Ili bidi tu hawa jamaa hawa jamaa wafe kisabuni katika mwaliko wao huku Ikulu jana maana kama mnavyoona hakuna cha maji ya uhai wala filigisi wala mapaja ya kuku na mayai ya kuchemsha kama tulivyozoea hafla kama hizi huko nyuma.
Kikubwa Mh JPM alichofanya ni kuwaonyesha bomba la maji kupitia dirishani na kuwaambia kama mtu anasikia kiu basi anaweza kwenda kukata kiu kwenye bomba ya maji ile paleeeeeee!
Mh Abdallah Bulembo ndiye iliyekufa kinyasa babu kubwa kwa sababu ni majuzi tu greda lilitoka kupiga deki sehemu yao waliyoluwa wanapatia ruzuku pale Sinza dagaa dagaa na wote mliona alivyokuwa anatoa povu, sasa katika mwaliko wa jana huyu bwana aliaambulia kukaa high table,labda nimedokezwa ni mtoto wake wa kike kaambulia ubunge wa viti maalumu.
Wasanii wengi wameenda kwenye mwaliko huo wengi wakiwa teyari wameisoma namba
Wangine wana madeni makubwa na wana kesi mahakamani CCM imewanawa, wengine mamepolomowa mimba walizopewa wakati wa kampeni, wengine nyumba zao zimevunjwa walizijenga maeneo hatarishi, wengine waliahidiwa kwenda kufanya show inje ya nchi safari za nje zimeota mbawa.
Kwa hiyo ki ukweli jana wengi walikuwa pale kimwili tu lakini rohini walikuwa mbali sana ndiyo maana tunasema wamekufa kinyasa na tai shingoni.