Wasabato matengenezo

Status
Not open for further replies.
sda pasta.shetan alitupw akaend ktk mifumo yote y galaxy kueneza chuki,mifumo mengne walimkataa,mfumo hu wetu walimkubal
 
Kwa uelewa wangu kidogo Mashahidi wa yehova limeanza nyuma ya SDA na mwanzilishi inasemekana alitokea SDA.

Mbona sijakuelewa,lilianza nyuma unamaana kabla yakuanzishwa kwa SDA sasa iweje tena kiongoz atoke SDA????
 

Jibu la swali lako ni refu kidogo, labda kama upo fb kuna group niliyoanzisha kwa ajili ya kujifunza mambo ya Mungu na hata hii nimeeleza ila kwa urefu wake hadi naona uvivu hata ku ileta hapa. Group yenyewe inaitwa Hakuna Jipya Duniani.
 
Ukirejea nilichoandika utagundua nilikuwa naongelea 'DIBAJI' kama ilivyoandikwa na wadhamini wa White.Katika utangulizi kama kweli waliona ubaya wa MAUMAU waliwezaje kutoona ubaya wa ukoloni?

Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums


Sasa ndio umerekebisha! Lkn mwanzo Ulitaka kutuaminisha moja kwa Moja Kua hicho kitabu kiki Na shida! Na mpk ukafikia kusema Kua hakuna cha wasabato, Sijui na dhehebu gani ukataja Hapo!

Ata Yesu aliona umuhimu Wa Kua Na dhebu Au Kua ktk Kundi Moja km tunavyoona ktk Yohana 10:16
 
Jibu la swali lako ni refu kidogo, labda kama upo fb kuna group niliyoanzisha kwa ajili ya kujifunza mambo ya Mungu na hata hii nimeeleza ila kwa urefu wake hadi naona uvivu hata ku ileta hapa. Group yenyewe inaitwa Hakuna Jipya Duniani.

nitafikiria kujiunga fb.
Salaam.
 

Ok Mkuu! Ngoja kidogo nitoe maelezo katika hili!

Kuna matukio ktk ujio Wa Yesu mara ya pili!

Tukio la kwanza ni kwa Yesu kuja mawinguni

Tukio la pili ni watakatifu watafufuliwa kwanza km ulivyo Pewa Mafungu Hapo nyuma

Tukio la Tatu ni wadhambi watakufa ambao watakutwa Duniani wakiwa hai

Na Tukio la nne Shetani atafungwa miaka 1000.

Ngoja Nikifika home ntakuwekea Mafungu vzr!
 
nitafikiria kujiunga fb.
Salaam.

Hata usihangaike kama haupo fb, waweza nitumia email address yako kwa kuni PM, then nitakutumia hizo doc kwenye email.yako.
 

nashukuru kwa mwongozo, nitafurahia zaidi utakapoweka mafungu vizuri ufikapo nyumbani. Hili ni moja ya vitu vyenye mtiliriko unaonisumbua.
 
Jibu la swali lako ni refu kidogo, labda kama upo fb kuna group niliyoanzisha kwa ajili ya kujifunza mambo ya Mungu na hata hii nimeeleza ila kwa urefu wake hadi naona uvivu hata ku ileta hapa. Group yenyewe inaitwa Hakuna Jipya Duniani.
Wakristo wote siku ya kuabudu ni jumapili sasa nyie hii jumamosi yenu mlitoa wapi?
 
Kitu kingine ndugu pleo, kuna fungu Yesu aliongelea kuja kwake kwa kufananisha na siku za Lutu(rejea Luka 17 kuanzia mstari wa 28 na kuendelea). Na hapo ndipo kuna siri nyingi sana ambazo watu hawazielewi vizuri. Ingawa nimezieleza vizuri katika doc hizo ambazo kama utanitumia email nitakutumia, si vibaya nikiandika kwa uchache mambo kadhaa katika habari za Lutu.
Mambo hayo ni kama ifuatavyo.
1. Kabla ya Sodoma kuchomwa, malaika watatu walipelekwa ili kuchunguza na kutoa tahadhari(rejea Mwanzo sura ya 18 na 19). Kabla ya kuja duniani kwa Yesu mara ya pili, jumbe tatu za malaika watatu zitasikika duniani(rejea Ufunuo 14:6-11). Na ndio maana wa SDA wakati mwingine tunajiita watangaza jumbe hizo tatu maana tunawaonya watu kuhusu Hukumu, babeli na alama ya mnyama.
2. Wakati wa Lutu, moto uliteketeza na hakikusalia kitu, ni vivyo kwa dunia yetu hii.
 
