ni marafiki wetu wa enzi.
Tuliopata kuishi huko, kufanya kazi huko tunawajua fika kuanzia namna wanavyowaza, namna wanavyotenda na hata maamuzi yao.
Makala hii imeandika mambo mengi ya kweli, imenikumbusha namna ambavyo Mchina mmoja nikiwa Beijing alivyonishangaza kwa swali la kipuuzi.
"Hivi kwa weusi huu wa ngozi zenu mkiwa mnatembea huko kwenu huwa hamgongani?", aliniambia mwanadada mmoja wa Kichina.
Mwanzoni nilitaharuki kwa swali hilo lakini nikapiga moyo konde na kumuuliza, "Ni shi shenme yisi?" nikiwa na maana "Ni nini nia ya swali lako?"
Mwanadada yule akaniambia, "Wengi wa Wachina huwa wanaamini kuwa kwa weusi wa Waafrika basi nyakati za usiku huenda huwa hamuonani na hata wakati wa kutembea mnagongana gongana tu".
Unaweza kucheka au kushangaa lakini ndio ukweli huo...