Missile of the Nation
JF-Expert Member
- May 24, 2018
- 13,498
- 51,092
Watu wa sayansi wana kitu wanakiita saturation point, yaani ni point ambayo hata ukiongeza kitu fulani kilichokuwa na matokeo chanya kwenye mchakato fulani hapo awali, basi kitu hicho kinakuwa hakina msaada tena kwenye kuuongezea kasi mchakato huo.
Sasa kwa kampeni hizi za CCM, Wasanii kweli walisaidia kuvutia umma kuja kwenye mikutano ya mgombea wa CCM ndugu Magufuli, lakini sasa suala linalokuja ni kuwa je Baada ya Wasanii what next?
1. Je, Utaendelea kubeba wasanii na kurudi nao katika mikoa ambayo umeshaenda nao tayari?
2. Utaweza kubeba wasanii na kwenda nao kila jimbo la kila mkoa?
Kinachofuata baada ya burudani ya wasanii wananchi wanataka kusikia sera. Na wananchi wetu wana ufahamu, wanajua ipi ni burudani waifurahie na ipi ni sera kwa ajili ya kuboresha maisha yao!
CCM isitegemee eti itapewa kura na wananchi wengi kwa sababu imewapelekea mauno ya Diamond, au mikogo ya Zuchu au amsha amsha ya Harmonize.
Wananchi ni waelewa sana wanataka kuelezwa kwa nini CCM haijatimiza ahadi za Ilani yake uchaguzi ya mwaka 2015,na hivyo wanaiuuliza kwa nini iaminiwe kwa ilani ya sasa ya mwaka 2020. Kama ilishindwa kutimiza ahadi zilizomo kwenye ilani ile ya mwanzo, iaminiweje kutimiza ahadi za ilani mpya?.
Kwa mfano wananchi wanataka kujua
1. Ziko wapi milioni 50 kila kijiji
2. Iko wapi Katiba mpya
Lakini pamoja na hayo wananchi wanataka kujua
1. Kwa nini serikali haikupandisha mishahara ya watumishi wa umma iliyoko kisheria, na ikiingia itafanya nini kuhusu malimbikizo ya madai yao?
2. Wananchi wanataka kujua ina mpango gani wa kulinda usalama wa wananchi dhidi ya wasiojulikana na itafanya lini uchunguzi kuhusu matukio ya utekwaji na kupotea kwa watu nchini.
3. Serikali ina mpango gani kuhusu ajira za vijana wetu, kufufua na kujenga viwanda vipya, kuboresha kilimo, elimu, Afya n. k. Tena wanataka kusikia mpango kwelikweli siyo maneno ya jumlajumla tu ambayo hayajashiba taarifa
Sasa mambo hayo hayapatikani kwenye mauno au mikogo ya Zuchu, yanapatikana kwa wagombea wenyewe.
CCM haihitaji kutumia gharama nyiingi kuburudisha wananchi kwenye Disko za mchana wanazozianda, bali wanahitaji kupiga kampeni zenye kuelezea masuala ya wananchi na haya ndo wananchi wanayohitaji zaidi kuyasikia.
Kwa phase hii ya kampeni tuliyopo, Wasanii hawaisaidii tena CCM. Wasanii ni kama wachawi wa Firauni/Farao, hawana msaada tena kwa Farao.