Wasabato msituchangishe kama hamtaki bia

Wasabato msituchangishe kama hamtaki bia

Acha uongo Mkuu! Mara ya ngapi Leo unazungumza uongo juu ya mama White?

Mkuu kuna kitabu nasoma hapa kinaitwa The Four Cult.......Kimeandikwa na Pastor aliye toka SDA na kuwa Baptist Minister huko USA.... Anaelezea the kwa ufasaha "The Great Dis-appointment"........
 
Kitabu kinataja the four Cult kuwa ni

Jehova Witness

Mormon

Seventh Day Adventist

Christian Scientist
 
Mkuu kuna kitabu nasoma hapa kinaitwa The Four Cult.......Kimeandikwa na Pastor aliye toka SDA na kuwa Baptist Minister huko USA.... Anaelezea the kwa ufasaha "The Great Dis-appointment"........

Bado hujanijibu!
 
Hakuna mtu anaetoa mchango apate huduma mbovu,mchango uendane na huduma,hizi kamati zinakuwaga na siri sana...
 
JEKI uko wapi? Mimi msabato niko hapa nakusikiliazia!

Au nianze kukupa neno ufahamu Maana ya kutoa? Au nikufahamishe kwamba mwili wako Ni hekalu la Bwana hivyo hutakiwi kuutia unajisi Wa ulevi etc? Maana Mungu hukaa ndani yetu! Sasa Km unalitia unajisi hekalu la Bwana, bila Shaka Mungu hawezi kukaa ndani yako!

Nakusubiri Mkuu kwa hoja Zaidi!
Ntuzu sasa wewe unahusikaje, si uniache nitakuja kuhukumiwa mimi? kwa mtindo huu sitashangaa siku moja mkavamia bar na kuzuia watu kunywa bia, isitoshe ni chakula gani utakula kisichoharibu hekalu la bwana? harusini tunakula kuku wa wiki 6, au hao hawaharibu hekalu la bwana?
 
Last edited by a moderator:
Harusi za kisabato zimekuwa za kero kubwa, wanasema hawataki kuweka vinywaji vyenye alcohol kisa imani yao, hawajui kama hayo mambo yanzuiwa kanisani tu, mkitoka kanisani huku kwingine ukumbini ni kwa Kaisali lazima watuachie ya Kaisali na ya Mungu tunakuwa tushayamaliza kanisani, kinachoudhi zaidi wanachukua michango yetu halafu wanatuchagulia cha kutumia, ile michango siyo hela yao, nakuwa nimetoam mimi na wala hoja ya kusema wananua wao si sahihi.

Kama wanasimama kwenye imani yao basi wasichangishe pesa zetu bali watumie zao na sisi tutakuja kunywa soda na juice kama wanavyotaka na siyo mchango wangu wa pesa waupangie cha kuninunulia.

Wewe ni Pimbi,kwani walikulazimisha kuchangia??
 
Kwani mkuu anayeoa anakuwa wa imani hiyo au wanakuja kwenye harusi yako wanaleta imani zao?
Na hapa ifahamike kuwa kuchangia harusi,haimaanishi wewe kwenda kula na kunywa,ni zaidi ya hapo
ni ishara ya kuunga mkono kile anachoenda kufanya huyo unayemchangia iwe umehudhuria au hukuhudhuria,sasa kama issue ni kunywa
watu wana uwezo wa kunywa hata nje ya kumbi za harusi,kwanini usubiri harusi ya mtu ndo unywe au ndo yale ya kutokula matunda mpaka uandikiwe na daktari?
 
sasa hela tunazochanga zinafanya kazi gani kama sisi wachangiaji hatufurahii?
 
sasa hela tunazochanga zinafanya kazi gani kama sisi wachangiaji hatufurahii?
Hii tabia ikiendekezwa tutafika mahali tutamwomba bwana arusi atupe bibie alale kwetu coz tumemchangia,
nadhani ni wakati muafaka wa kumchangia mtu ili aoe hata asipofanya sherehe poa,coz tunakuwa tunaunga mkono na kufanikisha aoe
Tuondoe ile dhana ya nipe nikupe.
 
Ntuzu sasa wewe unahusikaje, si uniache nitakuja kuhukumiwa mimi? kwa mtindo huu sitashangaa siku moja mkavamia bar na kuzuia watu kunywa bia, isitoshe ni chakula gani utakula kisichoharibu hekalu la bwana? harusini tunakula kuku wa wiki 6, au hao hawaharibu hekalu la bwana?

Usianze kupiga kelele hapa! Kwani ulileta hoja hapa kwa mazumuni gani? Lengo lako Si lilikua kila mmoja kutoa moan yake na Wewe kutoa dukuduku lako? Au sio?

Kwa msabato anaelewa lishe hawezi kula hizo Kuku zako! Na pia Kuku sio haramu!

Sasa tafuta hoja ingine!
 
Last edited by a moderator:

Similar Discussions

Back
Top Bottom