Warning: Disturbing pics!

Warning: Disturbing pics!

Ulevi, ujinga, umasikini, mila potofu,kuchanganyikiwa,kuchokana, kukosa moyo wa huruma,khiyana,mfumo dume,......................................inaweza ikawa sababu moja wapo.

Hivi unajua kuna wanaume tunanyanyaswa na tunapigwa lakini tunaogopa kuripoti?????
 
mhh aisee hii ni kali... Ndiyo jamii nyingi za kiafrika zilivyo. Lakini zitabadilika kwani hata huko tunako tolea mfano walikuwa kama sisi. Hivyo inabidi elimu iendelee kutolewa kuwa mwanamke si kitu cha kupiga tu au kupiga siyo njia pekee ya kumfunza mtu au kumwelewesha...

...huko tunakotolea mifano kibao kimegeuka, mwanaume ndio anatandikwa makofi kisha anatupiwa virago nje, majority utawakuta kwenye subways, sleeping rough! 🙂

Hivi unajua kuna wanaume tunanyanyaswa na tunapigwa lakini tunaogopa kuripoti?????

...unaogopa kwa sababu zipi mkuu? yaani unadundwa halafu anakwambia ukishtaki mkong'oto zaidi nawe unaamini? 🙁
 
Jamani najua wengi humu ni watetezi wa haki za wanawake, lakini kuna wakati inabidi kichapo kichukue nafasi yake ndio heshima ipatikane. Nina live case, kuna siku mume wangu alinipigia simu kwamba angechelewa kurudi nyumbani kwa sababu alikuwa na mkutano muhimu na baadhi ya watu na alinieleza kwenye mkutano huo atakuwepo jirani yetu mmoja hivi ambaye ni mwanaume. Mume wangu alirudi nyumbani siku hiyo saa saba usiku ambayo sio kawaida yake lakini kwa kuwa aliishanitaarifu, sikuwa na pressure. Tatizo lilikuwa kwa huyo jirani yetu ambaye alipewa lift na mume wangu kurudi nyumbani. Ilichukua karibu dakika 40 huyo mke wa jirani yetu kumfungulia mume wake mlango. Na mlango ulipofunguka ilikuwa kasheshe moja kwa moja na uliibuka ugomvi wa ajabu mpaka tukakubaliana na mume wangu twende kusaidia kuamulia huo ugomvi. Tatizo mke wa huyo jirani yetu hana simu na hivyo ilikuwa vigumu kumfikishia ujumbe mke wake kama alivyofanya mume wangu. Tulifanikiwa kuumaliza huo ugomvi lakini tayari mwanamke aliisha umia vibaya sana.

Nia ya kusema hayo ni kuwaomba wana JF wasikimbilie kuwalaumu wanaume kwani mara nyingi wanawake na sisi tunakuwa chanzo cha matatizo bila kusema wanaume ambao nao wanapata kibano kwa wake zao ingawa katika mazingira ya kawaida hawapigi kelele kama tunavyopiga sisi wanawake.

Tiba
 
Tusiwe watu wakulamu tu,kuna makabila kama ya wakulya(ambalo ndilo langu),usipompiga mkeo hiyo inamaanisha huna upendo kwa mkeo,kutokanana hali hiyo atafanya kila njia kusudi umuezeke makofi,nabaada ya hapo upendo unaongezeka ndani ya nyumba,maana ukiwa umemtandika sawasawa itabidi uanze kukumbebeleza na kumpeleka hospital na kumjulia halikila mara,na hilo ndilo alilo kuwa analitaka,nasema hivyo maana mimi ni kabila hilo na huwaga mke wangu,akitaka tuwe karibu zaidi,huwa anatafuta sababu za mimi nimuezeke makofi,hiyo ni sehemu ya utamaduni wetu(Mara boys and our neighbors).


Nilijua tu lazima hawa watakuwa watani zangu Wakurwa. Murra Amang'ana gasarikire!
 
...Nia ya kusema hayo ni kuwaomba wana JF wasikimbilie kuwalaumu wanaume kwani mara nyingi wanawake na sisi tunakuwa chanzo cha matatizo bila kusema wanaume ambao nao wanapata kibano kwa wake zao ingawa katika mazingira ya kawaida hawapigi kelele kama tunavyopiga sisi wanawake.

Tiba

...te he 😀 dah,....ndio kusema uliona sawa huyo mw'mke alivyokula mkong'oto?
 
Kwa maoni yangu hakuna chochote anachoweza kufanya girlfriend au mke kinachostahili apate kipigo toka kwa boyfriend au mumewe. Mkishindana kila mtu achukue hamsini zake salama salimini.

Kama hujui kucontol hasira zako na umemrushia ngumi, teke au hata kichwa kaanguka na kufariki, utajuta for the rest of your life. Life is precious to have such a regret for the rest of your life.
 
Tatizo lilikuwa kwa huyo jirani yetu ambaye alipewa lift na mume wangu kurudi nyumbani. Ilichukua karibu dakika 40 huyo mke wa jirani yetu kumfungulia mume wake mlango. Na mlango ulipofunguka ilikuwa kasheshe moja kwa moja na uliibuka ugomvi wa ajabu mpaka tukakubaliana na mume wangu twende kusaidia kuamulia huo ugomvi. Tatizo mke wa huyo jirani yetu hana simu na hivyo ilikuwa vigumu kumfikishia ujumbe mke wake kama alivyofanya mume wangu. Tulifanikiwa kuumaliza huo ugomvi lakini tayari mwanamke aliisha umia vibaya sana.

Tiba

Yaani kuchelewa kufungua mlango kwa dakika 40 kulistahili kipigo!? Je, angemkuta na mwanaume humo ndani si angemuua kabisa? Inasikitisha kuona baadhi ya wanawake wanaona 'wanastahili kipigo' toka kwa waume zao.
 
............... Tatizo mke wa huyo jirani yetu hana simu na hivyo ilikuwa vigumu kumfikishia ujumbe mke wake kama alivyofanya mume wangu.


Tiba

Hiyo ilikuwa kasheshe, lakini wewe kama jirani pia ulikuwa na nafasi ya kumueleza jirani yako kabla, ya kwamba hao waume zenu watachelewa.
Lakini hata hivyo bado tatizo lilikuwa kwa mwanaume kama alijua kuwa atachelewa alipaswa kumfahamisha mke wake mapema kama alivyofanya wa kwako. Suppose kama ingekuwa ni wewe obvious unge-react negatively,japo in a different way.
 
Back
Top Bottom