Last edited by a moderator:
pleo then ktk Hiyo miaka 1000 hao Watu Wa Mungu Yani watakatifu Wa mbinguni Dunia itabaki ukiwa na utupu! Na Shetani atabaki akiwa kafungwa! Na kamwe kutakua hakuna binadamu anaishi ktk USO Wa Dunia ktk Hiyo miaka 1000.


Then kuna Tukio jingine baada ya Hiyo miaka 1000.

Mji Wa Jerusalem utashuka: ufunuo 21:2

Then wazambi watafufuliwa na Shetani atafunguliwa ufunuo 20:7,8

Then dhambi na wadhambi wataangamizwa!

Na Dunia itafanywa upya!!!
 
Last edited by a moderator:
Wakristo wote siku ya kuabudu ni jumapili sasa nyie hii jumamosi yenu mlitoa wapi?

Unaniuliza mimi au mimi ndio natakiwa nikuulize kuhusu ibada ya siku ya kwanza ya juma ilianza lini. Siku ya saba ilianzishwa katika siku ya saba baaada ya uumbaji. wakati siku ya kwanza ya juma(jumapili) imeanza kuabudiwa rasmi miaka ya 300s baada ya kristo.
 
nashukuru kwa mwongozo, nitafurahia zaidi utakapoweka mafungu vizuri ufikapo nyumbani. Hili ni moja ya vitu vyenye mtiliriko unaonisumbua.


Ok Mkuu Ngoja Nikifika ntajitahidi kukupa! Lkn mtiririko Wa matukio hayo ni km nilivyo eleza Hapo!
 

.
Yesu hakuwa na dhehebu wala hapajawahi kuwa na nabii aliyetokana wala kuanzisha dhehebu lolote. Kulikuwepo na madhehebu ya mafarisayo, mazadukayo, Zeelote, othodox, Rc, angelikana, Lutheran na sasa haya ya kipentekoste yaliyo mlengi kama utitiri hakuna nabii aiyewahi kuwa wa lolote katika hayo. Au kama kuna mwenye ushahidi wa nabii yeyote wa kibiblia kuanzia Nuhu, Abraham, Daudi, Yeremia, Ezekieli, Isaya, Daniel, Malaki, Yohana, Petro , Paulo ama Bwana Yesu kuwa mwanachama wa mojawapo ya hayo, atupe. Na ni lipi kati ya yote?
.


.
 
anyway nimeona nitupie hapa hapa kwa ajili ya watu wote. Nitaandika kwa sehemu tatu kuchambua fungu la Luka 17:28-32.

