WASAFIRI: Barabara ya Kibiti Lindi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

WASAFIRI: Barabara ya Kibiti Lindi

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by nachid, Dec 26, 2011.

 1. nachid

  nachid JF-Expert Member

  #1
  Dec 26, 2011
  Joined: Apr 14, 2011
  Messages: 898
  Likes Received: 50
  Trophy Points: 45
  Barabara mbovu kuliko maelezo kuanzia maeneo ya Nyamwage baada ya kuvuka daraja la Mkapa, ina mashimo ya ajabu kama una wazo la kusafiri na gari dogo e.g opa, noah etc ondoa ilo wazo otherwise utaua gari yako
   
 2. Msolopagazi

  Msolopagazi JF-Expert Member

  #2
  Dec 26, 2011
  Joined: Nov 26, 2010
  Messages: 659
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 45
  Mmmh si kuna ka msemo ka Magufuli Mtwara mpaka Mwanza kwa bajaj imewezekana
   
 3. matumbo

  matumbo JF-Expert Member

  #3
  Dec 26, 2011
  Joined: Jul 9, 2011
  Messages: 7,199
  Likes Received: 85
  Trophy Points: 145
  Ivi kile kipande bado akijaisha hadi leo??..sitopasahau pale nililala njiani bila kupenda nikienda Liwale.
   
 4. nachid

  nachid JF-Expert Member

  #4
  Dec 26, 2011
  Joined: Apr 14, 2011
  Messages: 898
  Likes Received: 50
  Trophy Points: 45
  basi lenyewe linapita kwa taabu then bajaji upite wapi?
   
 5. nachid

  nachid JF-Expert Member

  #5
  Dec 26, 2011
  Joined: Apr 14, 2011
  Messages: 898
  Likes Received: 50
  Trophy Points: 45
  bado hapajaisha tena sijui wanaendelea na kazi au wameacha coz wao na vifaa vyao wamepaki tu, na kipande cha mchina wametoa ile lami isiyo na kiwango wanaweka nyingine
   
 6. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #6
  Dec 26, 2011
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  Serikali imeshindwa kulipa makandarasi, vifaa kukaa site bure bila kazi serikali huvilipia kwa kila saa moja fedha nyingi tu.
   
 7. nachid

  nachid JF-Expert Member

  #7
  Dec 26, 2011
  Joined: Apr 14, 2011
  Messages: 898
  Likes Received: 50
  Trophy Points: 45
  si waendelee kukopa kazi iishe
   
 8. Bitabo

  Bitabo JF-Expert Member

  #8
  Dec 26, 2011
  Joined: Sep 27, 2011
  Messages: 1,896
  Likes Received: 124
  Trophy Points: 160
  Mh jamani mi ni mkazi wa kusini. Kuna issue mbili hapa.
  1. Ndundu Somanga na Nyamwage. ni zile 60 km za zamani. Unajua mwanzoni ilitakiwa ichangiwe na serikali yetu na ile ya kuwait but Kuwait walijitoa japo sababu siijui. Now inajengwa kwa pesa za Tanganyika ( oh sorry Tanzania)
  Kuna kipindi serikali yetu ilikuwa inadaiwa karibu bil. 3 na mkandarasi na kazi ikabidi isimame but few months back wameanza kazi na kuna kipande almost 20-30km kimeshapigwa lami na kimefunguliwa japo si chote. sehemu iliyobaki nilimsikai magufuli anasema ameshawalipa almost 2 bil na kweli wamerudi site. tatizo la pale mvua kubwa zikianza kama sasa, kazi inabidi isimame maana kuna maji si mchezo japo sijui kitaalam ni kwa nini inasimama but nilipita like 2wks walikuwa wanaendelea na kazi ya backfilling ili kuweka level sawa na madaraja then kazi nyingine ziendelee. I hope mvua zikipungua kazi itaendelea.
  2. Ni ile Nangurukuru to Mbwemkuru ya wachina. hii ilikataliwa na JK baada ya ujenzi kumalizika na kukosa viwango. Sasa jamaa wanatindua lami yote na kuanza upya. eneo hili lina udongo wa mfinyanzi linateleza balaa. Uzuri ni kwamba kila siku wanakuwa site labda kipindi hiki cha sikukuu ndo sijui. kama wapo wanajitahidi kusaidia magari yapite hata kama mvua inanyesha sana.
  Lets hope for the best lakini kama unasafiri nyakati hizi bora ubebe mikate ya kutosha na kama mko wengi basi bebeni mchele na maharage ya kutosha na jiko la mchina maana kulala njiani nji kawaida sana ila kuna mbu balaa.
  Cha ajabu kama kuna mabasi yamelala humo asubuhi utakuta used condoms kibao, sijui hizi show huwa zinafanyikia kwenye tope???
  Kaazi kweli kweli
   
 9. nachid

  nachid JF-Expert Member

  #9
  Dec 27, 2011
  Joined: Apr 14, 2011
  Messages: 898
  Likes Received: 50
  Trophy Points: 45
  Asante kwa taarifa mkuu
   
 10. trachomatis

  trachomatis JF-Expert Member

  #10
  Dec 27, 2011
  Joined: Jun 7, 2011
  Messages: 3,653
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 145
  mengine inabidi mshuke mkanyage tope! gari lipunguze uzito lipite mkalikute mbele!
   
 11. trachomatis

  trachomatis JF-Expert Member

  #11
  Dec 27, 2011
  Joined: Jun 7, 2011
  Messages: 3,653
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 145
  Wajua watu hawaamini kama Mtwara-Dar ni hardly kilometa 560! Ni kipande korofi tu hicho chenye matatizo tena wakati wa mvua. Kipande hicho km 60[wastani wa Dar-B'moyo] unatumia masaa mawili mpaka mawili na nusu barabarani,ila wakati wa mvua,hata masaa manne na zaidi! Gari binafsi inabidi iwe na 4wheel kwa kipindi hiki!
   
Loading...