Zack Abdul
JF-Expert Member
- Mar 9, 2026
- 319
- 314
Mwanasiasa Jacob Samwel Malate wa Ilala Dar es Salaam amemshutumu Waziri Mkuu Mstaafu Mzee Joseph Sinde Warioba kwa kusababisha taharuki na kuchochea mzozo katika jamii kufuatia kauli alizotoa hivi karibuni alipohojiwa na chombo kimoja cha habari za mtandaoni.
Mzee Malate ameelezea kushangazwa na tabia ya Mzee Warioba akisema Mzee huyu amekuwa na tabia zisizo za kiuongozi na zenye nia mbaya kwa Serikali na nchi ambayo yeye mwenyewe aliwahi kuitumikia.
Mzee Malate ameungana na kauli iliyowahi kutolewa na Marehemu Kepteni John Komba kuwa Mzee Warioba ni tatizo pale alipokuwa akizungumza na vyombo vya habari kupinga mjadala uliokuwa unaendelea Bungeni kuhusu mchakato wa Katiba Mpya ambao hatimaye ulisababisha Katiba Mpya kutopatikana.
“Huyu Mzee anadhani mawazo yake ni lazima yawe, anataka Serikali ifanye anavyotaka yeye, anapenda sana umaarufu wa kwenye vyombo vya habari, na anadharau sana viongozi wa Serikali waliopo, hiki kitu sio sawa” amesisitiza Mzee Malate.
Aidha, Mzee Malate ameshauri Chama Cha Mapinduzi na Serikali imchukulie hatua Mzee Warioba kutokana na kutumia wadhifa wake uliopita vibaya kwa kuwa unaweza kuiingiza nchi katika matatizo makubwa yatakayoleta athari kwa watu wengi.
“Sasa Mzee Warioba aliwahi kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, kama Sheria zina shida kwa nini hakurekebisha wakati huo? Kama ni suala la Katiba Mpya kwa nini alishiriki kuvuruga mchakato wa Katiba Mpya mwaka 2014? Nakubaliana na Marehemu Kepteni Komba huyu Mzee Warioba ni shida kubwa sana, anapaswa kuthibitiwa” ameongeza Mzee Malate
Aidha, Mzee Malate ameomba Serikali katika hali iliyopo sasa isicheke na mtu yeyote anayetaka kuvuruga amani na utulivu wa nchi kwani tunakokwenda kuna watu wanaona wamepata mwanya wa kuivuruga Tanzania na inatisha namna wanavyotumia fedha nyingi kufadhili vijana na magenge ya watu wanaochochea vurugu Tanzania.