Kwa mujibu wa taarifa za TBC leo asubuhi, muimbaji mkongwe Mwanahawa Alli aliyeimba 'Kinyago cha Mpapure' ni mmoja wa majeruhi watano. Alikuwa kwenye safari hiyo kama muimbaji mualikwa. Wakati anahojiwa na muandishi wa TBC anaonyesha kabisa kuwa bado ana mawenge ya ajali na haamini kilichotokea. RIP Five Stars waliotutoka, wanaume saba na wanawake watatu. kwa ataarifa za mwanzo za Clouds Fm zikimnukuu RPC wa mkoa wa Morogoro, Dereva wa Coaster iliyowabeba wasanii hao na kupata ajali, ni mmoja wa walionusurika na ajali hiyo.