Dr Matola PhD
Platinum Member
- Oct 18, 2010
- 61,429
- 108,580
Hakuna wanaoongoza kwa ubaguzi kama waislamu binadamu mwenzio huwezi kumuita kafir kisa siyo muislamu.
So it's OK wewe ubague ila ukibaguliwa ni issue..akili za Matope!
Tumekusikia dogo haya rudi darasani ukasome ili ukamilishe kilichokupeleka huko. Huu umbeya uuache hukohuko kwao.
Wewe kijana utakuwa mwepesi sana kudanganywa...ina maana hata sosi (Gazeti la Raia Mwema) hapo chini hujaiona
Tena umesahau ukipanda bus kama wewe ni mweusi utaona wanafunika pua zao ,jamani watu wale wanashangaza .
hahahaha umenipa raha, JF idumu milele.
Hahahahaha mimi huwa siwaelewi ila nilikua nikiona wanaziba pua ndo nawasogelea na kujifanya bus limenisukuma.Obama amesaidia kwa kiwango flani kwani wengine wakikuona wanadhani umetoka kwa Obama lol.Au wana kawaida ya kuwaita Waafrika "xiao hei gui" (小黑鬼😉 au "hei gui" wakiwa na maana shetani mdogo mweusi au shetani mweusi.
Ukishawashtukia na kuwaumbua wasivyo watajifanya kuomba msamaha huku wakivunga kuwa hawana maana mbaya.
Kuhusu hili nadhani ni kasumba ya nchi za bara la Asia, nliona Bangkok-Thailand mchezo huo upo sana, unaulizwa maswali ya ajabu ajabu, Pia huko India ndio usiseme. Most of them hawajui nchi ya Africa tofauti na South Africa.
Nchi hizi za Asia i.e, India hawako exposed na Dunia tofauti na nchi yao, kila kitu wanafanya kivyao vyao tu.
Nlikua nafanya kazi fulani India ilikua ya mwaka mmoja, so ilifika time Visa yangu ilikwisha ikabidi nifanye extension...Hapo ndipo nlipowachukia na kuwadharau Wahindi...Extension ilinicost miezi miwili...
Ilikua kwenye jimbo la BIHAR ktk mji wa PATNA, ni kaskazini mashariki mwa India. Unaenda kwenye Ofisi za serikali zinazo shughulika na Wageni( Foreigners) but chakushangaza hakuna mtu anaeongea kiingereza..Dah, ilibidi niwe natoka na jamaa Ofisini ili awe translator...yani huko ni NAMASTE, KYON, APKAA NAM KYA HEI......ACCHAA,,TICKEE..UHHHH
Hahahahaha mimi huwa siwaelewi ila nilikua nikiona wanaziba pua ndo nawasogelea na kujifanya bus limenisukuma.Obama amesaidia kwa kiwango flani kwani wengine wakikuona wanadhani umetoka kwa Obama lol.
kama unawahitaji wamejazana sana mitaa ya congo corridor kariakooo tutakuitia ukitaka ila kwa bei lakini
Huu aliouleta ndio ujinga. Wewe kama unabisha mchukue mchina mpeleke kijijini kwenu uone jinsi watu watakavyomshangaa na hata kutaka kumgusa ili kuona kunani kwenye ngozi yake. Huo nao utaita ubaguzi? Wewe kama unahisi hukubaliki huko uliko na hufurahii hali hiyo rudi nyumbani utakapothaminiwa. Hata mimi nimeishi huko na kuamua kurudi nyumbani kujenga nchi ifanane na za huko ughaibuni ili vijana mbaki hapa nyumbani.Mkuu hebu acha udhadhalishaji bana! Mwenzio kaleta hali halisi inayotutokea watu weusi huki mashariki halafu wewe unanena uji.nga tu?
Aargh!
Tumekusikia dogo haya rudi darasani ukasome ili ukamilishe kilichokupeleka huko. Huu umbeya uuache hukohuko kwao.
RAFIKI yangu, sitamtaja jina ambaye wote tunasoma chuo kimoja hapa Shanghai anapenda sana wasichana wa kichina. Rafiki yangu huyu Mmalawi, anasomea shahada ya kwanza ya lugha ya kichina na hivyo bado ni kijana. Katika harakati zake za kutongoza wasichana wa kichina, anakiri kuwa siku zote hudanganya kuhusu utaifa wake.
Rafiki yangu ananiambia: Nikisema ninatoka Afrika siwezi kukubaliwa. Kwa Wachina wengi, Afrika ni msamiati mwingine unaomaanisha umasikini, na hapa China, fedha ni kigezo muhimu katika uhusiano wa kimapenzi baina watu. Kama ni lazima useme unatoka Afrika, basi walau taja Afrika Kusini na hapo kidogo utaonekana wa maana.
