Sikiliza baadhi ya kazi za wasanii kutoka Tabora, wanahitaji sapoti yenu

Feb 6, 2024
40
50
Habari za wakati huu wadau wa Muziki natumai mmeamka salama.

Wapenzi wa Muziki Aina ya Hip Hop nina imani mnaitambua vyema Historia ya Muziki huu, Muziki huu Asili yake ni nchini Marekani, lakini kibongo bongo Muziki huu ulishirika "Hatamu" Miaka 1990 na kuna makundi kibao ya Muziki wa Hip Hop yalioanzishwa Miaka Hiyo, lakini pia kuna movement kibao pia zilianzishwa na vitu vingine kama hivyo.

Kwa siku ya leo nawaleta kwenu wasanii wanaofanya Muziki wa Hip hop kutoka kijijini cha Kayombo, kijiji kinachopatikana katika wilaya ya Nzega, mkoa wa Tabora.

Wasanii hawa wanafanya Muziki aina ya Hip hop, wamekwishafanya kazi kibao na mastaa kibao ndani ya Bongo, sema bado hawajapata chance ya kutoboa kimuziki.

Wasanii hawa wanafahamika sanaa mtaani kwao; PK, TOLO, Hamisi.

Kuna kazi kadhaa wamefanya ila kuna ngoma ambayo wametumia beat ya producer kutoka studio za Togwe Records, kiukweli wasanii hawa wamefanya kweli.

Wadau naombeni mwenye connection na producer Bin laden kutoka Studio za Tongwe aweze kunisaidia kufikisha ujumbe huu kwa mwamba.

Maana raia wameitendea haki hiyo beat.

Salute

#funguka.

Nichek kupitia hizi namba: 0767542202/ 0784486100

Sikiliza hizi ngoma kama kweli unathamini cha kwetu kutoka kwa real MS's from Kayombo village, Nzega Tabora.

Am out.
 

Attachments

  • 17089339936373016561853323525740.jpg
    17089339936373016561853323525740.jpg
    275 KB · Views: 10
Niaje wadau?

Sikilizeni kazi za wasanii kutoka Kayombo, kijiji kinachopatikana wilaya ya Nzega mkoa wa Tabora.

Wanafanya Muziki Aina ya Hip Hop, wamekwisha fanikiwa kutoa kazi kadhaa, lakini hizi hapa chini ni baadhi ya kazi zao walizofanya.

Mwenye connection na producer Bin Laden kutoka studio za Togwe Records na msanii Roma naombeni namba zao, naombeni support yenu, vijana wanaweza muziki.
 
Togwe records - Tongwe records
MS's - MC's

Ukiachana na wao kufanya uchenguaji(Emceeing), wanaweza pia kufanya breakdance na graffiti?

Kwa nini Bin Laden na sio producer mwingine?

Ukinijibu hayo maswali nakutumia fasta namba ya Bin laden
 
Togwe records - Tongwe records
MS's - MC's

Ukiachana na wao kufanya uchenguaji(Emceeing), wanaweza pia kufanya breakdance na graffiti?

Kwa nini Bin Laden na sio producer mwingine?

Ukinijibu hayo maswali nakutumia fasta namba ya Bin laden
Ndio huo uwezo wanao kwenye event mbalimbali za serikali tumeshuhudia uwezo wao, changamoto yao kuwa ni ile halo kuwa wao wapo kijijini,

Kuhusu inshu ya bin laden kuna kazi wamefanya KWA kutumia instrumental ya producer huyo Bin laden.

Ingawa sio official coz hiyo beat imetumika kwenye Ngoma ya roma.
 
Mafanikio mema kwenu , mcheki Roma insta au Twitter mtafanya kitu . Zingatia namna ya kum - approach
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom