Wasabato Masalia watimuliwa tena uwanja wa ndege, polisi watoa onyo la mwisho

kwani ni lazima wapae kutokea uwanjani(jka)?,mimi nilifikiri kwasababu wanatumia miujizaa wangeweza kupaa tokea eneo lolote ,na walipaswaniurukia hukohuko musoma
 
Yote yanategemea maana unazoweka kwenye sifa za "ubaba" na "utakatifu". Kwa Wakatoliki binadamu anaweza kabisa kupewa hadhi ya Utakatifu, na kuna Watakatifu wengi tu kwenye dhehebu la Ukatoliki. Sasa sijui wewe unashangaa kitu gani? Bottom line ni kwamba tafsiri ya mambo ya dini kiini chake ni imani. Kama huna imani utakuwa unapoteza muda wako bureee kukosoa imani za wenzako. Takbiru allah walibalu!

......"tha true substance of life"........welcome back man
 
Date::9/13/2008
Wasabato Masalia: Maisha halisi, imani za kutengana na familia, kuacha kazi (1)
Na Jackson Odoyo (wa gazeti la Mwananchi)

WIKI iliyopita nilifanikiwa kuishi kwa siku na waumini 52 wa dhehebu la Wasabato Masalia walioweka kambi maeneo ya Tabata Segerea jijini Dar es Salaam, ili kwenda Ulaya kuhubiri injili bila pasi za kusafiria wala viza.

Nilifika katika eneo hilo kwa mara ya kwanza Septemba 6 mwaka huu majira ya saa 2:00 asubuhi nilijitambulisha kwa waumini hao kama mwenzao mwenye malengo sawa ya kwao ya kuhubiri injili Ulaya na nchi nyingine nje ya Tanzania bila kujali kama nina pasi ya kusafiria au la.

Lakini lengo langu mahususi lilikuwa kutaka kujua jinsi waumini hao wanavyoishi katika eneo hilo na mikakati ya kutimiza matarajio yao.

Waumini hao walinipokea kwa furaha na kwa kuwa ilikuwa ni siku ya ibada, muda wa kuingia kanisani uliwadia walinipeleka mahali wanaposali.

Waumini hao wanasali katika jengo bovu lililoezuliwa paa yake na ndani yake hakuna viti, meza wala sakafu.

Ibaada yao inatofautiana kwa baadhi ya vipengele na ya Wasabato wa kawaida au Jumuia ya Makanisa ya Kisabato duniani.

Mambo yanayotofautiana ni namna ya kuendesha ibaada yao ambapo waumini wa kawaida wanaendesha vipindi vyao vya ibaada kwa kuzingatia ratiba maalumu kuazia shule ya sabato, mafunzo kwa njia ya vikundi, sadaka, burudani ya nyimbo za injili, kwaya na ibaada kuu.

Kwa upande wao wanayo ibaada kuu ambayo inafanyika kwa njia ya mafundisho ya bibilia na baadhi ya vitabu vinavyoelezea imani ya Masalio na kusujudu kwa kuinamisha vichwa hadi ardhini wakati wa sala.

Nilipata maelezo ya waumini mbalimbali, ikiwamo kanuni kuu ya kujiunga na dhehebu hilo, kuwa ni lazima uikane familia yako na kazi unayoifanya, ili uweze kumtumikia Mungu peke yake, kwa kuwa binadamu hawezi kuwatumikia mabwana wawili kwa wakati mmoja.

"Hiyo ndiyo kanuni kuu inayowafanya masalia kuzikimbia familia zao, kuacha kazi na kuamua kuzunguka sehemu mbalimbali kuitangaza imani ya dini yao kama walivyofanya mitume," alisema mmoja wao aliyejitambulisha kama Eric Mwakyusa.

Katika kundi hili kuna watu walikuwa wakifanya kazi katika migodi mbalimbali hapa nchini na wengine walikuwa wakulima, wafanyabiashara na watatu kati yao walikuwa walimu - wote wameacha kazi na kufanya kazi ya Mungu.

Wasabao hao wametoka maeneo mbalimbali ya nchi na ni wa makabila tofauti. Wapo Wapare, Wanyakyusa, Wahehe, Wasukuma, Wajita, Wakurya, Warangi, Wafipa,Wahaya na Wanyamwezi.

Kutokana na udadisi wangu, nilielezwa kuwa wengo wao walifika mahali hapo baada ya kutembea kwa miguu umbali mrefu kutoka katika mikoa yao na baadhi yao walifika kwa kuunganisha safari baada ya kupata rifti za magari ya mizigo.

Ibaada iliyoanza saa 2:30 asubuhi ilimalizika saa 7:30 mchana, tukaondoka kwa mguu kurudi mahali walipoweka kambi umbali wa takriban mita 400. Baada ya kufika mahali hapo tuliingia ndani ya pagale lenye vyumba vitatu na sebule, halina sakafu, fremu za madirisha wala milango.

Nilikaribishwa na kuketi kwenye vumbi kama wenyeji wangu walivyofanya, bila kujali unadhifu wangu wa siku hiyo hasa ikizingatiwa kuwa siku hiyo ilikuwa ya ibaada, kama ilivyo kawaida ya Wasabato siku hiyo ni moja ya siku maalumu ya kuvaa vizuri kuliko siku zote.

Baada ya makaribisho, nilipewa nafasi ya kujitambulisha mbele ya waumini wakiwamo wanawake na watoto wenye umri kati ya miaka saba na 12. Mmoja wa watoto hao Masinde ambaye ni mahiri katika imani ya dhehebu hilo.

Wanawake walioko katika kundi hilo ni kati ya nane na 10 na kwa ujumla waumini hao ni wenye umri kati ya miaka 40 na 65. Nilijieleza kadri ya uwezo wangu na kuonyesha moja vitambulisho vinavyoashia kuwa mimi ni Msabato halisi na kuwaeleza nia ya kujiunga nao na kuwa mmoja wa waumini wa dhehebu hilo.

Chakula

Baada ya utambulisho huo tulisujudu na kusali kwa pamoja na kasha chakula aina ya kande kikaandaliwa na sote tukashiriki pamoja mlo huo wa mchana.

Chakula hicho kilipikwa kwenye masufuria mawili makubwa na kupakuliwa katika masinia karibu 10 na kisha tukajigawa katika vikundi vya watu kati ya watano na sita kila moja na kuanza kupata mlo wetu.

Upatikanaji wa chakula cha waumini hao ni kudra za Mungu kwani hawafanyi kazi wala biashara yoyote lakini wanakula ingawa kula kwao ni kwa mashaka, kwani wanasema wakati mwingine wakikosa chakula wanashinda na kulala njaa.

Uchunguzi wangu ulibaini kuwa waumini hao wanapata chakula kwa njia ya misaada kutoka kwa wasamalia wema ambao wanaamini kwamba kundi hilo ni halali linalofanyakazi ya kutangaza injili, hivyo kila anayeguswa anapeleka chakula kama vile mchele, unga, sukari, chunvi, mboga za majani, na kuni. Wakati waumini hao hulazimika kuingia porini kutafuta kuni.

Moja ya imani ya Masalio hao ni kutokula samaki, ndege wala nyama na hawatumii mafuta ya aina yoyote zaidi ya mafuta ya karanga kwa madai kuwa ni vyakula vya anasa.

Huduma za choo na bafu

Baada ya kupata chakula katika siku yangu ya kwanza nilitaka kuonyeshwa sehemu ya kujisaidia. Si kwamba nilikuwa na haja hiyo, bali nilitaka kufahamu ni mahali gani wanajisaidia, hasa baada ya kuripotiwa kuwa jirani na eneo hilo amewafungia choo chake cha pipa kwa mdai kuwa wanakijaza.

Badala ya kuonyeshwa choo, nilionyeshwa njia ya kuelekea porini, kwamba ndio sehemu wanayojisaidia. Huko porini ni kuchafu kupindukia kwa kuwa wamepachafua kwa muda mrefu.

Nilipoulizia maji ya kuoga, nilielezwa nisubiri jioni ili niende kwenye mto unaopita jirani na eneo hilo, hivyo sikufanikiwa kuoga.

Mafundisho ya mchana

Saa chache baada aya chakula tulianza mafundisho ya bibilia na kila baada ya nusu saa tulikuwa tunapiga magoti na kusali na tunaendelea na mafundisho ya bibilia ya kujenga imani ya Sabato Masalio.

