Wasafi TV kuanguka kabla ya kuanza

Wasafi TV kuanguka kabla ya kuanza

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Posts
142,528
Reaction score
287,064
index.jpeg

Kitendo cha Diamond Platnumz kufahamika kwa Umma kuwa ana mahusiano ya Karibu na Makonda kimetafsiriwa na wataalam wa mambo ya biashara kama anguko la kituo kipya cha Tv kinachotarajiwa kuanza hivi karibuni kiitwacho Wasafi.

Ikumbukwe kwamba Makonda ndio mtu anayeshika nafasi ya pili kwa kuchukiwa na wananchi wa Tanzania, sasa kushirikiana na mtu wa namna hii katika jambo lolote ni sawa na kutumbukiza jambo lenyewe kwenye moto wa milele.

Bado haijafahamika kisa wala malengo halisi ya urafiki huu wa ghafla, bali kinachofahamika ni kwamba Makonda hawezi kuisaidia chochote Wasafi kwa vile kabla hata ya yeye kuingia DSM Wasafi ilishakuwa maarufu kutokana na kukubalika na watu wote masikini ambao umasikini wao umeletwa na chama ambacho Makonda anakitumikia miaka lukuki.
 
Makonda anashika nafasi ya pili ...kwa kuchukiwa ...ina maana wa kwanza ...ni Jiwe ...Yaani wasafi Tv Aiwezi kuanguka ..kwasababu Mtaji wanao ...maana mashabiki wa mond watamsaport kiana.
Washabiki wa Mondi ndio waliotuletea masikitiko yao baada ya kustukia uhusiano wa Makonda na Mondi
 
Waswahili tunapenda sana kuona biashara za watu waliofanikiwa zikuanguka.
Hiyo ni roho mbaya ya ushetani.
Hatufanikiwi sababu ya husuda Na roho ya chuki
wakati mwingine waswahili tunajichanganya wenyewe kutokana na kukosa maarifa , sina chuki na mondi bali nimeweka maono yangu baada ya kusikia manung'uniko.
 
Ikumbukwe kwamba Makonda ndio Mtu anayeshika nafasi ya pili kwa kuchukiwa na wananchi wa Tanzania

Ume exaggerate, Mikoa mingine haina haina sababu ya kumchukia mchapa kazi, mpenda haki, mtatua kero, mcha Mungu...

Labda tuwachukie wauza unga, matapeli wa viwanja, wanaume wasiowajali wake na watoto wao, wale wauza magari kama karanga mjini, wapenda kupiga miziki usiku kucha na kuwa kero kwetu tunaotaka kulala, wanyima haki kwenye mirathi na wauza nyumba za watu kitapeli...

Honestly, yupi ambaye anapiga kazi? Makonda au Mdee? au Mnyika? au Waitara?!!!!
Tatizo hapa ni dogo sana, kushindwa hoja na itikadi, kutafuta KIKI kwa raia kwa kuvunja sheria na taratibu kwa makusudi ili vyama pinzani vipate "political symphathy"! Its pathetic...
 
Erythrocyte

Wewe ulisikia hasira zako kwa mkuu wa mkoa basi watu wote wanachuki nae

Kila biashara na marketing strategy yake, Lazima utaste Idea zako kwanza kwenye biashara yeye na idea zake

Mbona wenzako waligoma kumuandika kwenye magazeti leo neno Paul wanaandika.

Elimu elimu elimu
 
Erythrocyte
Kuchukiwa. Are you serious. We unawajua Watanzania kweli. Au huku mnavyojihamasisha kupinga hata swala La kibaologia la kunya. Wewe Sema unamchukia na sijui kwa lipi. Mana chuki kwa mtu na akili zake. Zinamla Ndani mbaya zaidi jamaa hta hakujui. Akiita Watu wanaenda.

Kutibiwa mpka mkeo alienda. Hakukwambia .wodi ile ya kina mama wanatibiwa. We umefanya nini Watu wakupende. Wasome Wtz kwanza Bwana maarufu wa JF. Makonda mtu maarufu na hata Leo akigombea ubunge na Lema wako. Anamtoa Kout kabisa. Kuna mgonjwa yupo China. Iwe kwa kuiba kwa kula. Anafanya kitu. Ukiwa mjinga jaribu kuficha kwa kukaa kimya. Acha KUWA MGANGA WA KIENYEJI.
 
Waswahili tunapenda sana kuona biashara za watu waliofanikiwa zikuanguka.
Hiyo ni roho mbaya ya ushetani.
Hatufanikiwi sababu ya husuda Na roho ya chuki
Kuna watu wanaroho mbaya lakini nimatajiri ...kuwa tajiri na roho mbaya avina uhusiano.
 
Je kosa lake ni kuwa na urafiki makonda? Ninavyojua hii ni siasa na siasa haina rafiki wala adui wa kudumu. Kipindi cha uchaguzi asilimia kubwa ya wasanii walishiriki kwenye kampeni za ccm. Watu wengi walisema wanajiharibia kutokana na kujihusisha na hiki chama. Lakini mpaka leo naona wanaendelea kung'ara.
Huwezi jua chibu anafaidika vipi na huo urafiki wao
 
Back
Top Bottom