SEHEMU YA KWANZA
Mji wa Sodoma ni mji miongoni mwa miji ambayo
katika nyakati za Lutu iliteketezwa kwa moto, na
katika kipindi cha Yesu Kristo hapa ulimwenguni,
alipokuwa akieleza kuhusus ujio wake mara ya
pili, baadhi ya matukio aliyoyatabiri kutukia kabla
ya kurudi kwake ni lile alilosema 28.Ndivyo
ilivyokuwa katika siku za Lutu: Watu walikuwa
wakila na kuinywa, wakinunua na kuuza,
wakilima na kujenga. 29Lakini siku ile Lutu
alipoondoka Sodoma, ikanyesha mvua ya moto
na kiberiti kutoka mbinguni ukawaangamiza
wote. 30‘‘Hivyo ndivyo itakavyokuwa siku ile
Mwana wa Adamu atakapofunuliwa. 31Siku hiyo,
mtu ye yote aliyeko kwenye dari ya nyumba yake,
vitu vyake vikiwa ndani ya hiyo nyumba asishuke
kuvichukua. Vivyo hivyo mtu aliyeko shambani
asirudi nyumbani kuchukua cho chote.
32Mkumbukeni mke wa Lutu!
( Luka 17:28-32).
Kabla ya kuangalia Sodoma na dunia ya leo
tuangalie kwa uchache kuhusu Sodoma ya zamani
katika mambo yafuatayo.
1. MAHALI NA MAANA
Sodoma ni miongoni mwa miji mitano iliyokuwa
katika bonde la Yordani(Mwanzo 13:10, mwanzo
14:2-3, Kumb 34:4).
Bonde hilo lilikuwa na maji ya kutosha na
hivyo kuwa na malisho ya kutosha ya mifugo
ambayo ilimvutia Lutu, pia inafananishwa na
bustani ya Mungu. Tunasoma haya katika Ezekieli
16:46 46Dada yako mkubwa alikuwa Samaria,
aliyeishi upande wako wa kaskazini na binti
zake, pamoja na dada yake, naye dada yako
mdogo, aliyeishi kusini yako pamoja na binti
zake, alikuwa Sodoma
.
Hakuna maana halisi kwa majina ya
Sodoma na Gomora, lakini kutokana na Lugha za
awali, Sodoma yaweza kuwa ni jina la neno
lililotokana na Lugha za Kisemiti hasa
likihusianishwaa na neno la Kiarabu SADAMA
limaanishalo fasten, fortify, strengthen. Nayo
Gomora yaweza kuwa ilitokana na mzizi GH M R
imaanishayo be deep, copious(water).
2. MAASI YALIYOKUWA
YANATENDWA SODOMA

i. Watu wa Sodoma walitenda
uhalifu wa kiuchumi, makufuru na umwagaji wa
damu. Mfano, walikopesha mali kwa mwombaji
kwa kumpatia ingots na kuandika majina yao pale,
lakini walikataa kumuuzia chakula na mwisho mtu
Yule alikonda kwa kukosa chakula na mwisho
kufa, baada ya kifo chake, walidai kurudishiwa
mali zao.
ii. Mafundisho ya kirabi ndani ya
Mishnah(sharia za kiyahudi) inaelezwa kuwa
dhambi ya Sodoma na Gomora ilikuwa kwa
upande wa mali, wasodoma waliamini kuwa
”changu ni changu, na chako ni chako” ambayo
inaelezwa kama ukosefu wa huruma.
iii. Utamaduni mwingine wa kirabi
unaonyesha kuwa miji hiyo miwili ambayo ilikuwa
ni miji tajiri iliwatendea wageni katika mtindo wa
sadistic(great physical or mental cruelty). Hii
ilikuwa ni stori kuhusu kitanda ambacho wageni
walilazimishwa kukitumia. Kitanda hiki kilitumika
kwa uzinzi, uwe unataka, ama hutaki, watu wa
Sodoma wangekulazimisha kukilalia kitanda hicho.
Na kama ulikuwa mfupi kuliko kitanda,
wangekifungua kitanda kile na kuweka urefu wako,
na kama ni mrefu zaidi, kingeongezewa urefu ili
mradi tu uenee pale.
Tunasoma haya ndani ya Biblia takatifu ‘’ 49“
‘Sasa hii ilikuwa ndiyo dhambi ya dada yako
Sodoma: Yeye na binti zake walikuwa na
majivuno, walafi na wazembe, hawakuwasaidia
maskini na wahitaji. 50Walijivuna na kufanya
mambo ya machukizo sana mbele zangu. Kwa
hiyo niliwakatilia mbali nami kama mlivyoona.
Pia walikuwa wanafanya ushoga katika warumi
1:26-27 tunasoma 26Kwa sababu hii, Mungu
aliwaacha wavunjiane heshima kwa kufuata
tamaa zao za aibu. Hata wanawake wao
wakabadili matumizi ya asili ya miili yao
wakaitumia isivyokusudiwa. 27Vivyo hivyo
wanaume pia wakiacha matumizi ya asili ya
wanawake wakawakiana tamaa wao kwa wao.
Wanaume wakafanyiana matendo ya aibu na
wanaume wengine nao wakapata katika maisha
yao adhabu iliyowastahili kwa ajili ya upotovu
wao
.
KATIKA DUNIA YA LEO
Mambo yote yanatokea kama yaliyotokea Sodoma
nyakati hizo
i. Kutokuwajali maskini leo ni jambo
la kawaida
ii. Mambo ya ufisadi , kufuru ya kudai
hakuna Mungu na hata kudai binadamu
hakuumbwa bali alitokana na nyani
iii. Leo hii ushoga imekuwa ni suala
ambalo linaingizwa hata ndani ya katiba za nchi.
 
