Uchaguzi 2020 Wasanii hawawasaidii tena CCM, Watu wanataka kusikia kuhusu masuala yanayohusu nchi yao!

Missile of the Nation

JF-Expert Member
May 24, 2018
8,380
2,000
Watu wa sayansi wana kitu wanakiita saturation point, yaani ni point ambayo hata ukiongeza kitu fulani kilichokuwa na matokeo chanya kwenye mchakato fulani hapo awali, basi kitu hicho kinakuwa hakina msaada tena kwenye kuuongezea kasi mchakato huo.

Sasa kwa kampeni hizi za CCM, Wasanii kweli walisaidia kuvutia umma kuja kwenye mikutano ya mgombea wa CCM ndugu Magufuli, lakini sasa suala linalokuja ni kuwa je Baada ya Wasanii what next?

1. Je, Utaendelea kubeba wasanii na kurudi nao katika mikoa ambayo umeshaenda nao tayari?

2. Utaweza kubeba wasanii na kwenda nao kila jimbo la kila mkoa?

Kinachofuata baada ya burudani ya wasanii wananchi wanataka kusikia sera. Na wananchi wetu wana ufahamu, wanajua ipi ni burudani waifurahie na ipi ni sera kwa ajili ya kuboresha maisha yao!

CCM isitegemee eti itapewa kura na wananchi wengi kwa sababu imewapelekea mauno ya Diamond, au mikogo ya Zuchu au amsha amsha ya Harmonize.

Wananchi ni waelewa sana wanataka kuelezwa kwa nini CCM haijatimiza ahadi za Ilani yake uchaguzi ya mwaka 2015,na hivyo wanaiuuliza kwa nini iaminiwe kwa ilani ya sasa ya mwaka 2020. Kama ilishindwa kutimiza ahadi zilizomo kwenye ilani ile ya mwanzo, iaminiweje kutimiza ahadi za ilani mpya?.

Kwa mfano wananchi wanataka kujua

1. Ziko wapi milioni 50 kila kijiji
2. Iko wapi Katiba mpya

Lakini pamoja na hayo wananchi wanataka kujua
1. Kwa nini serikali haikupandisha mishahara ya watumishi wa umma iliyoko kisheria, na ikiingia itafanya nini kuhusu malimbikizo ya madai yao?

2. Wananchi wanataka kujua ina mpango gani wa kulinda usalama wa wananchi dhidi ya wasiojulikana na itafanya lini uchunguzi kuhusu matukio ya utekwaji na kupotea kwa watu nchini.

3. Serikali ina mpango gani kuhusu ajira za vijana wetu, kufufua na kujenga viwanda vipya, kuboresha kilimo, elimu, Afya n. k. Tena wanataka kusikia mpango kwelikweli siyo maneno ya jumlajumla tu ambayo hayajashiba taarifa

Sasa mambo hayo hayapatikani kwenye mauno au mikogo ya Zuchu, yanapatikana kwa wagombea wenyewe.

CCM haihitaji kutumia gharama nyiingi kuburudisha wananchi kwenye Disko za mchana wanazozianda, bali wanahitaji kupiga kampeni zenye kuelezea masuala ya wananchi na haya ndo wananchi wanayohitaji zaidi kuyasikia.

Kwa phase hii ya kampeni tuliyopo, Wasanii hawaisaidii tena CCM. Wasanii ni kama wachawi wa Firauni/Farao, hawana msaada tena kwa Farao.
 
G'taxi

JF-Expert Member
Sep 15, 2013
4,609
2,000
Sijataka hata kusoma upuuzi wote mpaka mwisho lakini kichwa cha habari yako kinajieleza na binafsi ninajibu ya kwamba..sisi wananchi wanyonge tunamuelewa sana JPM na kipindi hiki mpaka ninyi mlio jifyatua akili mtakuja kukikumbuka sana huko mbeleni na kutamani JPM angerudi mamlakani kunyoosha nchi
 
Frank Wanjiru

JF-Expert Member
Apr 12, 2012
14,397
2,000
Sijataka hata kusoma upuuzi wote mpaka mwisho lakini kichwa cha habari yako kinajieleza na binafsi ninajibu ya kwamba..sisi wananchi wanyonge tunamuelewa sana JPM na kipindi hiki mpaka ninyi mlio jifyatua akili mtakuja kukikumbuka sana huko mbeleni na kutamani JPM angerudi mamlakani kunyoosha nchi
Wewe ni Mnyonge wa akili mpaka hali yako ya kimaisha.
 