Waumini hao wanatumia bibilia na kuijengea hoja kuwa inaweza kuwapeleka kuhubiri mahali popote. Kwamba kitabu hicho kinaweza kuwafungulia njia kwenda popote wanapotaka.

Ilipofika saa 12 jioni tulikusanyika na kuendesha ibaada ya kufunga sabato. Katika ibaada hiyo kulikuwa na mafundisho na ufafanuzi wa kina na msisitizo wa uwezekano wa safari yao ya kwenda katika nchi za Ulaya kuhubiri njili kwa kutumia bibilia kama viza na pasi, hata kama serikali inawazuia lazima wataondoka.

Maisha ya usiku

Baada ya ibada hiyo kulikuwa na mapumziko mafupi. Wakati huo wa mapumziko nilipata fulsa ya kubadilishana mawazo na baadhi ya waumini hao nikilenga kufahamu sababu ya msingi iliyosababisha waamini kwamba kitabu hicho kitakatifu kilitosha kuwapeleka Ulaya.

Mmoja wao, Mwakyusa alisema kundi hilo lilikuwepo tangu zamani enzi za mitume, lakini kutokana na binadamu kumtendea Mungu dhambi na kuibuka kwa makundi mbalimbali ya manabii wa uongo waliamua kuliasi kutokana na sera zake kuwa ngumu.

Alisema kwa hapa Tanzania kundi hilo lilianzishwa rasmi mwaka 2006 chini ya Mchungaji Nyagori ambaye kwa sasa ni marehemu baada ya kugundua kwamba kundi la wanaojiita Wasabato Kamili linaendeleza ibada za kumchukiza Mungu.

Alifafanua kuwa moja ya ibaada hizo ni kupenda mambo ya anasa kama vile kuishi kwenye majumba ya kifahari, kula vyakula vya anasa, kununua magari ya kifahari, kuabudu kazi za mikoa na elimu dunia na kuangaikia mambo ya kidunia badala ya kuhangaikia masuala la Mungu.

Tuliendelea na mapumziko hayo mpaka wakati wa chakula cha usiku. Uliandaliwa uji na slesi za mkate na karanga. Baada ya chakula tuliingia tena katika mafundisho ya biblia na kusali kwa muda wa nusu saa.

Ibaada hiyo ilimalizika saa 4:00 usiku lakini kabla ya kuanza kwa utaratibu wa kulala nilifuatwa na wazee wawili wa kundi hilo na kuniuliza suala la kulala.

"Kijana, sisi tulitegemea kuwa utakuwa mgeni wetu kwa siku moja na baada ya Sabato kufungwa ungeondoka, lakini tunashangaa kukuona hapa mpaka hivi sasa una mpango wa kulala hapa?" alisema mmoja wao.

Niliwambia kuwa nilipofika hapo, niliwaeleza mipango yangu ya kuwepo mahali hapo na kuishi nao kwa zaidi ya siku mbili hadi tatu.

Utata wa mahali gani nitalala ulizidi kuwa kikwazo kati yangu na Masalio, kwani hawakutaka nilale nao katika jengo hilo. Tuliendelea na mazungumza kwa muda mrefu kiasa ambacho baadhi ya waumini walitufuata tulipokuwa tumeketi.

Sababu kubwa waliyoitoa ili nisilale pamoja nao ni kwamba kutokana na utaratibu wa maisha yao, sipaswi kulala pamoja nao kwani sijawa mshiriki kamili wa dhehebu hilo, hivyo wakanitaka niondoke usiku huo na kwenda kutafuta mahali pa kulala ili kesho waweze kukamilisha taratibu zao.

Mbali na sababu hiyo pia walisema kuwa mahali walipokuwa wamekabidhiwa na Wasamaria wema na idadi yao inafahamika, hivyo nisingeweza kulala hapo mpaka watakapokwenda kutoa taarifa kwa walimiki wa eneo hilo na mwenye pagale hilo.

Baada ya maelezo hayo, waumini watatu waliamua kunisindikiza mpaka maeneo ya Karakata kwenda kutafuta nyumba ya kulala wageni, kwa kuwa niliwaeleza nimetoka Musoma na sina mahali pa kufikia hapa jijini.

Hivyo, shauku yangu ya kuona jinsi waumini hao wanavyolala kwenye pagale lao ikagonga mwamba.