Ni ndefu lakini vumilia hivyo hivyo
SEHEMU YA PILI
28.Ndivyo ilivyokuwa katika siku za
Lutu: Watu walikuwa wakila na kuinywa,
wakinunua na kuuza, wakilima na kujenga.
29Lakini siku ile Lutu alipoondoka Sodoma,
ikanyesha mvua ya moto na kiberiti kutoka
mbinguni ukawaangamiza wote. 30‘‘Hivyo ndivyo
itakavyokuwa siku ile Mwana wa Adamu
atakapofunuliwa. 31Siku hiyo, mtu ye yote
aliyeko kwenye dari ya nyumba yake, vitu vyake
vikiwa ndani ya hiyo nyumba asishuke
kuvichukua. Vivyo hivyo mtu aliyeko shambani
asirudi nyumbani kuchukua cho chote.
32Mkumbukeni mke wa Lutu
! (Luka 17:28-32).
Haya ni maneno yaYesu Kristo alipokuwa akieleza
kuhusu mambo yatakayotokea kabla ya kurudi
kwake. Sodoma inatajwa kama mji ambao watu
wake walikuwa wenye kutenda dhambi nyingi sana
(Mwanzo 13:13). Na Lutu anatajwa kama mtu
aliyekuwa akiishi katika mji huo.
WAGENI WALIOMTEMBELEA IBRAHIMU
BWANA akamtokea Abrahamu karibu na
mialoni ya Mamre wakati alipokuwa ameketi
kwenye ingilio la hema lake wakati wa adhuhuri.
2Abrahamu akainua macho akaona watu watatu
wamesimama karibu naye. Alipowaona,
aliharakisha kutoka kwenye ingilio la hema lake
kuwalaki na kuwasujudia hadi nchi
(Mwanzo
18:1-2). Wageni hawa watatu, wakiwa
wameongozana na Bwana(Yesu Kristo),
walipokarimiwa na Abrahamu Na baada ya
kumbariki Sarah mke wa Abrahamu(Mwanzo
18:10) waliaga na walipoelekeza nyuso zao
Sodoma, Abrahamu akiwa anawasindikiza
(Mwanzo 18:16), ndipo Bwana akawaza ya
kwamba hatamficha Ibrahimu kuhusu kile
alichokuwa amekusudia kutenda fungu la 17.
Kumbe basi, ugeni huo haukuwa kwa ajili ya
kumtembelea Abrahamu, bali ulikuwa ni ugeni
uliomtembelea kwa kusudi maalumu, na kusudi
lenyewe likiwa ni kutangama MAMBO
YALIYOKUWA MBIONI KUIPATA MIJI YA SODOMA
NA GOMORA. Sasa tuangalie jumbe ambazo
malaika wale pamoja na Bwana walikuwa
wamepeleka kuhusiana na Sodoma na Gomora.
UJUMBE WA
KWANZA

