Wasaidieni walimu wa Private schools

Wasaidieni walimu wa Private schools

St. Paka Mweusi

JF-Expert Member
Joined
Sep 3, 2010
Posts
7,994
Reaction score
5,231
Salam kwenu.. Nije kwenye hoja.. Hawa walimu wanasikitisha.. Mishahara ni midogo sana.. 200,000/- mpaka 400,000/- kwa mwezi.

Kazi ni kuanzia saa 12 asubuhi mpaka saa 12 jioni. Jumatatu mpaka Jumamosi. Hakuna overtime wald posho.. Lakini wewe mzazi unalipa 2,000,000/- kwa mwaka..

Swali la kujiuliza ni Je huyo mwalimu anayemfundisha mwanao ana thamani ya kumfundisha mwanao.. Jibu ni hapana.. Shule zinaajiri vijana wadogo wasio na uzoefu wala weledi wa Ualimu. Lengo ni wamiliki wa shule kupata Super profit..

Je.wewe mzazi unaona sawa mwanao afundishwe na mwalimu wa kuokoteza wakati wewe unalipa mamilioni.?? Jibu ni hapana. Wakaguzi, wazazi na idara ya kazi pitieni kwenye hizi shule mkajionee mauzauza
 
hapana. Wakaguzi, wazazi na idara ya kazi pitieni kwenye hizi shule mkajionee mauzauza

Wakaguzi na wizara ya kazi lazima waufyate. Shule zao wao zina stink to high heaven! Ofisi ya Rais Tamisemi, Captain Yusuph Makamba Secondary School Dar es Salaam, watoto wana division sufuri kama wote.
*
Wazazi nao hawana nguvu ya kulalamika. Private schools wanamiliki mitihani ya NECTA. Shule ya wasichana ya Masista, Mbeya, mwaka huu Form 4 wameandikwa Guiness Book of World Records. Watahiniwa wote shule nzima wana pointi saba. Utawaambia nini ?

Na hela wanapiga. St. Marian Boys and St. Marian Girls wamefanya intetview Bagamoyo. Wamekuja watoto 6,000. Mtihani buku 50. Jumla 300 Milion non refundable quick cash.

They dont give a flying fvck about what you say, and they can afford not to.
 
Wakaguzi na wizara ya kazi lazima waufyate. Shule zao wao zina stink to high heaven! Ofisi ya Rais Tamisemi, Captain Yusuph Makamba Secondary School Dar es Salaam, watoto wana division sufuri kama wote.

Wazazi, on the other hand, nao hawana nguvu ya kulalamika. Private schools wanatunga mitihani ya NECTA. Shule ya wasichana ya Masista Mbeya mwaka huu Form 4 wameandika Guiness World Record. Watahiniwa wote wa kituo cha mtihani wana pointi saba Utawaambia nini, hutaki mtoe mtoto wako.

Na hela wanapiga. St. Marian Boys and St. Marian Girls wamefanya intetview Bagamoyo. Wamekuja watoto 6,000. Mtihani buku 50. Jumla 300 Milion non refundable quick cash.

They dont give a flying fvck about what you say, and they can afford not to.
Wizi wa mtihani ndio umetawala huko. Inasikitisha sana
 
Shule za private zina classes. Zipo ambazo zinajitafuta na zipo zilizojipata. Kuna shule zinatafuta wanafunzi ili zimudu kulipa vizuri walimu, lakini pia kuna shule zinatafutwa na wanafunzi hadi zinawakataa kwa kufikia idadi waliyojipangia kulingana na miundombinu ya kuwaweka hapo.

Vivyo hivyo, kuna walimu wa private schools wanaoenjoy maisha ya ualimu na huko huko private school kuna walimu kama hao wanaozungumzwa katika uzi.
 