Ukiwa mgeni unayeishi China, utaifa na rangi ya ngozi yako vinaweza kuwa faida au hasara katika kurahisisha au kufanya maisha yako yawe magumu. Kwa ujumla Wachina, wanathamini watu wanaotoka katika nchi tajiri, maana wao wanaleta fedha, na wanachukia wanaotoka nchi masikini kwa sababu wanaamini wao wanakuja kuchuma.
Mmarekani ni kama mungu wao hapa. Wazungu wa Ulaya kadhalika wanapendwa. Waarabu nao wanakubalika kiasi kwa sababu ya fedha. Kama unatoka nchi masikini ikiwemo za Kiasia kama Tajikistan, Uzbekhstan na nchi nyingine zinazoishia na stan, una matatizo. Mtu mweusi ndio kabisa. Mtu mweusi anayetoka nchi zilizoendelea atapendwa baada ya kufafanua kuwa yeye sio mweusi wa Afrika.
Katika hali hii ya unyanyapaa, mtu mweusi anaathirika mara mbili. Kwanza, kutokana na ukweli kwamba anatoka nchi masikini na pili ni kuwa na ngozi nyeusi. Kwa Wachina wengi, kuwa tu mweusi hata bila kujali kipato, ni tatizo. Mambo kadhaa yanathibitisha ukweli huo.
Kule Beijing, Waafrika wamekuwa wakilalamika kuwa madereva wa teksi wengi hawasimami kama wakimwona abiria mweusi. Baadhi ya abiria weusi wamekuwa wakiwatumia Wachina kuwasimamishia teksi! Hayo ni ya kuambiwa. Yapo niliyoyashuhudia mwenyewe.
Jumamosi iliyopita nikiwa na rafiki Mtanzania mwenzangu (jina namhifadhi) tulipanda treni na kushuhudia kinyaa cha wazi cha baadhi ya Wachina wanapokutana na Waafrika. Tulipoingia ndani ya treni, hakukuwa na viti (siti) zilizo wazi na hivyo kutulazimu kusimama. Nilikuwa wa kwanza kupata siti. Kisha baadaye mwenzangu naye akapata, lakini, mara tu baada ya yeye kukaa majirani zake waliokaa upande wa kulia na kushoto, mwanamke na mwanamme, na ambao hawakuwa katika msafara mmoja, wakanyanyuka na kutafuta siti nyingine. Hawakutaka kukaa na mtu mweusi.
Katika tukio jingine lilitokea tukiwa ndani ya duka moja kubwa, siku hiyo hiyo, tulipofika kwenye deski la kulipia, mhudumu alizikagua fedha tulizotoa, akizigeuza juu chini, na kuzikodolea macho kwa umakini, kuthibitisha kuwa ni halisi. Wateja waliotangulia mbele yetu fedha zao hazikukaguliwa namna ile.
Kama haitoshi, baada ya kutuhudumia, wakati tumekwishatoka katika meza ya malipo, wateja walio nyuma yetu wakamwambia mhudumu kuwa hatujalipia chupa ya maji, ambayo wao hawakujua kuwa tuliingia nayo. Mhudumu akatufuata, na bila kuzungumza nasi akachukua ile chupa ya maji ambayo mwenzangu alikuwa ameishikilia mkononi na kuangalia lebo. Akagundua kuwa sio ya duka lao, lakini hata hivyo alikwishatufedhehesha.
Huu ndio ubaguzi wa kimyakimya wa China. Hawakupigi au kushambulia mwili wako. Wanakuua kihisia.
Hata hivyo, ukweli ni kwamba unyanyapaa wa rangi hauathiri mwafrika mweusi tu, hata mchina mweusi, (labda awe na fedha). Hapa China, rangi nyeusi inanasibishwa na ukulima na umaskini. Nimeambiwa na mwenyeji mmoja kuwa kuna mji fulani huitwa waafrika wa China wengi ni wahamiaji mijini, wanafanya kazi duni, ni maskini na tabia zao ni mbaya!
Zipo sababu zinazochangia mtazamo hasi wa baadhi ya Wachina dhidi ya Waafrika. Kwanza, jamii ya China kwa muda mrefu imejifungia, ikiishi katika dunia yao. Njia zao kuu za kupata taarifa ni kupitia vituo vya televisheni vyao wenyewe, redio zao, magazeti yao na mitandao yao ya kijamii iliyochukua nafasi ya Facebook, Twitter, Blogu, Youtube. Watapata wapi muda wa kujifunza kuhusu mataifa mengine? Hapa China ni wageni wanaoruhusiwa kuona televisheni za nje. Katika vyombo vya China, hakuna habari nyingi za Afrika na zilizopo nyingi ni kuhusu vita, ukimwi, umasikini na kadhalika.
