Wasanii ni njaa imetawala au mnalazimishwa kumuimba Rais Magufuli na CCM

Yote sawa njaa na kulazimishwa kujipendejeza bila hivyo basata iko kazini si unajua chuki ya awamu hii tena?
 
Uchaguzi ni biashara kama biashara nyingine tu, waache wasanii watumie fursa.
 
Kwani wasanii hawaruhusiwi kuwa wanachama wa chama Fulani? Kwani Marehemu MWANACOTIDE na BABA LEVO kilichowapeleka CHADEMA ni njaa au vitisho?
Wanaruhusiwa kuwa CCM tu ukiwa chama cha upinzani unatekwa. Wapi Roma Mkatoliki?
 
Kuelekea Uchaguzi Mkuu naona imekuwa fashion kwa wasanii kila mmoja anatoa nyimbo za kumsifu Magufuli na CCM.

Hii si bure lazima kuna kitu kinaendelea nyuma ya pazia.

Inawezekana kabisa njaa imetawala kwa wanamuziki labda kutokana na janga la Covid-19 lililotukumba hapo nyuma. Au wanamuziki wanapokea vitisho na kulazimishwa kutoka juu waunge mkono juhudi. Yawezekana pia kuna donge nono wasanii wanahongwa kuikamilisha hii agenda.

Niwashauri baadhi ya wasanii wenye fan-base ndogo wabakie tu neutral kuna maisha baada ya uchaguzi.

Unakuta msanii akitoa nyimbo anapata view laki mbili kwa mwezi mzima halafu bado unawagawa mashabiki wako kwa siasa za kuwanufaisha wengine.
Ikiwa Mondi ana njaa sasa sijui wewe una nini!
 
Mimi ni Musician ,Niliwahi kufanya kampeni Zanzibar 2005 "hakuna pesa ya Maana" Hawa Wasanii Si njaa na hakuna vitisho ingawa Kusema kweli uchaguzi mwaka huu Wasanii wengi wametoa nyimbo ,ila wengi wao wanatumia fursa kujijenga .😅
 
Kuelekea Uchaguzi Mkuu naona imekuwa fashion kwa wasanii kila mmoja anatoa nyimbo za kumsifu Magufuli na CCM.

Hii si bure lazima kuna kitu kinaendelea nyuma ya pazia.

Inawezekana kabisa njaa imetawala kwa wanamuziki labda kutokana na janga la Covid-19 lililotukumba hapo nyuma. Au wanamuziki wanapokea vitisho na kulazimishwa kutoka juu waunge mkono juhudi. Yawezekana pia kuna donge nono wasanii wanahongwa kuikamilisha hii agenda.

Niwashauri baadhi ya wasanii wenye fan-base ndogo wabakie tu neutral kuna maisha baada ya uchaguzi.

Unakuta msanii akitoa nyimbo anapata view laki mbili kwa mwezi mzima halafu bado unawagawa mashabiki wako kwa siasa za kuwanufaisha wengine.

Nashindwaga kuelewa watu kama nyie Hapo tu. Nini maana ya Demokrasia na uhuru binafsi wa mtu. Sons of Contradictions.
 
Wanao uhuru huo kama itakuwa wanafanya kwa mapenzi yao. Mimi nina wasiwasi tu mkuu huenda ni njaa, vitisho au kuna fungu kutoka hazina.
Wakifanya kwa mapenzi yao watapotea bora wafanye kwaajili ya pesa ili wakipotea mfukoni kuwe vizuri
 
Nashindwaga kuelewa watu kama nyie Hapo tu. Nini maana ya Demokrasia na uhuru binafsi wa mtu. Sons of Contradictions.
Demokrasia inakataa watu kushurutishwa kufanya jambo au kutumia hongo. Wasanii inaonyesha wanajikomba kusudi either kwa njaa (vyuma kukaza) au wanshurutishwa kuunga juhudi au kuna kahakiba kilichobaki hazina kinatumiwa.
 
Back
Top Bottom