Warioba asisitiza katiba mpya Tanzania

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,790
288,007

Warioba asisitiza katiba mpya Tanzania​

WARIOBA ASISITIZA KATIBA MPYA TANZANIA | 13.07.2021​

57421551_101.jpg

Vuguvugu la kutaka mabadiliko ya katiba mpya Tanzania bado liko juu na safari hii, waziri mkuu mstaafu na aliyekuwa mwenyekiti wa tume ya mabadiliko ya katiba, Jaji Joseph Warioba ametoa himizo hilo.​

Nchini Tanzania vuguvugu la kutaka mabadiliko ya katiba mpya bado liko juu na safari hii, waziri mkuu mstaafu na aliyekuwa mwenyekiti wa tume ya mabadiliko ya katiba, Jaji Joseph Warioba amejitokeza na kusisitiza haja ya kuwa na maridhiano yatayosaidia kupatikana kwa katiba mpya.

Hayo yanajiri wakati Rais Samia Suluhu Hassan akisisitiza kuwa ingawa utawala wake unatambua jambo hilo lakini unatoa kwanza kipaumbele katika kukuza uchumi. Hoja ya Warioba aliyeitoa katika mahojiano na kituo kimoja cha televisheni cha jijini Dar es Salaam huenda ikachangiza madai yanayoendelea kuibuliwa na wanasiasa hasa wa upinzani wanashinikiza katiba mpya.

Medani ya siasa imechukua nafasi kubwa katika himizo la katiba mpya.

55471061_101.jpg

Kiongozi wa upinzani wa Tanzania, Freeman Mbowe
Wanasiasa hao kwa nyakati tofauti wamekuwa wazitolea mwito mamlaka za serikali kufufua mchakato wa katiba hiyo mpya uliokwama tangu mwaka 2014 baada ya kufika katika bunge maalumu la katiba.

Jaji Warioba katika mahojiano hayo ingawa hakubainisha msimamo wa moja kwa moja kuhusu takwa la katiba hiyo mpya, lakini ameashiria haja ya kuendelea na mchakato huo na amewashauri wanasiasa kuwa tayari kukutana na Rais Samia ili kuanzisha majadiliano yatayofungua njia ya kumaliza mkwamo huo.

Licha ya katiba kutajwa ni hitaji la kitaifa linapaswa kuwashirikisha wananchi wa kona zote, hata wanasiasa ndio wanaonekana kulivalia njuga zaidi jambo hilo na madai yao makubwa yanaangukia juu ya kutaka tume huru ya uchaguzi, mshindi wa urais awe ni yule anayepata zaidi ya asilimia 50 ya kura na matokeo ya uchaguzi wa urais kuhojiwa mahakamani.

Fikra ya kugawika wanasiasa kimtazamo Tanzania.

Kwa upande mwingine, hatua ya Jaji Warioba kutaka wanasiasa kuwa tayari kuanzisha majadiliano na Rais Samia kuhusu hoja zao hizo, baadhi ya wanasiasa na wachambuzi wamegawika katika kulijadili jambo hili. Mathalani, mwanasiasa na mchambuzi wa mambo, Sammy Ruhuza amesema anaepinga suala la katiba mpya anajiweka mbali na wananchi.

Wanasiasa wa upinzani wanadai kuwa katiba ya sasa iliyondikwa mwaka 1977 na baadaye kufanyiwa mabadiliko kadhaa ikiwemo ya mwaka 1992 kuruhusu mfumo wa vyama vingi inatoa upendelea kwa chama tawala CCM.

Chama hicho tawala ingawa katika ilani yake ya uchaguzi ya mwaka 2015 -2020 iliweka kipengele cha kuendelea na mchakato wa katiba na baadaye kipengele hicho kuondolewa kwenye ilani iliyofuata kimekuwa kikisitiza kuwa katiba ya sasa ni bora na inapendekeza kuendelea nayo.
 
Kuna watu wanapenda vitu kwa wepesi wepesi sana. Wanataka katiba kupitia watu wengine, TOKA DAI KATIBA KAMA KWELI UNAIHITAJI.
 
Watanzania tuinject uchumi tunge juhudi za mama katika kuinua uchumi, haya ya katiba yatatuchelewesha Ni ajenda za wanasiasa hasa upinzani
 
Only stupid people like you are very comfortable of what is going on in this country. Who told you that there is cut off date on what to post on this forum?

Reposting 13 July article shows some desperation
 
Kwa wenye ufinyu wa akili tu ambao wanadhani kubambikiwa kesi ya ugaidi Mbowe hakutawatokea wao. Wanataka kuendelea kuishi katika nchi iliyojaa dhuluma na udhalimu wa kutisha.
Watanzania tuinject uchumi tunge juhudi za mama katika kuinua uchumi, haya ya katiba yatatuchelewesha Ni ajenda za wanasiasa hasa upinzani
 
Only stupid people like you are very comfortable of what is going on in this country. Who told you that there is cut off date on what to post on this forum?

