Tumpongeze Rais Magufuli kwa kubadili siasa za Tanzania kuwa si matukio, vita za madaraka na ulaghai. CCM mpya hakika ni mpya.

KARLO MWILAPWA

JF-Expert Member
Apr 10, 2019
1,669
2,000
Moja ya mambo ambayo watanzania watayakumbuka kwa Rais wa sasa pale akistaafu ni kuacha mfumo wa kisiasa unaojiendesha wenyewe na si ule unaondeshwa kwa matukio, vita ya madaraka na ulaghai. Mfumo huu wa kisiasa ambao Rais anaujenga utasaidia upatikanaji wa viongozi bora na wenye uwezo wa kuongoza na kufanikisha malengo tofauti na ule unaotawaliwa na matukio, vita ya madaraka na ulaghai. Tanzania kwa sasa inashuhudia mageuzi makubwa sana kwenye siasa zake ambazo ni msingi mzuri wa maendeleo. Nikimnukuu Mwalimu Nyerere ‘ ili nchi iendelee inahitaji watu, ardhi, sera/siasa safi na uongozi bora’. Mwalimu Nyerere alituonya athari zitakazoikumba taifa kama siasa zitakuwa za matukio, vita ya madaraka na ulaghai na badala yake akatuasa kuwa na siasa safi.

Leo Mwalimu hayupo wa kutuasa na kutuonya lakini maneno ya mwalimu yanaishi ndani ya viongozi wazalendo, wenye nia madhubuti ya kuendeleza siasa safi na mmojawapo ni Rais Magufuli. Kizazi hiki kinaishi katika zama za kushuhudia yaliyofanywa, yaliyoonywa na yaliyosemwa na uongozi wa awamu ya kwanza kupitia Rais Magufuli. Rais Magufuli anatukumbusha historia muhimu ya ujasiri na mapambano ya mwalimu ambaye leo kuna wanasiasa wanambagaza.

Tukirudi nyuma miaka kama 15 iliyopita, ndipo siasa za matukio, vita ya madaraka na ulaghai zilipoasisiwa, kushamiri na kunawiri na watu kuanza kuona msingi wa kuwa siasa safi ni wa kizamani. Hakika nchi ilikuwa kila kukicha watu wanawaza migomo na maandamano na kuachana na msingi wa mwalimu aliyekuwa anaamini siasa ni kazi. Siasa za matukio zikawa zimeenea na kufanya shughuli za maendeleo na kazi za watu kusimama kupisha maandamano, baadhi ya vijana walikuwa hawana mawazo mbadala Zaidi ya kushiriki maandamano na migomo. Tangu kuingia kwa Rais Magufuli vijana wana ari na hamasa ya kufanya kazi, siasa za matukio, maandamano, migomo mitaani, vyuoni na kwingineko zimeisha na watu wamerudi kwenye misingi ya mwalimu ya siasa ni kazi

Miaka ya nyuma kipindi kama hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu upande wowote wa muungano ambapo ilikuwa lazima apatikane mtu mwingine baada ya aliyopo kumaliza ngwe yake joto la kisiasa lilikuwa kali si kwa CCM tu hata kwa upinzani kwa ujumla. Kwa upande wa Zanzibar ambapo Dkt. Shein anamaliza muda wake mwakani, ingekuwa ni kipindi cha siasa za vita ya madaraka hakika joto lake lingekuwa kubwa ila leo ni kama hamna kitu. Hali ni shwari, watu wanapiga kazi , wapiga ramli wanaojifanya watabiri wapo kimya na hii yote ni kwa sababu ya mwenyekiti wa CCM taifa Dkt. Magufuli kuhubiri siasa safi kwa ajili ya ujenzi wa taifa letu.