Bwana alipobaki na Abrahamu kabla ya
wale malaika wawili kwenda Sodoma, akafunua
juu ya kusudio lake kwa miji ile kwa rafiki yake
Abrahamu, 20Basi BWANA akasema, “Kilio dhidi
ya Sodoma na Gomora ni kikubwa sana na
dhambi yao inasikitisha sana, 21kwamba
nitashuka nione kama waliyoyatenda ni mabaya
kiasi cha kilio kilichonifikia. Kama sivyo,
nitajua
” (Mwanzo 18:20-21). Ndipo malaika
wawili wakaondoka na kumwacha Abrahamu
akiwa na BWANA, na ndipo Abrahamu akatamuka
25Hilo na liwe mbali nawe, kufanya jambo kama
hilo, kuwaua wenye haki pamoja na waovu,
kuwatendea wenye haki sawasawa na waovu. Iwe
mbali nawe! Je, Mwamuzi wa dunia yote
hatafanya lililo sawa?
’’(Mwanzo 18:25), ndipo
Abrahamu akaanza kumuuliza BWANA kama
wakiwemo watu waaminifu kadha wa kadha ndani
ya mji kama atawaangamiza, alianza na 45,40,
hadi 10. Hapa ujumbe tunaoupata hapa ni
TANGAZOLA HUKUMU
UJUMBE WA PILI
Katika Mwanzo 19:1 tunasoma Malaika
wale wawili wakafika Sodoma wakati wa jioni, …,
Lutu aliwakaribisha, na wakamwambia atoe kila
mtu wake katika mji maana wapo karibu
kuuharibu(Mwanzo 19:12), naye Lutu alipoenda
kutoa taarifa kwa wakweze waliokuwa wameposa
binti zake, Biblia inasema, 14Kwa hiyo Loti alitoka
ili kuzungumza na wakwe zake, waliokuwa
wamewaposa binti zake. Akawaambia, “Fanyeni
haraka kuondoka mahali hapa, kwa kuwa BWANA
ni karibu kuangamiza mji huu!’’ Lakini wakwe
zake walifikiri kwamba alikuwa akitania.
(Mwanzo 19:14). Ujumbe waliofikisha malaika wale ni
TANGAZO LA UHARIBIFU WA
MIJI ILE

UJUMBE WA
TATU

Mwanzo 19:15-16 tunasoma 15Kunako
mapambazuko, malaika wakawahimiza Loti,
wakamwambia, “Fanya haraka! Mchukue mke
wako na binti zako wawili walioko hapa,
vinginevyo utaangamizwa wakati mji
utakapoadhibiwa.’’ 16Alipositasita, wale watu
wakamshika mkono wake na mikono ya mke
wake na binti zake wawili na kuwaongoza salama
nje ya mji, kwa kuwa BWANA alikuwa na huruma
kwao. 17Mara walipokwisha kuwatoa nje, mmoja
wao akawaambia, “Mkimbie kwa usalama wenu!
Msitazame nyuma, wala msisimame popote
katika tambarare
! Kimbilieni milimani, ama sivyo
mtaangamizwa!’’ kwa hiyo hapa ujumbe
uliopelekwa na ale malaika kabla ya kuharibiwa
kwa Sodoma ni ONDOKA.
JUMBE HIZO TATU
KATIKA NYAKATI ZA LEO

Katika kitabu cha ufunuo 14:6-12 tunasoma
6Kisha nikamwona malaika mwingine
akiruka juu angani, naye alikuwa na Injili ya
milele ya kuwatangazia wale waishio duniani,
yaani, kwa kila taifa, kabila, lugha na jamaa.
7Akasema kwa sauti kubwa, ‘‘Mcheni Mungu na
kumtukuza, kwa maana saa ya hukumu yake
imewadia. Mwabuduni Yeye aliyeziumba mbingu,
dunia, bahari na chemchemi za maji.’’
8Malaika wa pili akafuata akisema,
“Ameanguka! Ameanguka Babeli aliye mkuu, yeye
aliyeyafanya mataifa yote kulewa kwa mvinyo wa
ghadhabu ya uasherati wake.’
9Malaika wa tatu akawafuata hao wawili
akisema kwa sauti kubwa, “Kama mtu ye yote
anamwabudu huyo mnyama na sanamu yake na
kutiwa chapa yake kwenye kipaji chake cha uso
au kwenye mkono wake, 10yeye naye, atakunywa
mvinyo wa hasira kali ya Mungu ambayo
imemiminwa katika kikombe cha ghadhabu yake
pasipo kuchanganywa na maji. Naye atateswa
kwa moto uwakao na kiberiti mbele ya malaika
watakatifu na mbele za Mwana-Kondoo. 11Nao
Moshi wa mateso yao hupanda juu milele na
milele. Hakuna mapumziko, mchana wala usiku,
kwa wale wamwabuduo huyo mnyama na sanamu
yake, au kwa ye yote anayepokea chapa ya jina
lake.’’ 12Hapa ndipo penye subira na uvumilivu
wa watakatifu, yaani, wale wanaozishika amri za
Mungu na kudumu kuwa waaminifu kwa Yesu