Hata wabakaji sasa mnajiona mna akili

pumbavu sana wewe
 
Warioba asisitiza katiba mpya Tanzania​

WARIOBA ASISITIZA KATIBA MPYA TANZANIA | 13.07.2021​

57421551_101.jpg

Vuguvugu la kutaka mabadiliko ya katiba mpya Tanzania bado liko juu na safari hii, waziri mkuu mstaafu na aliyekuwa mwenyekiti wa tume ya mabadiliko ya katiba, Jaji Joseph Warioba ametoa himizo hilo.​

Nchini Tanzania vuguvugu la kutaka mabadiliko ya katiba mpya bado liko juu na safari hii, waziri mkuu mstaafu na aliyekuwa mwenyekiti wa tume ya mabadiliko ya katiba, Jaji Joseph Warioba amejitokeza na kusisitiza haja ya kuwa na maridhiano yatayosaidia kupatikana kwa katiba mpya.

Hayo yanajiri wakati Rais Samia Suluhu Hassan akisisitiza kuwa ingawa utawala wake unatambua jambo hilo lakini unatoa kwanza kipaumbele katika kukuza uchumi. Hoja ya Warioba aliyeitoa katika mahojiano na kituo kimoja cha televisheni cha jijini Dar es Salaam huenda ikachangiza madai yanayoendelea kuibuliwa na wanasiasa hasa wa upinzani wanashinikiza katiba mpya.

Medani ya siasa imechukua nafasi kubwa katika himizo la katiba mpya.

55471061_101.jpg

Kiongozi wa upinzani wa Tanzania, Freeman Mbowe
Wanasiasa hao kwa nyakati tofauti wamekuwa wazitolea mwito mamlaka za serikali kufufua mchakato wa katiba hiyo mpya uliokwama tangu mwaka 2014 baada ya kufika katika bunge maalumu la katiba.

Jaji Warioba katika mahojiano hayo ingawa hakubainisha msimamo wa moja kwa moja kuhusu takwa la katiba hiyo mpya, lakini ameashiria haja ya kuendelea na mchakato huo na amewashauri wanasiasa kuwa tayari kukutana na Rais Samia ili kuanzisha majadiliano yatayofungua njia ya kumaliza mkwamo huo.

Licha ya katiba kutajwa ni hitaji la kitaifa linapaswa kuwashirikisha wananchi wa kona zote, hata wanasiasa ndio wanaonekana kulivalia njuga zaidi jambo hilo na madai yao makubwa yanaangukia juu ya kutaka tume huru ya uchaguzi, mshindi wa urais awe ni yule anayepata zaidi ya asilimia 50 ya kura na matokeo ya uchaguzi wa urais kuhojiwa mahakamani.

Fikra ya kugawika wanasiasa kimtazamo Tanzania.

Kwa upande mwingine, hatua ya Jaji Warioba kutaka wanasiasa kuwa tayari kuanzisha majadiliano na Rais Samia kuhusu hoja zao hizo, baadhi ya wanasiasa na wachambuzi wamegawika katika kulijadili jambo hili. Mathalani, mwanasiasa na mchambuzi wa mambo, Sammy Ruhuza amesema anaepinga suala la katiba mpya anajiweka mbali na wananchi.

Wanasiasa wa upinzani wanadai kuwa katiba ya sasa iliyondikwa mwaka 1977 na baadaye kufanyiwa mabadiliko kadhaa ikiwemo ya mwaka 1992 kuruhusu mfumo wa vyama vingi inatoa upendelea kwa chama tawala CCM.

Chama hicho tawala ingawa katika ilani yake ya uchaguzi ya mwaka 2015 -2020 iliweka kipengele cha kuendelea na mchakato wa katiba na baadaye kipengele hicho kuondolewa kwenye ilani iliyofuata kimekuwa kikisitiza kuwa katiba ya sasa ni bora na inapendekeza kuendelea nayo.
Huyo nae ni Kati ya wale dhaifu walioshindwa kuleta Katiba kipindi cha jk kwamba saizi ndio kajua Katiba inahitajika?

Hakuna Katiba hapo
 
Usipotoshe Warioba hakufanya lolote lile la kuzuia kupatikana kwa Katiba mpya. Kikwete ndiye alikuwa chanzo baada ya kutishwa na maccm wenzie kwamba “hawatashinda” tena chaguzi na kumtisha kuanika maovu yake aliyoyafanya yeye na kundi lake la wana mtandao katika Kampeni za 2005.

Back
Top Bottom