Wasanii wengi bongo hawajui kuimba in live performance na waandaaji wa live performance hawajui kuandaa.

James88

JF-Expert Member
May 14, 2017
1,700
1,754
Huu ni ukweli mchungu.

Nimejaribu kuangalia live performance za wasanii mbalimbali bongo kuanzia hao akina diamond na ali kiba, sijui weusi na wengine wengi sana, wote hamna kitu. Kusema ukweli when it comes to live performance, they do nothing, kama ww unajua how live performance should be, basi utakubaliana na mm.

Nasema tena kwamba hawajui kuimba kwa sababu;

1. Wasanii wengi akiimba in live performance basi sauti yake ni lazima itoke base.

2. Msanii anakuja kuimba kwenye show, lakini dj wake anampigia back vocal while jamaa anaimba. Huu ni upuuzi, sasa maana ya live performance ni nini?

3. Wasanii wengi hawana pumzi, so wanaishia tu kuwaimbisha mashabiki.

Pia waandaaji wa muziki nao hamna chochote maana unaangalia show ya mtu unaishia kusikia kelele za mashabiki na spika zao zikiwa zinakoroma. Hivi tunashindwa hata kujifunza kwa majirani zetu wakenya? Tunatia aibu aisee.

Msanii yeyote anayejua kuperform live ni lazima aweze kufanya mambo yafuatayo.

1. Sauti anayoimba akiperform live basi icorrelate kwa kiasi fulani na sauti yake ambayo watu wamezoea kuisikia katika nyimbo zake.

2. Msanii ukiimba basi kusiwe na back vocal ya wimbo wako. tulisikie tu beat plus sauti yako na siyo unaimba kufuatisha wimbo wako.

3. Mambo ya kuwaimbisha mashabiki kwa sehemu kubwa hatutaki, mnazingua.

Kama msanii haqualify katika hivyo vigezo vitatu nilivyovitaja hapo juu, basi huyo hajui kuimba. Mfano mzuri unaweza kuangalia kipande hiki kidogo sana cha rama dee mwaka 2016 katika Naamka tena Live concert. Au unaweza kuangalia live show kadhaa za rama dee japo bado wanaoandaa muziki ni tatizo kutokana na music system zao.

Pia unaweza kuangalia Nyanshiski hapa na Jua Kali hapa Kutoka kwenye hizi link mbili za mwisho hapo ndio natoa definition ya msanii anayejua kuperform live.

Mapovu ni ruksa kama kuna msanii wako nimemgusa.
 
Mi naona wazifuate kwaya hasa za catholic na wale SDA watafundishwa namna ya kuimba live. Kuna tatizo background yao ya kimziki.
 
Back
Top Bottom