Wakati tumejaza mizoga serikalini Watanzania wataendelea kufa hadi pale watakapobaini kwamba kuwaendekeza mafisadi ni usaliti wa hali ya juu.
Jana tarehe 21/03/2011 taifa lilipoteza wasanii zaidi ya 10 wa kikundi kimoja cha taarab baada ya kupoteza maisha kufuatia basi waliokuwa wakisafiria kutoka mikoa ya nyanda za juu kusini kugonga nyuma ya lori ambalo linadaiwa kuharibika na kisha kutelekezwa barabarani.
................
Lakini kutokana na kujitafutia sifa binafsi, tokea achaguliwe mwaka jana waziri Magufuli amekuwa akihangaika na mambo yanayoweza kumpatia sifa binafsi kama vile kuagiza bomoa bomoa holela kwa madai ya kutekeleza sheria ilihali akiacha wananchi wakiendelea kupoteza maisha, kuwa vilema, mayatima kuongezeka kutokana na sababu ambazo kama sheria za barabara zingekuwa zinatekelezwa kama amabvyo Mhe Magufuli anadai kuzitekeleza vifo hivyo vingeweza kuepukwa.
...hush..hush, now Maria. It is just Satan's work. (Nakwazika mno watu wanaposema ni KAZI YA MUNGU! really? Mungu huyu huyu tunayemjua mwenye wingi wa rehema????)
barabara hata kama zikiwa kama ulaya bado madereva esp wafuasi wa chadema sio watumiaji wazuri wa barabara,na huwa wanaendesha hovyo sana bila kufuata sheria,mfano kwa macho yangu siku slaa alipokuja kutafuta udhamini pale mjini moshi wafuasi wengi wa chadema wakiwa na pikikipi na magari walikuwa wakikimbiza vyombo vyao na kuendesha kwa mbwembwe nyingi sana kiasi cha kusababisha ajari!rip marehemu wote
hapo hakuna siasa ila ukweli ni kuwa serikali inayo simamia miundo mbinu ndiyo inapaswa kubeba lawama zote kwani ajali tz ni nyingi sana na zinasababishwa na miundombinu mibaya
Maskini itakuwa ndo hao 5 star,mimi kama mimi walinipita nikiwa kazini(iringa~mafinga road) pale kilimani palipokuwa na makaburi yenye utata ya kiyeuyeu iringa.Ilikuwa ROSA moja yenye rangi intermediate ya nyeupe na kijivu.BWANA ALITOA NA BWANA AMETWAA,JINA LA BWANA LIBARIKIWE.