Warioba Anamdhalilisha Nyerere!

Warioba Anamdhalilisha Nyerere!

Mkuu watu wengi wanaongeaga bila kufikiri kabisa, safi sana kwa kuweka kumbukumbu sawa!
Wewe ni Mbumbumbu kabisa...
Kama ni kumvua nguo Nyerere,CCM wenyewe ndio walianza tena kitambo tu,
1: Alipinga ubinafsishwaji wa NBC,lakini Mkapa akapitisha..
2:Alikemea Rushwa,lakini ndani ya CCM rushwa ni kama Ibada.
3: Alikemea Undugu,Ukabila na Urafiki ktk kuwapa watu Vyeo/Nyadhifa mbalimbali,lakini leo hii,Jk,Mkewe,Mtoto na Mdogo wa JK ni Wajumbe ndani ya NEC ....
Swali,Angekuepo leo hii ,yanayoendelea ndani ya CCM yangekuapo? Tembo wangefyekwa namna hii!? Madini yange sepeshwa namna hii!? Twiga wangesafirishwa namna hii!? Wawekezaji ucgwara wangeshamiri kama ilivyo sasa!?
Fikiri kabla hujaleta Uzi wako hapa ili ujizolee Umaarufu!!
 
Nimemsikia Mwenyekiti wa Tume ya Katiba Jaji Mstaafu Warioba akidai kupitia ITV leo kuwa Mwalimu Nyerere hakuwa na mawazo mgando, na kwa maana yake, anataka kuhalalisha kuwa kama angekuwepo, Mwalimu angeunga mkono mawazo yao ya kuibuka na serikali tatu.

Amedai kuwa endapo angekuwepo Mwalimu leo angekuwa amekasirika mno kutokana na Katiba iliyopo ilivyochezewa. Naweza kumuunga mkono kwa hilo lakini ni ukweli ulio wazi Mwalimu asingeunga mkono muungano wa serikali tatu kamwe!

Ni udhalilishaji mkubwa wa mtazamo wa Mwalimu kudai kuwa Mwalimu angeunga mkono serikali tatu!! Sote tulikuwa hai wakati Mwalimu alipoingilia kati, tena kwa nguvu zake zote, na kuziua juhudi za kikundi cha 45 cha kuanzisha harakati za kuunda muungano wa serikali tatu, harakati zilizokuwa tayari zimeshaungwa mkono na Mzee Malecela akiwa Waziri Mkuu na Makamu wa Kwanza wa Rais chini ya utawala wa Mzee Mwinyi na aliyekuwa Katibu Mkuu wa CCM, marehemu Horace Kolimba.

Huu anaoutangaza hivi sasa Warioba ni udhalilishaji mkubwa wa mawazo na msimamo wa Mwalimu kuhusu muungano. Ukweli ni kwamba muungano chini ya serikali tatu sio muungano.

Hauna mashiko na ni rahiusi mno kuuvunja akitokea kiongozi mkorofi kutoka upande wa Tanganyika au Zanzibar kuliko muungano katika mtindo uliopo sasa.

Na Warioba pamoja na heshima zake, asiwadhalilishe wananchi wanaopinga mawazo ya kuwa na serikali tatu kwa kuwaita ni "wenye mawazo mgando"--kama anavyoupigia yeye debe muungano wa serikali tatu pia hao wana haki ya msingi na ya kikatiba kuupinga muungano wa serikali tatu.

Akae akijua sio suala la gharama tu linalopigiwa kelele, ila ni suala la mashiko katika muungano wenyewe. Kwa mtazamo wangu anayeupigia upatu muungano wa serikali tatu, hautaki muungano!

Ukweli ni kwamba pamoja na juhudi zote hizo za kuutetea muungano wa serikali tatu, lakini Warioba hayuko wazi kuhusu ni wananchi wangapi wanaoutaka muungano huo.