Endelea kufuatilia sehemu ya pili ya kisa cha maisha ya masalia hawa
 
Umetuacha na shauku kubwa sn mkuu tafadhali malizia sehem ya pili
 
Wabongo bwana!
Yaani Mama Rwakatare ametangaza kutungua watu waiokuwa wanruka hamkushangaa! Wakatoliki wanasema Bikira Maria alipalizwa mbinguni hamuwashangai, Wanaamini pia kwamba mtu akifa anakwenda Pargatory mpaka tumwombee kwanza, wala hamshtuki! Jamani mnakuja kushtuka hawa jamaa wanaoiamini BIBLIA kwamba inaweza kuwarusha kuwapeleka popote wapendapo?
Mimi jamani, zaidi ya kuona kama haki yao ya kimsingi nawasifia kwa kuwa na imani kubwa kwa kiwango hicho. Wako wengi wanaotangaza leo kwamba wanaponya bila dawa, wanaponya tena Ukimwi! kwa maneno tu, mbona hao nao hatuwasemi na kuwashangaa!

Ushauri wangu, naomba tuanze kuwashangaa kwanza wale wanaowamwita binadamu Baba Mtakatifu ilihali ni jina la Mungu muumbaji.

Period!

Hawana imani hata kidogo.
 
Wasabato Masalia watimuliwa tena uwanja wa ndege, polisi watoa onyo la mwisho

jamani nawaonea sana huruma.Kila mtu ana haki ya imani yake aamini atakavyo ili mradi asivunje sheria za mamlaka.Hata yesu aliheshimu mamlaka za Kaisari.Nawashauri watumie akili kuliko nguvu za kiimani.Ni kitu gani kinachofanya washindwe kutafuta pass za kusafiria muda wote huo.Pass ya kusafiria ni haki ya kila mwananchi ili mradi utaje vigezo vya unapotaka kwenda je ni kufanya nini?

Baadhi ya waumini Wasabato, wanaojitambulisha kama 'Masalia' baada ya kutimuliwa Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam, ambako wamekuwa wakipiga kambi kwa imani ya kunyakuliwa hadi Ulaya bila pasipoti, tiketi, visa na taratibu zingine za usafiri wa kimataifa.
Na Furaha Kijingo

KUNDI la waumini wa Dhehebu la Waadventista Wasabato Masalia, kwa mara ya tatu limesambaratishwa na askari wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere, baada ya kurudi tena uwanjani hapo huku wakiwa wameongezeka idadi yao kutoka 17 hadi kufikia 51.

Wasabato hao masalia, walifika katika uwanja huo mnamo saa 2:00 asubuhi huku wakiwa na mabegi yao tayari kwa safari wakisema: "Bwana alikuwa amewaambia tena kuwa jana ilikuwa ndio siku ya kuondoka na kuelekea nchi za Ulaya kuhubiri injili."

Mara baada ya kufika uwanjani hapo, askari wa uwanja huo wa ndege waliwauliza kwa lengo la kutaka kujua endapo awamu hii wamejikamilisha tayari kwa safari, lakini cha kushangaza waumini hao waliendelea kutoa majibu yale yale kwamba wao tiketi yao na hati za kusafiria ni Biblia.

Baada ya kujibiwa hivyo, askari hao waliamua kuorodhesha majina ya waumini hao na kuchukua jukumu la kuwapiga picha mmoja mmoja na kuwaamuru watoweke katika viwanja hivyo.

Kama ilivyokawaida ya waumini hao, pindi wanapotaka kufanya jambo lao lazima wainamishe vichwa vyao chini na kupiga magoti huku wakimuomba Mungu kimya kimya, ndivyo walivyofanya jana nje ya geti la kuingilia uwanjani hapo.

Baada ya kusali kwa dakika chache, waumini hao walianza safari ya kurudi katika eneo lao waliloweka kambi ambalo ni Tabata Magumi, ambapo waliondoka kwa maandamano huku wakiimba wimbo wao ambao ulikuwa una ujumbe usemao: “Tunasubiri Mavuno”.

Waumini hao wakati wakiondoka kwa maandamano, walisindikizwa na kundi la askari wa uwanja wa ndege, ambao walipofika barabara ya Nyerere, askari hao walizuia magari kwa muda wa sekunde kadhaa ili kundi hilo la waumini liweze kuvuka.

