Wasanii kuweni makini Ruge anawachonganisha | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wasanii kuweni makini Ruge anawachonganisha

Discussion in 'Celebrities Forum' started by Yo Yo, Nov 25, 2011.

 1. Yo Yo

  Yo Yo JF-Expert Member

  #1
  Nov 25, 2011
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 11,247
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 0
  Kama mdau wa muziki kwa muda sasa nafuatilia bifu la Ruge V/s Sugu na wasanii wenye uchungu na kazi zao.

  Huyu Ruge sio mzaha jamaa anawanyonya sana wasanii ana anachukua ujinga na elimu yao finyu kuendelea kwuakandamiza...jana nimesikia clouds wameandaa tamasha najua hii ni kulifanya tamasha la sugu likose shangwe.

  Katika list ya wasanii wapi Manzese Crew,Afande sele na wengine.....hawa ni moja ya watu ambao nyimbo zao zilikuwa hazipigwi redioni kisa walijitambua na uwizi wa Ruge na Clouds......Sugu kwenye tamasha lake alitangaza wasanii hao watakuwepo na wata perfom na Ruge katia ndimu nae kawatangaza watakuwepo......

  .....Nawashauri wasanii wawe makini na Ruge anawachonganisha sio mtu mzuri kwenye maisha yao ya muziki
   
 2. sulphadoxine

  sulphadoxine JF-Expert Member

  #2
  Nov 25, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,264
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Ruge anaweza akawa sio tatizo,bali tatizo ni wasanii wenyewe,na kikubwa ni ujnga na kukosa elimu (kutojitambua).

  Kwa hiyo Ruge anatumia huu mwanya wa ujinga na kuwanyonya kwa kuwapa ujira mdogo sana.Angalia mtu kama afande Sele, nyimbo zake zilikuwa hazipigwi Clouds hata siku moja, ila juzi wameanza kuzipiga kisa tu, Sugu alitangaza kuwa afande sele atakuwepo kwenye show yake pale ustawi,siku ya Jumamosi, kwa hiyo Clouds FM (wafu fm)wanatumia mwanya huu kuchonganisha wasanii.

  Afande Sele, alitakiwa kuwa na msimamo sio kuyumba na hilo ndio tatizo linalo wasumbua wasanii bongo, Dj Fetty kuna kipindi alimponda sana Afande Sele, nayeye mwenyewe analijua hilo lakini kasaau na tayari ametangaza kutokwenda kwenye show ya Sugu...
   
 3. Who Cares?

  Who Cares? JF-Expert Member

  #3
  Nov 25, 2011
  Joined: Jul 11, 2008
  Messages: 3,465
  Likes Received: 1,950
  Trophy Points: 280
  "mtu akijua kuwa una akili timamu na zakutosha akakuambia upuuzi na ukaukubali..atakudharau sana milele na milele ameen"....(haya maneno aliyasema hayati mwl. J.k. Nyerere)

  ruge akijua mwanamziki wa bongofleva una akili...akakuambia upuuzi (wa kufanya shoo ulipwe tsh 100,000/- wakati dmx analipwa usd 300,000 (tshs 500,000,000/=) ukakubali..ruge atawadharau sanaaa milele na milele ...ameeen
   
 4. Who Cares?

  Who Cares? JF-Expert Member

  #4
  Nov 25, 2011
  Joined: Jul 11, 2008
  Messages: 3,465
  Likes Received: 1,950
  Trophy Points: 280
  Hivi...dj fetty "anawezaje" kumtukana afande sele???...nisaidieni jamani maana naona kama sielewi vile...kitoto cha kike kinamtukana babayake tunda..mfalume selemani msindi???..how?...hiyo kibri kaitoa wapi huyu binti...

  Amepata malezi ya pande zote ..au ndo wale waloanza kutoka miguu wakati wa kuzaliwa???....bado sielewi kwann na aliwezaje kumtukana mfalme wa mistari wa mwisho tanzania....
   
