Mwanamutapa
JF-Expert Member
- Dec 5, 2011
- 513
- 489
Harusi za kisabato zimekuwa za kero kubwa, wanasema hawataki kuweka vinywaji vyenye alcohol kisa imani yao, hawajui kama hayo mambo yanzuiwa kanisani tu, mkitoka kanisani huku kwingine ukumbini ni kwa Kaisali lazima watuachie ya Kaisali na ya Mungu tunakuwa tushayamaliza kanisani, kinachoudhi zaidi wanachukua michango yetu halafu wanatuchagulia cha kutumia, ile michango siyo hela yao, nakuwa nimetoam mimi na wala hoja ya kusema wananua wao si sahihi.
Kama wanasimama kwenye imani yao basi wasichangishe pesa zetu bali watumie zao na sisi tutakuja kunywa soda na juice kama wanavyotaka na siyo mchango wangu wa pesa waupangie cha kuninunulia.
Kwani unalazimishwa kuhuzuria harusi zao? Tafuta zako zisizo na pombe na sio pombe tu wasabato pia hawavuti sigara na wala hawali nguruwe kama walivyo waisalamu in matter of fact hawali mnyama yeyote asiye na kwato kama mbwa, sungura nk na wala ambaye hacheui kama nguruwe ambaye ana kwato lakini hacheui, sungura na ngamia hanacheua lakini hawana kwato mnyama anatakiwa kuwa na vyote awe na kwato na pia anacheua mfano wa mbuzi, kondoo na ng'ombe. hii ni kwa mujibu wa imani yao soma zaidi (Mambo ya Walawi 11:1-47 & Kumbukumbu ya torati14:1-29)
Na si wao tu pia kwenye harusi za kiisilamu hakuna nguruwe wala pombe sawa na wasabato
Ni imai yao zaiwa