Akizungumza na Mwandishi wa habari hizi Mkuu wa Kituo cha Polisi cha uwanja huo wa ndege Saimoni Haule, alisema aliwapiga picha ili sura zao ziwe kumbukumbu na endapo wataonekana tena katika maeneo ya uwanja huo hatua kali zaidi zitachukuliwa dhidi yao.

“Sasa tumewaambia kuwa hii ni mara ya mwisho kwao kuja hapa, endapo tutaona tena sura zao hapa ndipo watakapo tutambua sisi nani,” alionya Kamanda Haule.

Haule alisema anasikitishwa kuona katika kundi hilo kuna watoto, ambao wangestahili kuwepo shuleni kwa kipindi hiki ukilinganisha na umri wao.

Hata hivyo, waumini hao walipoulizwa kuhusiana na msimao wao sasa, walisema msimamo wao kwenda Ulaya kuhubiri injili upo palepale hawajakata tamaa na kwamba wanaendelea kumsikiliza mungu atakachowaambia.

“Safari bado ipo, hata hivi unavyotuona tupo safarini hatujakata tamaa tunamsikiliza bwana, ”alisema mmoja wa waumini hao ambaye hakutaka kutaja jina lake, ila alisema yeye ni Mwinjilisti

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Abbas Kandoro, alisema kundi hilo la waumini analichukulia kama ni kundi la wazururaji pia wanakiuka sheria za nchi hivyo ni lazima atawachukulia hatua za kisheria.

“Kama unavyoelewa, serikali inapiga marufuku kitendo cha watu kuwatorosha wanafunzi shule sasa waumini hao wana watoto ambao wanahitajika kuwepo shule kwa sasa, lazima niwafuate huko waliko,”alisema Kandoro.

Kandoro aliongeza kwamba, anataka kujua kama dhehebu hilo limesajiliwa kisheria kutokana na imani yao ambayo watu wengi wameonekana kutokuielewa vizuri na kugeuka mshangao kwa kila mtu wa kizazi hiki.

Awali, Kandoro aliwapiga marufuku waumini hao kufika katika viwanja vya ndege kwani eneo hilo si la mchezo kama wanavyodhani.

Waumini wa Dhehebu la Waadiventista Wasabato Masalia, hivi sasa wameingia mwezi wa tatu tangu waweke kambi katika jiji hili la Dar es salaam, walifika kwa lengo la kusafiri kwenda nchi za Ulaya pasipokuwa na nyaraka zozote za kusafiria.

Awali, waumini hao idadi yao ilikuwa 17 lakini wamekuwa wakiongezeka siku hadi siku na sasa kufikia idadi ya watu 51, wameshafika katika uwanja huo wa ndege mara tatu kwa lengo la kusafiri pasipokuwa na nyaraka za kusafiria, mara zote hizo uongozi wa uwanja wa Ndege uliwafukuza katika eneo hilo.
 
Date::9/13/2008
Wasabato Masalia: Maisha halisi, imani za kutengana na familia, kuacha kazi (1)
Na Jackson Odoyo (wa gazeti la Mwananchi)

WIKI iliyopita nilifanikiwa kuishi kwa siku na waumini 52 wa dhehebu la Wasabato Masalia walioweka kambi maeneo ya Tabata Segerea jijini Dar es Salaam, ili kwenda Ulaya kuhubiri injili bila pasi za kusafiria wala viza.

Nilifika katika eneo hilo kwa mara ya kwanza Septemba 6 mwaka huu majira ya saa 2:00 asubuhi nilijitambulisha kwa waumini hao kama mwenzao mwenye malengo sawa ya kwao ya kuhubiri injili Ulaya na nchi nyingine nje ya Tanzania bila kujali kama nina pasi ya kusafiria au la.

Lakini lengo langu mahususi lilikuwa kutaka kujua jinsi waumini hao wanavyoishi katika eneo hilo na mikakati ya kutimiza matarajio yao.

Waumini hao walinipokea kwa furaha na kwa kuwa ilikuwa ni siku ya ibada, muda wa kuingia kanisani uliwadia walinipeleka mahali wanaposali.

Waumini hao wanasali katika jengo bovu lililoezuliwa paa yake na ndani yake hakuna viti, meza wala sakafu.