 5. Ye Soya

  Ye Soya Senior Member

  #5
  Nov 25, 2011
  Joined: Nov 24, 2011
  Messages: 187
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Kazi ipo, hii vita nani atakuwa starring? Yangu majicho.
   
 6. b

  bpouz Member

  #6
  Nov 25, 2011
  Joined: May 26, 2008
  Messages: 36
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  jamAn c ndo sugu kamtoa afande sele kimziki alikuwa anavuta bangi pale msamvu katika pita ya sugu afande akamuomba sugu amtoe sugu bila hiyana akampa mwimbo ktk albamu yake "nikianguka sitaweza kunyanyuka" kwel mfadhili mbuzi binamu anamaudhi leo hii anamsaliti mtu aliyemfikisha hapo kimziki hebu ww afande stuka jitambue
   
 7. sulphadoxine

  sulphadoxine JF-Expert Member

  #7
  Nov 25, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,264
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  DJ fetty alishamponda sana afande sele na kumwambia kuwa eti ajui kuvaa,maneno kibao aliongea juzi wamempa airtime Kalapina naye anamponda sugu anasema yeye(kalapina)ndio mwasisi wa hip hop sasa hii kitu mbona kichekesho sana who cares? umeongea point sana tatizo ni njaa za wasanii mtu kalapina kuna kipindi aliazisha hizi harakati ambazo sugu amezianzisha tena lakini alishindwa clouds wanamwita wanampa airtime kwa radio yao anaongea ujinga na kuwaponda wasanii wenzake.
   
 8. sulphadoxine

  sulphadoxine JF-Expert Member

  #8
  Nov 25, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,264
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Leo afande sele hilo alioni huu ndio ujinga nao usema (kutojitambua na kutokumbuka ulikotoka)
   
 9. Faru Kabula

  Faru Kabula JF-Expert Member

  #9
  Nov 25, 2011
  Joined: Mar 26, 2009
  Messages: 10,642
  Likes Received: 2,877
  Trophy Points: 280
  Mimi naona hiyo ya Afande Sele kwenda kwa Ruge ni moja ya mafanikio ya tamasha la Sugu, kwani kwa sasa Ruge/Clouds wataanza kupiga nyimbo za Sele redioni na kwenye TV yao, otherwise bila ya Sugu kuweka tamasha hilo, Clouds wangeendelea kumchunia Sele. Kwa hiyo Afande Sele itabidi amshukuru Sugu kwa kuifanya Clouds ilazimike kupiga nyimbo zake
   
 10. WAFU FM

  WAFU FM Member

  #10
  Nov 25, 2011
  Joined: Nov 24, 2011
  Messages: 49
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Unashangaa afande sele, alitukanwa prof jay kama mtoto na dada b 12 kisa alichelewa basi wakati wanaenda show ya fiesta mbeya na jay akakaa kimya ka cameroon wasanii wa kibongo aibu tupu utaumiza kichwa kuwapigania wakat wao wenyew hawajui thamn yao
   
 11. Mzee Wa Rubisi

  Mzee Wa Rubisi JF-Expert Member

  #11
  Nov 25, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 1,754
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Hapo Ruge atachemusha Grama kubwa bila ya sababu,
   
 12. sulphadoxine

  sulphadoxine JF-Expert Member

  #12
  Nov 25, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,264
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Mkuu Uhuru!afande awezi kumshukuru tena sugu,kwasababu afande ni kigeugeu(wasanii,wanasiasa wote vigeugeu)
   
 13. sulphadoxine

  sulphadoxine JF-Expert Member

  #13
  Nov 25, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,264
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Sasa hivi muda mwingi wanatumia kuwapa airtime wasanii kama kalapina ili wamponde sugu na kundi lake.
   