Hizo shule ni za kijinga sana! Ni wazazi tu ndio hawajui kinachofanyika wanadhani shule kuitwa english medium basi inatoa elimu kubwa. Wazazi wenyewe akili haziwatoshi kuchambua mambo ya elimu kwa kina pengine wao wenyewe wana elimu ndogo ya kawaida au hawafahamu kabisa misingi ya elimu. Ni kweli hizi shule zina tabia za kuokoteza walimu tena wasio na taaluma ya ualimu. Unakuta kijana ni form four failure au form six mchovu au aliyepitia chuo fulani hana ajira anaokotwa na kupangiwa kazi hiyo kiholela hata hakuna mkataba mradi tu ababaishe wanafunzi kwa kiingereza chake kibovu na chenye matege. Watoto wanaongea kiingereza kibaya cha walimu wao na wazazi wanaona vema tu kwa kuwa nao hawajui kabisa kinachoongelewa. Kuhusu mishahara ni ya hovyo isiyofuata scale za serikali. Mmiliki wa shule anaweza kutoa mabaki ya chenji zake akakupa hata elfu mbili na kukuambia zingine atamalizia kesho au uende dukani kwa mke wake ukapewe kilo ya sukari na unga mtakana mwisho wa mwezi. Mishahara yao ni laki au mbili
 
Salam kwenu.. Nije kwenye hoja.. Hawa walimu wanasikitisha.. Mishahara ni midogo sana.. 200,000/- mpaka 400,000/- kwa mwezi.

Kazi ni kuanzia saa 12 asubuhi mpaka saa 12 jioni. Jumatatu mpaka Jumamosi. Hakuna overtime wald posho.. Lakini wewe mzazi unalipa 2,000,000/- kwa mwaka..

Swali la kujiuliza ni Je huyo mwalimu anayemfundisha mwanao ana thamani ya kumfundisha mwanao.. Jibu ni hapana.. Shule zinaajiri vijana wadogo wasio na uzoefu wala weledi wa Ualimu. Lengo ni wamiliki wa shule kupata Super profit..

Je.wewe mzazi unaona sawa mwanao afundishwe na mwalimu wa kuokoteza wakati wewe unalipa mamilioni.?? Jibu ni hapana. Wakaguzi, wazazi na idara ya kazi pitieni kwenye hizi shule mkajionee mauzauza
Sema hata huko kwenye shule binafsi nako kumegawanyika. Zipo zinazolipa vizuri, na zipo hizo za wanyonyaji.

Mfano mdogo tu kuna shule moja maarufu ya binafsi huku Lushoto (inamilikiwa na Kanisa), hakuna mwalimu anayelipwa mshahara mbuzi kama huo. Nipo nao hapa hao walimu. Kuna wengine wanakunja milioni 2+ kila mwezi. Ukiwakuta wote wana vitambi!
 
Salam kwenu.. Nije kwenye hoja.. Hawa walimu wanasikitisha.. Mishahara ni midogo sana.. 200,000/- mpaka 400,000/- kwa mwezi.

Kazi ni kuanzia saa 12 asubuhi mpaka saa 12 jioni. Jumatatu mpaka Jumamosi. Hakuna overtime wald posho.. Lakini wewe mzazi unalipa 2,000,000/- kwa mwaka..

Swali la kujiuliza ni Je huyo mwalimu anayemfundisha mwanao ana thamani ya kumfundisha mwanao.. Jibu ni hapana.. Shule zinaajiri vijana wadogo wasio na uzoefu wala weledi wa Ualimu. Lengo ni wamiliki wa shule kupata Super profit..

Je.wewe mzazi unaona sawa mwanao afundishwe na mwalimu wa kuokoteza wakati wewe unalipa mamilioni.?? Jibu ni hapana. Wakaguzi, wazazi na idara ya kazi pitieni kwenye hizi shule mkajionee mauzauza
Nilichogundua ni walimu kukutumia wazaz kama vichwa. Yaani anakushawishi uwe unamlipa 30k au 50k kwa mwezi eti awe anamsaidia mwanao.

Yaani kuna shule ziko tabata ni upuuzi mtupu shule ukiangalia mhasibu ni shemeji wa mmiliki. Ni aibu anaifanya shule kama genge la nyanya.

Amepata wanafunzi wengi anaringa. Anadhani wazaz ni vipofu
 
Back
Top Bottom