Ibaada yao inatofautiana kwa baadhi ya vipengele na ya Wasabato wa kawaida au Jumuia ya Makanisa ya Kisabato duniani.

Mambo yanayotofautiana ni namna ya kuendesha ibaada yao ambapo waumini wa kawaida wanaendesha vipindi vyao vya ibaada kwa kuzingatia ratiba maalumu kuazia shule ya sabato, mafunzo kwa njia ya vikundi, sadaka, burudani ya nyimbo za injili, kwaya na ibaada kuu.

Kwa upande wao wanayo ibaada kuu ambayo inafanyika kwa njia ya mafundisho ya bibilia na baadhi ya vitabu vinavyoelezea imani ya Masalio na kusujudu kwa kuinamisha vichwa hadi ardhini wakati wa sala.

Nilipata maelezo ya waumini mbalimbali, ikiwamo kanuni kuu ya kujiunga na dhehebu hilo, kuwa ni lazima uikane familia yako na kazi unayoifanya, ili uweze kumtumikia Mungu peke yake, kwa kuwa binadamu hawezi kuwatumikia mabwana wawili kwa wakati mmoja.

"Hiyo ndiyo kanuni kuu inayowafanya masalia kuzikimbia familia zao, kuacha kazi na kuamua kuzunguka sehemu mbalimbali kuitangaza imani ya dini yao kama walivyofanya mitume," alisema mmoja wao aliyejitambulisha kama Eric Mwakyusa.

Katika kundi hili kuna watu walikuwa wakifanya kazi katika migodi mbalimbali hapa nchini na wengine walikuwa wakulima, wafanyabiashara na watatu kati yao walikuwa walimu - wote wameacha kazi na kufanya kazi ya Mungu.

Wasabao hao wametoka maeneo mbalimbali ya nchi na ni wa makabila tofauti. Wapo Wapare, Wanyakyusa, Wahehe, Wasukuma, Wajita, Wakurya, Warangi, Wafipa,Wahaya na Wanyamwezi.

Kutokana na udadisi wangu, nilielezwa kuwa wengo wao walifika mahali hapo baada ya kutembea kwa miguu umbali mrefu kutoka katika mikoa yao na baadhi yao walifika kwa kuunganisha safari baada ya kupata rifti za magari ya mizigo.

Ibaada iliyoanza saa 2:30 asubuhi ilimalizika saa 7:30 mchana, tukaondoka kwa mguu kurudi mahali walipoweka kambi umbali wa takriban mita 400. Baada ya kufika mahali hapo tuliingia ndani ya pagale lenye vyumba vitatu na sebule, halina sakafu, fremu za madirisha wala milango.

Nilikaribishwa na kuketi kwenye vumbi kama wenyeji wangu walivyofanya, bila kujali unadhifu wangu wa siku hiyo hasa ikizingatiwa kuwa siku hiyo ilikuwa ya ibaada, kama ilivyo kawaida ya Wasabato siku hiyo ni moja ya siku maalumu ya kuvaa vizuri kuliko siku zote.

Baada ya makaribisho, nilipewa nafasi ya kujitambulisha mbele ya waumini wakiwamo wanawake na watoto wenye umri kati ya miaka saba na 12. Mmoja wa watoto hao Masinde ambaye ni mahiri katika imani ya dhehebu hilo.

Wanawake walioko katika kundi hilo ni kati ya nane na 10 na kwa ujumla waumini hao ni wenye umri kati ya miaka 40 na 65. Nilijieleza kadri ya uwezo wangu na kuonyesha moja vitambulisho vinavyoashia kuwa mimi ni Msabato halisi na kuwaeleza nia ya kujiunga nao na kuwa mmoja wa waumini wa dhehebu hilo.

Chakula

Baada ya utambulisho huo tulisujudu na kusali kwa pamoja na kasha chakula aina ya kande kikaandaliwa na sote tukashiriki pamoja mlo huo wa mchana.

Chakula hicho kilipikwa kwenye masufuria mawili makubwa na kupakuliwa katika masinia karibu 10 na kisha tukajigawa katika vikundi vya watu kati ya watano na sita kila moja na kuanza kupata mlo wetu.

Upatikanaji wa chakula cha waumini hao ni kudra za Mungu kwani hawafanyi kazi wala biashara yoyote lakini wanakula ingawa kula kwao ni kwa mashaka, kwani wanasema wakati mwingine wakikosa chakula wanashinda na kulala njaa.

Uchunguzi wangu ulibaini kuwa waumini hao wanapata chakula kwa njia ya misaada kutoka kwa wasamalia wema ambao wanaamini kwamba kundi hilo ni halali linalofanyakazi ya kutangaza injili, hivyo kila anayeguswa anapeleka chakula kama vile mchele, unga, sukari, chunvi, mboga za majani, na kuni. Wakati waumini hao hulazimika kuingia porini kutafuta kuni.

Moja ya imani ya Masalio hao ni kutokula samaki, ndege wala nyama na hawatumii mafuta ya aina yoyote zaidi ya mafuta ya karanga kwa madai kuwa ni vyakula vya anasa.

Huduma za choo na bafu

Baada ya kupata chakula katika siku yangu ya kwanza nilitaka kuonyeshwa sehemu ya kujisaidia. Si kwamba nilikuwa na haja hiyo, bali nilitaka kufahamu ni mahali gani wanajisaidia, hasa baada ya kuripotiwa kuwa jirani na eneo hilo amewafungia choo chake cha pipa kwa mdai kuwa wanakijaza.

Badala ya kuonyeshwa choo, nilionyeshwa njia ya kuelekea porini, kwamba ndio sehemu wanayojisaidia. Huko porini ni kuchafu kupindukia kwa kuwa wamepachafua kwa muda mrefu.

Nilipoulizia maji ya kuoga, nilielezwa nisubiri jioni ili niende kwenye mto unaopita jirani na eneo hilo, hivyo sikufanikiwa kuoga.

Mafundisho ya mchana

Saa chache baada aya chakula tulianza mafundisho ya bibilia na kila baada ya nusu saa tulikuwa tunapiga magoti na kusali na tunaendelea na mafundisho ya bibilia ya kujenga imani ya Sabato Masalio.

Waumini hao wanatumia bibilia na kuijengea hoja kuwa inaweza kuwapeleka kuhubiri mahali popote. Kwamba kitabu hicho kinaweza kuwafungulia njia kwenda popote wanapotaka.

Ilipofika saa 12 jioni tulikusanyika na kuendesha ibaada ya kufunga sabato. Katika ibaada hiyo kulikuwa na mafundisho na ufafanuzi wa kina na msisitizo wa uwezekano wa safari yao ya kwenda katika nchi za Ulaya kuhubiri njili kwa kutumia bibilia kama viza na pasi, hata kama serikali inawazuia lazima wataondoka.

Maisha ya usiku

Baada ya ibada hiyo kulikuwa na mapumziko mafupi. Wakati huo wa mapumziko nilipata fulsa ya kubadilishana mawazo na baadhi ya waumini hao nikilenga kufahamu sababu ya msingi iliyosababisha waamini kwamba kitabu hicho kitakatifu kilitosha kuwapeleka Ulaya.

Mmoja wao, Mwakyusa alisema kundi hilo lilikuwepo tangu zamani enzi za mitume, lakini kutokana na binadamu kumtendea Mungu dhambi na kuibuka kwa makundi mbalimbali ya manabii wa uongo waliamua kuliasi kutokana na sera zake kuwa ngumu.

Alisema kwa hapa Tanzania kundi hilo lilianzishwa rasmi mwaka 2006 chini ya Mchungaji Nyagori ambaye kwa sasa ni marehemu baada ya kugundua kwamba kundi la wanaojiita Wasabato Kamili linaendeleza ibada za kumchukiza Mungu.

Alifafanua kuwa moja ya ibaada hizo ni kupenda mambo ya anasa kama vile kuishi kwenye majumba ya kifahari, kula vyakula vya anasa, kununua magari ya kifahari, kuabudu kazi za mikoa na elimu dunia na kuangaikia mambo ya kidunia badala ya kuhangaikia masuala la Mungu.

Tuliendelea na mapumziko hayo mpaka wakati wa chakula cha usiku. Uliandaliwa uji na slesi za mkate na karanga. Baada ya chakula tuliingia tena katika mafundisho ya biblia na kusali kwa muda wa nusu saa.

