Wasanii wataofanya video za muziki bila kukaguliwa na Bodi ya Filamu ‘Watakiona cha Mtema Kuni’

real G

JF-Expert Member
Feb 7, 2013
5,227
5,287
Ali-Kiba-AY-Diamond-na-Navy-Kenzo.jpg


Wizara ya Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo imetangaza kuwachukulia hatua kali za kisheria wasanii ambao watakiuka agizo la kufanya video za muziki na kuzitoa bila kukaguliwa na Bodi ya Filamu ili zikaguliwe.

Mkuu wa Kitengo cha mawasiliano wa wizara hiyo, Zawadi Msalla, amewaonya wasanii kuendelea kufanya kazi zao za muziki bila kufuata taratibu.

“Taratibu zinaeleza wazi, kwamba kabla ya kushoot video yako unatakiwa upeleke script ikaguliwe kwanza na baada ya hapo utapewa ruhusa ya kuendelea,” alisema Msalla.

“Sasa hivi tutakuwa wakali kweli hili, hili ni swala la kisheria taratibu ziko hivyo, kwa hiyo nikufuata taratibu tu,” aliongeza.

Kwa upande wa Mwanasheria wa Wizara ya Habari amesema msanii kuendesha kazi bila ya kuzingatia sheria ni kosa huku akiwataka wasanii kupeleka kazi zao Bodi ya Filamu kukaguliwa kabla ya kutoka.

“Snura hajajisajiri, ametoa kazi bila ya kupata kibali pamoja na kuitoa nyimbo bila ya kuipeleka sehemu husika kwa ajili ya kuifanyia ukaguzi ili kuithibitisha kama inafaa,” Mwanasheria alimtolea mfano Snura.
 
~~~>>>Wakikiuka Mashart kamata peleka Segerea Week tatu na bakora 12..... Sita wakiingia na Sita wakitoka.
 
Ni kilele za chura ndio zimewaamsha? ashukuliwe chura
 
Inawezekana hawapeleki kwenye vituo vyenu vya TV iweje iwe nongwa!?
 
Back
Top Bottom