Watanzania kwa mujibu wa sensa ya 2012 wanafikia milioni 44.9, wanaoruhusiwa kupiga kura wanfikia milioni 20. Waliotoa maoni katika kuunda rasimu wanafika laki 3.5 kwa misingi hii hata yeye aliyefungua Bunge la Katiba anapohoji idadi ya watu anajikanganya nafikili ingekuwa ana akili kama angesema watanzania hawana haja ya kutengeneza Katiba mpya kwa sababu hawakujitokeza kutoa maoni. Hii maana yake nini! kama mkutano wa kujadili upatikanaji wa maji umeitishwa kukawa na watu sema 200 halafu waliotoa dukuduku lao kuhusu suala hili ni 10 maana yake hawa 190 wanaridhika na hali iliyopo hivyo hskuns haja ya kuleta maji au mradi wowote wa maendeleo kwa tafsiri yako. Naomba tutofautishe kati ya kura ya maoni na kutoa maoni, mbona wabunge wetu wanaenda bungeni kutunga sheria wakiwa karibia 350 kati ya wananchi milioni karibia 45 bila hata kukusanya sahihi za wananchi ili kujua kama ndiyo mtazamo wao lakini tunakubali? ni ujinga ambao umetokana na kuwa na majibu kabla ya swali. Dhamira yako ni kupinga mapendekezo ya Serikali 3 lakini sababu yako inapelekea kujikanganya zaidi kuliko kueleweka.