Missile of the Nation

JF-Expert Member
May 24, 2018
8,380
2,000
Sijataka hata kusoma upuuzi wote mpaka mwisho lakini kichwa cha habari yako kinajieleza na binafsi ninajibu ya kwamba..sisi wananchi wanyonge tunamuelewa sana JPM na kipindi hiki mpaka ninyi mlio jifyatua akili mtakuja kukikumbuka sana huko mbeleni na kutamani JPM angerudi mamlakani kunyoosha nchi

Unaona fahari kuwa mnyonge?
 
Pythagoras

JF-Expert Member
Feb 24, 2015
12,903
2,000
Amekusanya wasanii wafuatao.....Pinda, Jk, Sumaye, Nape, Kinana, Makamba, Mwinyi,

Too little too late.😂😂
 
Missile of the Nation

JF-Expert Member
May 24, 2018
8,380
2,000
Amekusanya wasanii wafuatao.....Pinda, Jk, Sumaye, Nape, Kinana, Makamba, Mwinyi,

Too little too late.😂😂

Wanatumi mabilioni kulipa wakata viuno wakati wangeweza kwa fedha hizo kupunguza makali ya waliowavunjia nyumba kikatili, au kusaidia kulipa mafao ya wazee wanaosaga lami kupigania mafao yao!. Hawa jamaa ni wabinafsi mno, kwao madaraka ni priority kabla ya maisha ya watu!
 
Pythagoras

JF-Expert Member
Feb 24, 2015
12,903
2,000
Wanatumi mabilioni kulipa wakata viuno wakati wangeweza kwa fedha hizo kupunguza makali ya waliowavunjia nyumba kikatili, au kusaidia kulipa mafao ya wazee wanaosaga lami kupigania mafao yao!. Hawa jamaa ni wabinafsi mno, kwao madaraka ni priority kabla ya maisha ya watu!
Hehee they like short cuts
 
jaji mfawidhi

JF-Expert Member
Feb 20, 2016
9,358
2,000
wasanii wameenda kuvunja maadili huko mikoani na vijijini, wamekula vitoto vya vyuo huko mikoani, wamesambaza gonjwa la HIV, wamepeleka mila na tamaduni za ajabu na watu wanaona sawa tu.
 
FUSO

JF-Expert Member
Nov 19, 2010
21,655
2,000
CCM mmebadili gia angani, awamu ya tatu ya kampeni ni Mgombea pamoja na timu wafia chama tu, hakuna msanii hata mmoja atapanda jukwaani. Hoja zote za wapinzani zilizotolewa zinakwenda kupata majibu mujarabu!! Stay turned. !!
 
Kibanga Ampiga Mkoloni

JF-Expert Member
Aug 9, 2007
18,465
2,000
Sijataka hata kusoma upuuzi wote mpaka mwisho lakini kichwa cha habari yako kinajieleza na binafsi ninajibu ya kwamba..sisi wananchi wanyonge tunamuelewa sana JPM na kipindi hiki mpaka ninyi mlio jifyatua akili mtakuja kukikumbuka sana huko mbeleni na kutamani JPM angerudi mamlakani kunyoosha nchi

uNAMUELEWA MGOMBEA AU UNALIELEWA uno LA zuchu ?
 
Ikitotanzila

JF-Expert Member
Sep 22, 2020
301
500
Sijataka hata kusoma upuuzi wote mpaka mwisho lakini kichwa cha habari yako kinajieleza na binafsi ninajibu ya kwamba..sisi wananchi wanyonge tunamuelewa sana JPM na kipindi hiki mpaka ninyi mlio jifyatua akili mtakuja kukikumbuka sana huko mbeleni na kutamani JPM angerudi mamlakani kunyoosha nchi
Kuteka watu na kuwaua ndo kunyoosha nchi we mkata kiuno
 
Sky Eclat

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
48,852
2,000
1601279300155.png
 
May 28, 2020
66
125
Sijataka hata kusoma upuuzi wote mpaka mwisho lakini kichwa cha habari yako kinajieleza na binafsi ninajibu ya kwamba..sisi wananchi wanyonge tunamuelewa sana JPM na kipindi hiki mpaka ninyi mlio jifyatua akili mtakuja kukikumbuka sana huko mbeleni na kutamani JPM angerudi mamlakani kunyoosha nchi
Yaaani sikuhizi UNYONGE umekua sifa nzuri
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom