Wasanii waungana kupinga maandamano ya UKUTA

Wasanii waungana kupinga maandamano ya UKUTA

Hao sio wasanii ni wanachama wa ccm. Unafiki tuweke pembeni. Kuna mtu kawatuma na hao ni kwamba wanatumikia matumbo yao. Hadija kopa ni msanii au mwanachama wa ccm?
 
Awamu hii wamesahaulika bora wajitutumue mh.ajue kwamba wapo, Le mutuz ni msanii wa nini mcheza filam au mwanamuziki?
 
Tatizo la bongo kuwa msanii ni kujichubua ngozi (haijalishi jinsia), kuwa na skendo za ukahaba (huu ni wa kingono na kiitikadi) na kufuata penye maslahi zaidi. Tuliona mifano hai kipindi cha uchaguzi. Ndani ya mwezi mmoja tu msanii mmoja kahama vyama hata mara kumi kidogo na hapa ni dhahiri kwa kufuata ulaji tu. Sasa mtu kama huyo atasema nini aeleweke ilhali akiwekewa fungu kubwa zaidi na UKAWA atakana kauli yake mwenyewe. Bongo hakuna wasanii kuna walalahoi wanaofanya maigizo. Msanii miaka 20 kwenye tasnia hata pa kulala hana anaishi kwa wazazi sasa hapo kuna nini kama sio njaa na matatizo tu.
 
Ndo huyo aliyejichubua??
Lazima uweze kucreate public opinions ili kuzishinda propaganda nakumakinisha propaganda.

##ndio maana, wanazitafuta kwawanasiasa, wasanii na hata kwavyama vya siasa##
 
Wasanii wa muziki na filamu wameungana kupinga maandamano ya UKUTA wamesema wanawaomba wananchi wasifanye maandamano hayo kwa kuwa watafungwa
Aidha wamwaasa viongozi wa CHADEMA kuacha maandamnao hayo na kutafuta njia nyingine kwa kuwa wao pia wanafamilia zao zinaowategemea.

Pia wamesema maandamano hayo yatasababisha shughuli za kijamii na biashara kusimama na pia wazazi wataumia kuona watoto wao wameumizwa wakiwa kwenye maandamano hayo.

​

Hao wasanii siku wakiugua waende ofisi za ccm kupewa michango sii kwetu wananchi
 
Ajabu sana leo wasanii washabiki na wanachama wa CCM wanazungumzia wasanii wote mpaka wale wanaoshabikia upinzani.
 
Wanatafuta kick kupitia ukuta,
Pia hao wote wanufaika wa ccm kipindi cha kampeni
 
hata kama tunataka maendeleo nadhani hayawez kuja kwa njia ya UKUTA me naona zpo tu njia nyingine au kama vp jipangeni vzr 2020 mayb mtawin kuliko kujitoa kafara kwa watu ambao hata msaada kwen hawana zaidi ya hasara tu
 
Back
Top Bottom