Tunapata jumbe tatu katika mafungu hayo
juu
i/. HUKUMU ikiwa ni tangazo toka kwa
malaika wa kwanza(Ufu 14:7).
ii/. TANGAZO LA ANGUKO(UHARIBIFU) WA
BABELI
huu ni ujumbe toka kwa malaika wa pili
(Ufunuo
14:8)
Iii/. Onyo kwa wale wasiotii agizo la kutoka
BABELI ambalo linatolewa katika Ufunuo 18:4
4Kisha nikasikia
sauti nyingine kutoka mbinguni ikisema:
Tokeni katikati yake, enyi watu wangu, ili msije
mkashiriki, dhambi zake,ili usije
ukapatwa na pigo lake lo lote
Jumbe zote hizi ni sawa kabisa na jumbe zile
zilizotolewa kabla ya anguko la sodoma. Kumbe
kabla Yesu kristo kurudi hapa duniani, jumbe hizi
zitatangulia, watu waandaliwe kuhusu hukumu,
wajue BABELI NI NINI ili wajihadhari wasije
wakaingia huko, na pia wakimbie kutoka huko
BABELI (walio watu wa Mungu). Cha kujiuliza leo
hii makanisani na misikitini, jumbe hizi
zinahubiriwa?
 
Hii inahusu moto wa milele, samahani kama zitaonekama kama hazijapangiliwa, maana natumia simu na ninacopy na ku paste toka huko fb.
SEHEMU YA TATU
MOTO WA MILELE
Kabla ya kurudi kwa Yesu Kristo, dunia itapitia
nyakati za Lutu. Na wakati wa Lutu, makundi
yaliyokutwa ndani ya miji ile pia yatakuwepo kabla
ya kurudi kwa Yesu, makundi hayo ni kama
ifuatavyo.
i. Watakaokutwa ndani ya miji, rejea
Lutu na familia yake. Na hapa kutakuwepo na
makundi mawili ya watakaokutwa mjini, kundi la
wema(Lutu) na kundi la waovu.
ii. Watakaokutwa vijijini, mfano
Ibrahimu. Pia vijijini watakuwepo wema na waovu
maana hata katika eneo la Ibrahimu, walikuwepo
watu wengine lakini hata hawakuwakaribisha wale
wageni watatu.
iii. Watakaokuwa wamepokea ujumbe
wa onyo lakini wakaamua kuupuuzia mfano
wakwe wa Lutu walivyokataa kuamini ujumbe
ambao Lutu aliwapelekea(Mwanzo 19:14).
iv. Watakaokuwa wamechagua kupotea
kwa kujiunga katika mambo ya kishetani mfano
wa wasodoma.
Baada ya Lutu kutoka Sodoma, kilichofuatia ni
kuteketezwa kwa miji ile, katika Mwanzo 19:23-24
tunasoma 23Wakati Loti alipofika Soari, jua
lilikuwa limechomoza katika nchi. 24Ndipo
BWANA akanyesha moto wa kiberiti juu ya
Sodoma na Gomora, uliotoka mbinguni kwa
BWANA
. Leo hii watu wanafundishwa fundisho
hatari kuwa MOTO UTAWAUNGUZA WAOVU
MILELE NA MILELE, lakini hata kwa kurejea kauli
ya Yesu katika kitabu cha Luka 17:28-32,
utagundua kuwa watu wa Sodoma na Gomora
waliteketezwa milele na hivyo hakubaki hata mtu.
Shetani anatumia fundisho hilo ili kumuweka
Mungu machoni pa watu kama mkatili,
anayefurahia kuona waovu wakiwa wanateketea
motoni. Hebu tuone sifa za moto huo wa milele.
i. Huu ni moto aliowekewa tayari
IBILISI na malaika wake(Mathayo 25:41),
binadamu yeye atakuwemo baada ya kuchagua
yeye mwenyewe.
ii. Ni moto utakaowateketeza kabisa
waovu, katika kitabu cha Malaki 4:1-3 tunasoma
‘‘Hakika siku inakuja, itawaka kama tanuru.
Wote wenye kiburi na kila mtenda mabaya
watakuwa mabua makavu na siku ile inayokuja
itawawasha moto,’’ asema BWANA Mwenye
Nguvu. “Hakuna mzizi wala tawi litakalosalia
kwao. 2Bali kwenu ninyi mnaoliheshimu jina
langu, jua la haki litawazukia, lenye kuponya
katika mbawa zake. Nanyi mtatoka nje na
kurukaruka kama ndama aliyeachiwa kutoka
zizini. 3Kisha ninyi mtawakanyaga waovu nao
watakuwa majivu chini ya nyayo za miguu yenu
siku ile nitakayofanya mambo haya,” asema
BWANA Mwenye Nguvu
. Waovu hawawezi kuwa
majivu kama hawajaungua. Zaburi 37:9 tunasoma
9Kwa maana waovu watakatiliwa mbali, bali wale
wanaomtumaini BWANA watairithi nchi
. Na
warumi 6:23 inasomeka 23Kwa maana mshahara
wa dhambi ni mauti, bali karama y Mungu ni
uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu.

