Kweli?
Lakini Mbona.....
Uturuki ni Taifa liloshika dini ya Kiislamu na limepiga hatua kubwa sana ya maendeleo katika kila fani, liko sambamba na karne ya 21. Hilo halina shaka kabisa.
Ujerumani ni Taifa la Kikiristo hata maadili ya Utawala wao unaendeshwa Kikiristo, lakini ndio Taifa limezalisha the Best Engineers on Earth and honesty society on earth, as per various studies.
Dini iwe ya Ukiristo au Uislam, kwa kipindi hiki cha miaka 2000 iliyopita imechangia sana kumuinua mwanadamu na kumuweka katika maadili mazuri.
Bila dini, wanaadamu wangekuwa katika hali mbaya sana ya Kinyama. Dini zipo bado hali ya Ubinaadamu imepotea.
Hata Ukomunisti wenyewe, unaofai hauna dini, falsafa yake yote ni mkusanyiko wa maadili na madundisho ya dini mbalimbali.
Kwa wale waliosomea "Sociology" watakubaliana na hili.
Wanaadamu tunahitaji dini. Na imani nzuri haitakataa Sayansi na Teknolojia yake, elimu yoyote ile inayoleta faida nzuri kwa mwanadamu basi lazima itakubaliwa na dini.
Sema hapa Afrika, kuna dini na imani zingine ni kwa ajili ya kuwapumbaza Waafrika, na ndio maana na sababu Mwalim Nyerere alizizuia dini nyingi kuingia Tanzania. Botswana tayari wameshawazuia wahubiri wa kigeni. Afrika ya Kusini wamewapeleka wahubiri fulani kwenye vyombo vya haki za binaadamu, wengine wanalishwa ukoka, nyoka waliokufa, petroli nk.
Tulipokuwa Congo, tuliona watu wanamchomba mbwa na kumla hadharani, tulipouliza tuliambiwa "Yesu kasema tule kila kitu kwa jina lake". Hivi ndivyo vitabu vitakatifu vinavyotumika vibaya. Kwa hata Israeli inavyotawala kwa Ubaguzi na Unyama. Utawala wa Kikaburu ulitumia Biblia. Vita vya Mashariki ya Kati, wanavyotumia Qur'an vibaya kwa kuuwana wenyewe kwa wenyewe.
Dini ni kwa ajili ya maadili mazuri na kumlinda na kumuwekea mwandamu heshima yake. Kujua thamani halisi ya maisha. Kuabudu aliyetuumba. Dini ilitakiwa kudumisha Ubinaadamu katika maisha yetu na kuleta amani kwenye roho zetu na majirani wetu.