Wasafiri tuwe makini na wanatudhulumu uhai wetu

fantastic philip

Senior Member
Oct 17, 2015
194
680
SOMO KWA WASAFIRI (PART 1)

1/Ili ni somo kwa ajili ya kusaidia mamlaka husika au wadau mbalimbali kutambua haki zao.

2/Leo tutaanza na somo la kampuni husika za mabasi kwenda na muda, hapa lazima tuweke sawa kuna tofauti kubwa kati ya kwenda na muda na kwenda mwendo kasi.

3/Kuna wimbi kubwa la vijana wengi tunaweza sema vijana ambao bado hawajajua maana ya maisha (hawana familia yoyote).

5/Vijana hawa wamekua mashabiki wa kushangilia mwendo kasi badala ya kwenda na muda mfano imekua ni jambo la kushangaza basi kisheria dar mpk mwanza ni masaa kuanzia 18+ ila basi nyingi zinatumia masaa 13.

6/Mabasi ya dar kwenda mwanza na dar kwenda kahama imekua ni kawaida kwa wao kuzipita basi za morogoro ambazo kikawaida sio sahihi maana umbali ni tofauti.

7/Kwenda na mda ni gari ifike ndani ya muda sahihi wa kisheria sio chini ya hapo.

8/Madereva na wao wamekua wakichangia ili jambo kwa kufuata maneno ya vikundi vichache vya watu ambao ni wapenzi wa mwendo kasi kumbuka dak 30 zinaweza kuleta janga la kitaifa.

JE ni sahihii umekufa ndio watu wanakutembeza spidi 50-80 wakati ulipokua hai ulitembezwa spidi 100+ ukakubali kudhulumiwa uhai wako

TUWE MAKINI MWENDO KASI UNAWEZA KUFUTA NDOTO ZETU VIJANA TUWAKEMEE VIKALI MADEREVA WOTE WENYE VITENDO HIVI...

Copy and paste

b3066b72-7c48-4b20-9a4a-67ed1d405210.jpg
 
Tatizo ni umasikini wetu unaosababisha watu ushabiki kwenye mabasi badala ya kwenye racing, rally and driffting cars. Watu wengi hawawezi kuaford kununua magari ya mashindano kwa hiyo wanaamua waweke ushabiki kwenye mabasi. Cha msingi watu wawekeze kwenye mchezo wa mbio za magari mbona haya mabasi mtaona yanatembea mwendo wa kobe.
 
Back
Top Bottom