sinza pazuri
JF-Expert Member
- Aug 16, 2014
- 2,525
- 7,377
Picha hii inamuonesha Nash MC, mmoja kati ya wasanii wa Hip Hop Nchini
Ni wazi muziki wa hip-hop wa bongo umepotea kabisa. Wasanii wa hip-hop hawafanyi vizuri sokoni yani kwa sasa bongo ukiimba hip-hop unaonekana kama umechanganyikiwa. Tofauti na zamani kidogo hiphop ulikuwa inafanya vizuri sana.
Sasa huu muziki umefikaje hapa?
Wasanii wa hip-hop ndio chanzo.
Kwanza, hawataki kubadilika kuendana na soko linachotaka.
Pili, hawawezi kujibrand yani unakuta msanii mchafu kavaa makubazi anakula kashata mitaani hawezi kuvutia makampuni kumtumia kama image ya biashara zao.
Tatu, wasanii wa hiphop kila mtu mjuaji umkute Wakazi, Roma, Niki Mbishi sijui Nash MC wao wanajua kila kitu hawataki kujifunza.
Nne, usela wa kizaman tuliitaga usela nondo. Kujifanya umepinda unakaza, mtu akifanya mambo ya maana utasikia sio real huyo wana zile wanaita wanatunza misingi mara wanaokoa mitaa imagine mtaa uokolewe na mvuta ganja mmoja aliyekwama maisha 😄😄
Tano, kupenda lawama hakuna wasanii wenye lawama nchi hii kama watu wa hiphop wanasemaga muziki wao unabaniwa ila wakiambiwa wabadilike kidogo kuendana na soko wanakuwa wakali sijui kwa kuwa vipaji vyao haviruhusu kubadilika 🤔🤔 sasa nani atafanyia promotion bidhaa isiyo na soko
Mwisho nawashauri watu wa hiphop wabadilike muziki unazidi kuwaacha, Prof J alikuwa nominated MTV awards lakini kizazi cha leo ikitoka list ya wasanii wanaofanya vizuri kwenye hiphop Africa huwezi waona ukiuliza bongo hiphop mbona hatuwaoni utaambulia matusi au kumlaumu Sallam Mendez au watajifichia kuwa wao hawaimbii tuzo wanaimbia vijana wa mitaani 😂😂
Ni hayo tu watu wa hiphop msitafute wa kumlaumu tatizo ni nyinyi wenyewe...unakunywa double kick muda wote alafu unataka upewe show mil 10 inawezekana vipi