Wasabato ujumbe wenu huu hapa

Status
Not open for further replies.

Akili yako,mwili na damu haviwezi kukufunulia mambo hayo;kwani mambo ya rohoni hutambulika kwa jinsi ya rohoni pia!
 
nimekuelewa kiasi kwa uliloandika, ukipata wasaa jibu swali zima, likiwa na nyongeza ya dodoso uliyotoa litakaloonyesha kwa nini Yesu hakufanya ubatizo wa japo kundi dogo, japo alitabiriwa kwamba atabatiza.

Yesu hakutabiriwa kubatiza watu kwa maji. Kumbuka huyu ni Mungu aliyefanyika mwanadamu ili aje kufanya kazi ya kumfia mwenye dhambi. Maelezo ya Yesu na Uungu vimeelezwa vizuri katika Yohana 1:1-18.

Soma Mathayo 3:11-12
Yohana mbatizaji hasemi kwamba Yesu atabatiza watu kwa maji, bali kwa ROHO MTAKATIFU NA MOTO. Hapa anamaanisha kwamba yeye Yohana anawabatiza kwa maji ikiwa ni ishara ya toba kwa dhambi zao na hana uwezo wa kuwapatia nguvu yoyote kama vile yule ajaye(YESU) ambaye ana uwezo mkubwa na ndiye mwenye kutoa Hukumu. Kumbuka wakati Yesu akipaa zake mbinguni aliwaahidi wanafunzi wake kuwapatia Roho Mtakatifu ambaye aliwaongoza na anaendelea kutuongoza hadi leo(pale unapojisalimisha kwake). Kwa hiyo katika habari alizozisema Yohana kumebaki habari ya Moto ambayo hii itakuwa ni hatua ya mwisho katika kuteketeza wale wote watakaoonekana makapi (soma fungu la 12)
 
Oh kumbe pasaka papa alijitungia tu.... hatari kabisa hii.
 
Mkuu uko uliko-bold unaweza nipa maana yake.
 
Niseme tu kwamba siwezi kubishana na msabato kwa sababu yeye yuko tayari kufanya urafiki hata na muislamu ili kumpinga mkristo wa dhehebu tofauti na sabato. Tunapotoshwa kwa sababu tunasubiri watu watusomee na kututafsria biblia, wakati sisi wenyewe uwezo huo tunao! Kimsingi na kibiblia Yesu ametuagiza kwamba, tunapaswa kumwomba bila kukoma, kwa maneno mengine, kila siku unapaswa kuwa na muda wa kusogeza mahitaji yako kwa Mungu. Yani ya Kiroho na Kimwili.
 

huwa tunaongoka maana kuoka hadi ajapo yesu
 
Oh kumbe pasaka papa alijitungia tu.... hatari kabisa hii.

Huo mwili na damu upoje tufafanulie basi yani huko kanisani mnakunywa na kula mwili wa bwana au neno lake ndo mnaita mwili na damu?
 

Ok, Kwa hiyo wasabato ni wafarisayo au wasadukayo? Alafu naomba unisaidie mistari inayoelezea kuwa Yesu alienda kusali kwenye Sinagogi nataka niisome zaidi.
 
Ntuzu mbona hamtoi majibu humu au maswali magumu?



Mkuu nilikua nilikua na pilika Kidogo!

Naona kuna hoja nyingi sn mnazungumza!

Ebu Naomba uniulize hayo Maswali nione nitakavyoweza kukujibu Ingawa niko njiani!
 
Mkuu kabla sijaingia kwenye kukujibu hoja yako kwa kirefu naomba unijibu hili swali

Kabla ya Yesu kuja duniani Torati ilikuwa imehubiriwa sehemu nyingine za Dunia tofauti na Israel?



Mkuu dhumuni la neno la Mungu lilikua ni kuhubiriwa Ktk ulimwengu wote!

Lkn kwa Waisrael walipokea neno vibaya Ike habari wakaikumbatia wao tu! Na ndio Maana Yesu alipokuja aliweza kuhubiri mpk kwa Watu Wa mataifa na waliotengwa! Mfano Wa mwanamke msamaria unafaa kuonesha ni jinsi gani Yesu alivunja matabaka kwa kuwapa Watu Wa mataifa habari njema!
 
Ok, Kwa hiyo wasabato ni wafarisayo au wasadukayo? Alafu naomba unisaidie mistari inayoelezea kuwa Yesu alienda kusali kwenye Sinagogi nataka niisome zaidi.


Mkuu kwanza nikuulize nini Maana ya Farisayo?
 


Yesu anasema ukinipenda utazishika sheria zangu! Na ndani ya hizo sheria imo sabato!

Sheria za Mungu zimezungumzwa Ktk agano la kale na Yesu mwenyew na pia Ktk kitabu cha ufunuo!

Sasa Wewe unapo sema sabato ni dini ya kishetani kwa kigezo gani Mkuu? Na ukumbuke Kua Yesu mwenyewe alikua akitunza sabato!
 
Mkuu nilikua nilikua na pilika Kidogo!

Naona kuna hoja nyingi sn mnazungumza!

Ebu Naomba uniulize hayo Maswali nione nitakavyoweza kukujibu Ingawa niko njiani!
Maswali yangu ilikuwa kuhusu pasaka,embu tueleze wasabato na kufa na kufufuka kwa Yesu,ni kwa nini hamsherekeagi Pasaka,pili ni kwa nini hamtumiagi vinywaji venye gesi?,Yesu aliposema kimwingiacho mtu hakimtii unajisi bali kitokacho kinywani alimaanisha nini?,sorry kwa kutoka nje ya mada(binafsi kunena kwa lugha sikuafiki).
 
Kuhusu sabato tusome kutoka12;16, Matendo 20;7 Mungu aliagiza kupumzika siku ya kwanza juma na siku ya saba ya juma ambazo ni jumapili na jumamosi. Na Paulo alimega mkate na kuhutubu siku ya kwanza ya juma, maana yake walifanya ibada siku ya jumapili. Kuthibitisha siku ya kwanza ya juma soma Marko16;1-2 baada ya sabato kupita siku ya kwanza ya juma ndiyo siku aliyofufuka Yesu Kristu. Sasa wasabato wana ushirika na yule mpinga Kristu? Kwa sababu wanadai tunaoabudu j'pili tunabadili majira na nyakati,tena wakrisu wenzao wakati Mungu ameagiza kupumzika j'mosi na j'pili,na mitume waliabudu j'pili inakuwaje wakati kuna jamii ambayo haiabudu j'pili wala j'mosi hawaisemi ila wakristu wenzao wanaofuata maandiko? Tunajua shetani adui yake mkubwa ni kanisa je ameshapata sehemu ya kushambulia kanisa? Wasabato mnanitisha
 

Mkuu usinielewe vibaya! Bado uko na Maswali mengine?

Umezungumza kusheherekea kufa na kufufuka kwa Yesu hapo una Maana gani Mkuu? Yani kile Kitendo cha Yesu kufa na kufufuka ndio Maana ya sherehe ya pasaka?
Nikuombe ufafanuzi Kidogo kabla sijaanza kujibu!
 
Kama Yesu alituza Sabato mbona aliponya na hata kukemea wakuu wa sunagogi waliomkaripia(lk13:10-17)..
 
Status
Not open for further replies.

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…