Nakumbuka katika siku ya mwisho ya masomo ya lugha ya Mandarin kwa muhula ulioisha, somo lilihusu majina ya wanyama, mwalimu wangu alionyesha kwa kutumia projekta picha ya mbuga mojawapo ya wanyama iliyoko Afrika na kisha akaniuliza kwa mshangao nyumba mbona hazionekani. Eti, yeye alijua kuwa Afrika yote ni mbuga tu na kwamba tunaishi porini na wanyama. Mwalimu wangu mwingine nilipomfuata wiki chache baada ya kuanza masomo ili kutaka kujua Bara la Afrika linaitwaje kwa lugha ya kichina, alikuwa hana uhakika kama Afrika ni bara au nchi!
Ujinga huu ndiyo kwa kiasi fulani unachangia dharau na ubaguzi wa chini chini dhidi ya watu weusi hapa Shanghai. Unatembea mtaani, Wachina wengi wanakuangalia utadhani wameona kiumbe cha ajabu kilichodondoka kutoka mbinguni. Kwa rafiki zangu ambao rangi yao nyeusi iliyokolea, dharau ya Wachina wanapowaona ni mara mbili zaidi. Wengine wanakuuliza eti ni kweli kuwa Waafrika ni weusi kwa sababu ya jua kali. Na hii ni Shanghai, jiji la kubwa zaidi la China.
Ipo dhana pia kuwa Waafrika tuliopo hapa China tumekimbia nchi zetu zenye dhiki za kutisha na kuja kuhemea kwenye nchi yao. Hawa hawajui kuwa kuna Wachina wengi waliopo Afrika ambao nao wamekimbia shida za kwao, wakifanya biashara za kimachinga ambazo huenda sisi hatufanyi kwao.
Kadhalika, wapo wachina wanaofikiria pia kuwa wanafunzi tunaofadhiliwa kwa udhamini wa serikali tunafaidika kwa gharama yao, wakati wao wenyewe wanahitaji msaada wa serikali, wakisahau kwamba kampuni za nchi zao zipo kila nchi zikipurura maliasili zetu, na pia tumekuwa soko la bidhaa duni la China. Wanavuna mabilioni ya faida kwa kila senti moja wanayotusomeshea.
Zipo fikra kuwa Waafrika wenyewe waliopo China ni sababu ya huuunyanyapaa kwani baadhi yao wanajihusisha na vitendo viovu na kupelekea Wachina wengi kuamini kuwa sisi ni wezi, majambazi na wauza madawa ya kulevya. Unaweza kudhani kuwa ni hoja yenye mashiko ukizingatia taarifa za Waafrika tunazozisikia huko nyumbani za kukamatwa kwa Waafrika wanaojihusisha na dawa za kulevya. Hata hivyo, vyombo vya habari vya China vinaarifu matokeo ya uhalifu mengi zaidi kuliko hayo ya waafrika. Halafu kama tatizo ni uhalifu mbona kuna wachina wahalifu wanaomaliza tembo wetu lakini hatuwabagui.
Kuna mambo mengi ya ubaguzi dhidi ya weusi yanayotokea hapa China hususan katika ajira na kwenye taasisi za elimu. Kwa ujumla kwa baadhi ya wachina (sio nwachache, ingawa sitaki kusema wengi), kila mwafrika ni mhalifu, masikini na dhaifu kitaaluma mpaka atakapothibitisha vinginevyo.
Huwa nacheka na kusikitika pale ambapo mara nyingi ninapotembea hujitokeza mchina kutaka kuniuzia bangi. Mtu mweusi!? lazima anavuta tu!, ndivyo inavyoonekana wanavyofikiria.
Hata hivyo, si Wachina wote ambao wana mitazamo ya dharau na ubaguzi. Ni yule yule rafiki Mmalawi ambaye hudanganya utaifa wake anapotongoza wasichana wa kichina ambaye amepata hadi familia ya kichina, ambayo imempokea kama mwana familia. Kila wakati wa likizo huenda kupumzika na kujumuika nao wakimfurahia kama sehemu ya familia, ingawa hata hivyo siku zote hulalamika kuhusu bibi wa familia ambaye alikuwa hajapata kuona mtu mweusi maishani mwake na ambaye humsogelea na kumchunguza kwa ukaribu, (huyu ni binadamu kweli?) kila anapaopata muda.
Njonjo Mfaune - RaiaMwema