 14. mtzd

  mtzd Member

  #14
  Nov 25, 2011
  Joined: Jan 29, 2010
  Messages: 81
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  Hawa wasanii wetu sijui ni kutokwenda shule au,Nimekua kwenye hii industrty ya entertainment kwa muda mrefu bt ukweli kwa hapa bongo sioni progressive yoyote nilipokua nimejifunza mengi nakaja nayo na kujaribu kuwaelimisha baadhi ya wasanii ,ukweli wale waliyachukua nafurahi kwamba naona maendeleo yao bt wengine dah we acha tu,mtu uimbe ww then afaidike mwingine,igeni mifano ya wenzenu wa nje ,sio hata mbali sana,jirani tu kwa kina Kibaki na Raila,wasanii wana uwezo wa kujiandalia shoo zao wenyewe na wakatengeneza mikwanja ya kufa mtu hata wanapata shoo za mamtoni,tujaribu kujiuliza kwa hapa bongo ni wasanii wangapi wanaenda nje kufanya shoo.kama sio wawili au watatu cjui.Na hao ni wale wenye upeo wa kuona mbali.,Mkeni wasanii wetu acheni kunyonywa na wachache kwa faida zao.Mjaribu pia kuwa na wanasheria wenu ,msanii unakuja na idea yako bt baada ya mda unaskia kuna mtu au kikundi cha watu wamechukua idea yako na kwenda kuifanyia kazi kwa maslai yao.Na hawa BASata hivi kazi yao ni nini kwa kweli.
   
 15. M

  Maganiko Senior Member

  #15
  Nov 25, 2011
  Joined: Feb 20, 2011
  Messages: 131
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mheshimiwa sana Bob Marley alishasema katika wimbo wake wa ukombozi (Redemption song) kwamba "Emancipate yourselves from mental slavery...none but ourselves can free our mind!"

  Sugu alishajitambua kitambo ndo sababu anafanikiwa...hawa wengine bado sana, utumwa wa kimawazo wa kudhani Wafu FM ndo kila kitu unazidi kuwafunga minyororo ya kunyonywa na Wafu FM.

  Ni uchaguzi wao, Sugu kawaonesha njia.
   
 16. sulphadoxine

  sulphadoxine JF-Expert Member

  #16
  Nov 25, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,264
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Ruge anafanya kila awezalo ili aweze kurudisha hizi harakati nyuma.Lakini naamini mungu atasimama upande wa sugu.
   
 17. k

  keke Senior Member

  #17
  Nov 25, 2011
  Joined: Aug 10, 2011
  Messages: 108
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  maskini wasanii wetu, hawana msimamo hata kidogo, tatizo ni ufinyu wa Elimu na Ugumu wa maisha.
   
 18. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #18
  Nov 25, 2011
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Njaa mbaya huyo anaweza pewa pesa amtukane baba yake nae akafanya hivyo kwa sababu tu ya njaa
   
 19. Horseshoe Arch

  Horseshoe Arch JF-Expert Member

  #19
  Nov 25, 2011
  Joined: Aug 10, 2009
  Messages: 11,230
  Likes Received: 4,951
  Trophy Points: 280
  R.I.P sanaa ya Bongo..mbwembwe,majivuno,migogoro,na maisha yasiyo na uhalisia....ugomvi wa Sugu na Ruge mwisho wake nini!...kwanini wanachezea hisia za watu...kwanini wanagawa watu...kwanini wanatumia nafasi zao vibaya...why! Kwanini...
   
 20. engmtolera

  engmtolera Verified User

  #20
  Nov 25, 2011
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 5,081
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  dont underestimate your power to change yourself

  Namkubari Mh Sugu ni mtu anae jitambua na kuitambua haki yake,si mtu wa kukurupuka ndio maana vijana na wazee waliowengi wanamkubari
  Kaanza kitambo sana kuimba na hakuna aliweza kumsaidia hadi hapo alipofikia,huwezi kumfananisha na Msindi Mvuta bangi asiweza kujitafutia hadi atafutiwe,huwezi kumfananisha na akina kibonde wanaopata pesa kwa kuwasema watu vibaya

  hakika Sugu ni JEMBE
  MUNGU azidi kukupa nguvu na niimani yangu kuwa utafika mbali na utafanikiwa ktk kujaribu kuwatoa na kuwapa elimu wasanii wasiojitambua wajitambue na wazinduke
   
Loading...