Siasa za utapeli katika awamu hii zimekufa. Wale wagombea ubunge na udiwani waliokuwa wanaahidi wasiyoweza ili kuwalaghai wananchi wanaona mwisho wao wa kuwa wabunge umefika. Wote walioshindwa kutekeleza ahadi na kuwaletea wananchi maendeleo wanaona hawana nafasi tena. Leo ni nadra kuona mbunge anakaa miaka miwili bila kutembelea jimbo lake ila zamani ilikuwa ni kawaida mbunge kumaliza miaka mitano bila kukanyanga jimboni na anakanyaga tena wakati wa uchaguzi. Yote hii ni kutengeneza mfumo wa kisiasa unaojiendesha wenyewe bila kuendeshwa na matukio, ulaghai na madaraka na mfumo wenye nia ya kukuza na kuleta viongozi bora.

Wito:

Kwa ufupi hapo juu nimetoa mwangaza wa mfumo ambao Rais Magufuli anaujenga kwa maslahi mapana ya nchi yetu, jukumu letu sisi watanzania ni kumuunga mkono. Kwa sababu mabadiliko hayo yameanzia CCM na kwa kuwa Rais ndiye mwenyekiti wa CCM taifa ambaye atakuwa ndie mwenye jukumu kubwa la kuchuja wale wote walioshindwa kufanyia kazi ahadi zao ndani ya CCM na wale walioshindwa kuwaletea watanzania maendeleo, tumuunge mkono kwa KUCHAGUA WABUNGE, MADIWANI NA WENYEVITI WA SERIKALI ZA MITAA WA CCM naye atawahakikishia kupata viongozi bora kama alivyo yeye.
 
emmanuel mruma

JF-Expert Member
Feb 14, 2017
1,563

hakuna anaeweza kuzuia siasa ya vita hata siku moja yaani haiwezekani, nyerere tu pamoja nakuwa baba wataifa tena aliekaa muda mrefu madarakani hakuweza...je magufuli aliebakia na miaka 5 tu ataweza kubadilisha mfumo wa siasa. ..yani mm naona siasa za vita na chuki na makundi ndio yanarudi kwa kasi, kama huamin subiri magu apite 2020, then subiri 2023 akibakiza tumiaka tu wili tu madarakani, nguvu yake itapungua sana atapuuzwa na watu wa chama na vita itakolea kupita kiasi. ..hawa wanaotumbuliwa na kupigwa chini leo wataibuka mara 10000 2025
 
Tate Mkuu

JF-Expert Member
Jan 24, 2019
8,319
2,000
wagombea wa CCM pekee wanatosha

Sasa nini maana ya kuchagua mfumo wa vyama vingi! Ngoja siku yenu ifike, tutawacharaza bakora kokote kule mtakako onekana na kuwagaragaza kwenye madimbwi ya maji machafu na hizo nguo zenu za kijani zitageuka kuwa matope.
 
KARLO MWILAPWA

JF-Expert Member
Apr 10, 2019
1,669
2,000
hakuna anaeweza kuzuia siasa ya vita hata siku moja yaani haiwezekani, nyerere tu pamoja nakuwa baba wataifa tena aliekaa muda mrefu madarakani hakuweza...je magufuli aliebakia na miaka 5 tu ataweza kubadilisha mfumo wa siasa. ..yani mm naona siasa za vita na chuki na makundi ndio yanarudi kwa kasi, kama huamin subiri magu apite 2020, then subiri 2023 akibakiza tumiaka tu wili tu madarakani, nguvu yake itapungua sana atapuuzwa na watu wa chama na vita itakolea kupita kiasi. ..hawa wanaotumbuliwa na kupigwa chini leo wataibuka mara 10000 2025
binafsi ninaamini kwamba siasa za vita ya madaraka zimepungua na kwa kadiri muda unavyoenda zitaisha kabisa. kinyume na matarajio ya wengi, leo mtu asiye na umaarufu ila ana uwezo wa kuongoza anaweza kugombea na akashinda kinyume na zamani. Mabadiliko makubwa ya kisiasa nchi yameamsha ari na hamasa ya vijana na wasomi kuingia kwenye siasa.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom