Warioba: Mimi na Salim urais basi

Mzee Warioba Una heshima kubwa nchi hii Sikushauri ujihishishe nna waganga njaa wa aina yoyote iwe CCM au UKAWA
 
Wazo lako jema lakini napenda huyu mzee abakie tu hazina kwa nchii
 
Wadau, sio wazo wala mchango, wala si kitu cha kufikirika ila kwa uhahika kabisa Napenda kuwashauri vyama vyote vinavyounda ukawa, kua jibu sahihi la katiba ya tanzania, na ili kuleta mapinduzi katika taifa ili muweke tofauti, tamaa na matakawa yenu kichama na kumsimamisha Jaji Joseph Sinde Warioba kuwania uraisi kwenye uchaguzi mkuu mwakani. Sisi wapenda maendeleo, wapenda haki na usawa, wapenda tanzania mpya tutakua nyuma yenu. Tafadhari zingatieni hilo....najua humu ndani viobgozi wa cuf, chadema, nccr, na vyama vyote vinavyounda ukawa wapo msipuuzie hili.

NB: kwa msisitizo zingatieni hili.

Ukawa hii ni nafasi ya kuingia Ikulu, mgombea wenu awe WEarioba, straight IKULU. Nafasi hii Mungu kaileta, msiiachie!
 
Umri ni namba; Raisi Reagan wa Marekani aliingia madarakani akiwa na umri mkubwa kuliko umri wa Nyerere alipostaafu.

hata Mandela aliongoza akiwa mzee! unakumbuka cku ile anatoa hotuba bungen alisimama karibia masaa matano hata jk hawez kusimama muda mrefu huo laigwanan ndo kabsa nasikia hata kushikiria kikombe cha chai ni issue!
 
Umri kisiwe kigezo kikuu cha urais

tutazame uwezo binafsi na weledi

ujana au uzee usiwe kigezo cha urais

jaman watz tuelewe mara moja moja bas
 
Kwakweli anastahili kugombea, na kama vyama havimpi nafasi basi ikumbukwe kwamba 'katiba mpya' inaruhusu wagombea huru pia!

 
Ndugu zangu Kusema Kweli, huyu Mzee Jaji Joseph Warioba ambaye ni Mwenyekiti wa Tume ya Katiba Mpya, ametokea Kuwa Kiongozi wa tatu Baada ya Dr.Slaa na Mhe.Mbowe, Kunivutia sana hasa Kwa Misimamo yao ya Kiutendaji pale Wanaposimamia Kile Wanachokiamini Kwa niaba ya wengi. Jaji Warioba licha ya Kuwa Kada na Mwanachama wa CCM, ameuonyesha Dhahiri Ukomavu wake wa Kisiasa Katika Kujenga, Kutetea na Kusimamia hoja zake zenye Maslahi Kwa Taifa letu Kwa Ujumla bila Kuelemea Upande wowote. Jaji Warioba pamoja na Kukumbana na Shinikizo Kubwa Kutoka Upande wa Chama Chake, tena Shinikizo linaloambatana na Matusi, Kebehi, Dharau, Udharirishwaji n.k, Lakini Jaji Warioba anaendelea Kuwa Jasiri Kila Kukicha Katika Kutetea hoja za Wanyonge wa Taifa hili na Kubeba Mzigo wa Lawama zote Inazotupiwa Tume anayoiongoza, Ilimradi Kile anachoamini Kimeelezwa na Watanzania, Kiwasilishwe Bungeni. Mzee Warioba ni Mtu wa Pili baada ya Dr.Slaa, anayeweza Kugombea Urais 2015 Kwa Sababu ya Hekima, na Busara zake Kama za Mwl.Nyerere.

Mnataka kuigeuza Tanzania kuwa Zimbabwe?
 
Warioba mtu tuko nae kuna siku watamwelewa na haki itatendeka,tatizo la nchi yetu unafiki mwingi ,lakini viongozi wetu wanajua kabisa ukweli lakin wanafkiri wanatukomoa,one day kitaeleweka.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom