KERO Mwendokasi Mbagala – Uhalisia wa Wananchi

KERO Mwendokasi Mbagala – Uhalisia wa Wananchi

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
🚍 KERO MWENDOKASI MBAGALA
1. Mfumo wa kupanda 🚫


Mwendo kasi za Mbagala hairuhusiwi kugeuza. Ukifika mwisho, lazima ushuke halafu upange mstari upya ili upate siti.
👉 Hii inalazimisha baadhi ya watu kulipa nauli mara mbili, hasa wazee na wenye changamoto za kusimama muda mrefu.

2. Nauli iko juu 💸
Nauli za mwendo kasi bado ni kubwa ukilinganisha na umbali wa safari.
👉 Tukizingatia mabasi yanatumia CNG na ni mradi wa serikali, wananchi wanategemea nafuu zaidi.

3. Kuondoa daladala = kuongeza kero ❗
Kuondoa daladala kumeongeza changamoto kwa wananchi:
👉 Nauli ya daladala ni nafuu zaidi
👉 Hakuna limit kubwa ya mizigo
👉 Mchana nauli hupungua
👉 Ilikuwa option mbadala muhimu kwa watu wengi

4. Usumbufu wa foleni Ilala 🚗
Mofat imeshindwa kudhibiti matumizi ya njia ya Ilala.
👉 Magari mengine yanaingia kwenye njia za mwendo kasi na kusababisha foleni kubwa, huduma inapoteza maana yake.

5. Express hazieleweki ❓
Express za Ilala Boma hazieleweki vituo vyake rasmi, tofauti na Kivukoni na Gerezani.
👉 Hii inaleta mkanganyiko kwa abiria, hasa wanaotoka Mbagala kwenda Ilala.

🔥 HITIMISHO

Mwendo kasi ni mradi mzuri, lakini bado kuna changamoto zinazohitaji maboresho ili kuwahudumia wananchi kwa haki na ufanisi.
 
Duh hii nchi ina walalamishi balaa!
1. Kwahio mnataka kupanda na kugeuza na bus lakini mlipe nauli moja?
2. Bus jipya,full AC,dakika chache umefika ila mnataka nauli iwe kama daladala?
3. You can't eat your cake and have it. Aidha ni daldala au mwendokasi.
4. Kudhibiti matumizi ya hizo njia sio kazi ya Mofat.
5.....

Labda namba tano ifanyiwe kazi ila hayo mengine ni nong nongwa tu.
 
Back
Top Bottom