Hajasema mshahara wa dhambi ni kuishi milele
katika moto, bali ni mauti. Moto huu ni wa milele
kwa sababu utafutilia mbali uovu na kuukomesha
milele, malaki anasema ni moto ambao
hautabakisha hata shina moja la waovu.
MOTO WA MILELE NI NINI?
Kutoka 24:17 tunasoma 17Kwa Waisraeli utukufu
wa BWAN
A ulionekana kama moto uteketezao juu
ya mlima.
Kumbe Bwana ndiye moto uteketezao.
Pia Kumbukumbu 4:24 tunasoma 24Kwa kuwa
BWANA Mungu wenu ni moto ulao, Mungu
mwenye wivu. Bwana ni moto ulao
, na katika
Kumbukumbu 9:3 tunasoma 3Iweni na hakika leo
kwamba BWANA Mungu wenu ndiye
atakayetan
gulia kuvuka mbele yenu kama moto
uteketezao
. Atawaangamiza, atawatiisha mbele
yenu. Nanyi mtawafukuza na kuwaangamiza mara
moja, kama BWANA alivyowaahidi. Soma pia
Waebrania 12:29. Maungu hayo yote yanaeleza
kuwa Bwana ndiye moto uteketezao, na kwa kuwa
yeye hana mwanzo na mwisho, anaishi milele
hivyo basi yeye ndiye moto wa milele.
NI AKINA NANI WATAKAOKAA NA MOTO WA
MILELE?
Isaya 33:13-15 tunasoma 13Ninyi mlio mbali
sana, sikieni lile nililofanya, ninyi mlio karibu,
tambueni uweza wangu! 14Wenye dhambi katika
Sayuni wametiwa hofu, kutetemeka
kumewakumba wasiomcha Mungu: “Ni nani
miongoni mwetu awezaye kuishi na moto ulao?
Ni nani miongoni mwetu awezaye kuishi na moto
unaowaka milele?’’ 15Yeye aendaye kwa uadilifu
na kusema lile lililo sawa, yeye anayekataa faida
ipatikanayo kwa dhuluma. Kumbe watakatifu ndio
watakaokaa na moto uteketezao(BWANA) milele
na milele.

Kumbuka watu wa sodoma waliteketezwa
kwa moto na kiberiti rejea Mwanzo 19:24, na
mwisho waovu nao watateketezwa kwa moto na
kiberiti rejea Ufunuo 14:10, 20:10. Kwa hiyo
waovu watateketea milele katika ziwa la moto
(Moto na kiberiti) na sio kwamba watakuwa hai
milele na milele wakiungua, bali watakatifu ndio
watakaa na moto wa milele.
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…