Ni kweli kabisa hizo shule za Private zinaendeshwa kitapeli sana .
Kwenye fomu wakati mwanafunzi anaanza wanakuoaghai kuwa mtoto atalipa ada mara nne kwa mwaka yaani Januari,Aprili ,Julai na Septemba anakamilisha Ada yote .
Mtoto akifika Darasa la nne wanaanza Figisu za kusema alipe Ada mara mbili tu . Na wanaanza kumtoa Darasani na kumbughudhi mara kwa mara .
Seikali haina meno maana kila mtu anaangalia mambo yake na familia yake . Waziri anashangaa kusikia mtu ameshinda kulipa Ada yote mil. 3 . Anaona ni kama Efu tatu tu kwake hivyo wala hafuatilii vijihela vidogo kama hivyo kwa mzazi kushindwa kulipa kwa mara moja .
Maana wa uchaguzi lakini hatusikii Kampeni za Mipango ya Tanzania kwenye Elimu, Teknolojia ,ajira , mfumuko wa bei, Kupunguza Kodi,kupunguza ,riba kwenye mabenki, mishahara midogo ,kikokotoo,kupanda kwa bei ya umeme, Ujenzi wa makazi bora na salama na ya bei nafuu kwa watanzania waishio mijini .
Tunachosikia kwa chama Tawala ni vitisho na ushindi ni lazima ,mara ebola ,mara ,mitano tena ,mara tunaenda na mama ,mara .Election sijui no .
Hakuna midahalo ya kuzungumzia Tanzania ya miaka 50 ijayo na nini kifanyike .