Ibaada hiyo ilimalizika saa 4:00 usiku lakini kabla ya kuanza kwa utaratibu wa kulala nilifuatwa na wazee wawili wa kundi hilo na kuniuliza suala la kulala.

"Kijana, sisi tulitegemea kuwa utakuwa mgeni wetu kwa siku moja na baada ya Sabato kufungwa ungeondoka, lakini tunashangaa kukuona hapa mpaka hivi sasa una mpango wa kulala hapa?" alisema mmoja wao.

Niliwambia kuwa nilipofika hapo, niliwaeleza mipango yangu ya kuwepo mahali hapo na kuishi nao kwa zaidi ya siku mbili hadi tatu.

Utata wa mahali gani nitalala ulizidi kuwa kikwazo kati yangu na Masalio, kwani hawakutaka nilale nao katika jengo hilo. Tuliendelea na mazungumza kwa muda mrefu kiasa ambacho baadhi ya waumini walitufuata tulipokuwa tumeketi.

Sababu kubwa waliyoitoa ili nisilale pamoja nao ni kwamba kutokana na utaratibu wa maisha yao, sipaswi kulala pamoja nao kwani sijawa mshiriki kamili wa dhehebu hilo, hivyo wakanitaka niondoke usiku huo na kwenda kutafuta mahali pa kulala ili kesho waweze kukamilisha taratibu zao.

Mbali na sababu hiyo pia walisema kuwa mahali walipokuwa wamekabidhiwa na Wasamaria wema na idadi yao inafahamika, hivyo nisingeweza kulala hapo mpaka watakapokwenda kutoa taarifa kwa walimiki wa eneo hilo na mwenye pagale hilo.

Baada ya maelezo hayo, waumini watatu waliamua kunisindikiza mpaka maeneo ya Karakata kwenda kutafuta nyumba ya kulala wageni, kwa kuwa niliwaeleza nimetoka Musoma na sina mahali pa kufikia hapa jijini.

Hivyo, shauku yangu ya kuona jinsi waumini hao wanavyolala kwenye pagale lao ikagonga mwamba.

Endelea kufuatilia sehemu ya pili ya kisa cha maisha ya masalia hawa
Hivi kama wamekimbia familia zao hawaoni kuwa ni dhambi kubwa wanafanya? unaacha watoto wako na mke wako na ugumu wa maisha na sijui kama watoto wako shule ada inadaiwa itakuwaje.Kwa taarifa yao wamebugi step kama wanafikiria mafuta mengine ni mabaya basi mafuta ya karanga yana cholesterol nyingi mno.Kwa kumbukumbu yangu mbona YESU hakutumia mtindo huu wa kusambaza injili?.Nakumbuka kuna jamaa mzungu wingereza msabato alifariki dunia vile alikataa kuongezewa damu vile thehebu lake linasema damu ni uhai huwezi kuongezewa na binadamu mwingine.Kuna mama mmoja daktari namuhifadhi jina mama R alikuwa hospitali flani alifukuzwa kazi kijanja vile alikuwa msabato sasa kwa imani yake hata mgonjwa aje hospitali ana malaria na damu imekwisha kabisa hawezi muandikia aongezewe damu wakuu wa hosptali wakaona atawaharibia biashara wakamuondoa kijanja.Sipingi dini yao maana hakuna ajuaye atafika kwa nani akifa ila kuna baadhi ya mambo mtu na akili zako ukiona unaona hii sio sawa 1.Kukimbia familia yako 2.Kutokufanya kazi duhhhhh mungu siku ya mwisho atakuwa na kazi ngumu sana kuangalia sera mbali mbali kutoka dini mbali mbali
 
Mwaka 2008 Wasabato Masalia walitinga Airport Dar wakitaka kwenda ng'ambo wakaeneze injili bila kuwa na documents yoyote kama visa, passport, tiketi nk.

IMANI BILA ELIMU NI USHIRIKINA

#ElimikaWikiendi
 
Mwaka 2008 Wasabato Masalia walitinga Airport Dar wakitaka kwenda ng'ambo wakaeneze injili bila kuwa na documents yoyote kama visa, passport, tiketi nk

IMANI BILA ELIMU NI USHIRIKINA

#ElimikaWikiendi
 
Attachments

  • 1000022713.jpg
    1000022713.jpg
    12.7 KB · Views: 1
Back
Top Bottom