In fact, katika wananchi wapatao laki 3 waliohojiwa na tume yake kutoka bara na Visiwani, ni watu wapatao 19,000 tu waliounga mkono muungano wa serikali tatu--hakuna uhalali wowote wa kimahesabu na kimantiki unaoweza kusema kwa kujiamini kuwa Watanzania sasa wanaulilia muungano wa serikali tatu.

Kwa kuanzisha muungano wa serikali tatu, ni wazi kabisa tutadhoofisha mno uzalendo wa Utanzania, ambao miaka ya hivi karibuni umeanza kuimarika sana ndani na nje ya nchi.

Hivi sasa bendera ya Tanzania inapepea katika madaladala, bodaboda, viwanjani na vitu vyenye alama ama bendera ya Tanzania vimeanza kutapakaa nje ya nchi!! Watanzania tuwe makini sana katika suala hilo--mvi sio hekima!!

Inakera kuona watu wana li- personify suala la mapendekezo ya uwepo wa serikali tatu katika katiba mpya. Jamani rasimu aliyoandaliwa na tume ya jaji warioba ni mkusanyiko wa maoni ya watu wengi zaidi waliyotoa Na si maoni binafsi ya Jaji Warioba, km ambavyo baadhi ya wahafidhina wanaotaka kupotosha umma. Na kuwa Nyerere km angekuwepo si ajabu angebadili misimamo yake mingi ili kwenda na mahitaji ya sasa, na si mahitaji ya kale.
 
wewe jaribu sana kutumia akiri zako za kuzaliwa kuliko kumfanya Nyerere kama mungu wako. jiulize kwa nini Nyerere alipounganisha Tanu na Afro Shiraz hakuuiacha afro shiraz iwe huru visiwani. Ila alipounganisha Tanganyika na Zanzibar aliiacha zanzibar ijitawale? Muungano wa serikali tatu au mbili zote ni hisia za kipuuzi tupu. Muungano ni serikali moja tuu na raisi mmoja kwisha kazi.

Jaribu kujifunza kumkosoa nyerere ili uijenge nchi! usimfanye Nyerere ni mungu wetu wala eti fikira zake ni bora kupita watanganyika wote.

Well said...a nice food for serious brains!
 
Sijui siwaelewi au vipi? jinsi wengi wetu tunavyojadili ni kama muundo wa Serikali tatu umeshapita kitu ambacho si kweli! Kuna Bunge la katiba linafuata na nafikiri mnajua nani ni wengi mle......lakini hata kama ikipita sioni Nyerere anadhalilishwaje kwani ni huyuhuyu Baba wa Taifa aliruhusu mfumo wa Vyama Vingi baada ya kusoma nyakati.....ninaamini hata kama angekuwepo sasa angesoma nyakati na kama wengi wanataka Serikali tatu sidhani kama ngekataa....sanasana angeshauri tu......ila demokrasia ndio ingetoa jibu......sio yeye.....
 
Sasa hp ndo kamdhalilisha? Udaku huo kichwa cha habar kingine ukisoma unakuta haviendan na kichwa habar,
 
So, nani kakwambia na mimi ni CCM?

Mimi ni Mtanzania ndugu. Naitetea Tanzania yangu, na wala siijui Tanganyika na wala sina hamu ya kuijua. Nimezaliwa Tanzania!! Hayo ya faida na hasara--soma tena maandishi yangu! By the way, kuwa CCM ni dhambi ila kutokuwa CCM ndio ushujaa sio?
wewe mi mtanzania bara wala sio mzanzibar,kumbuka kuna watanganyika na wazanzibari. hivyo watanzania bara ndio watanganyika,hivyo kujifanya uutaki utanganyika ni sawasawa na kumkataa baba wa babu yako
 
Nimemsikia Mwenyekiti wa Tume ya Katiba Jaji Mstaafu Warioba akidai kupitia ITV leo kuwa Mwalimu Nyerere hakuwa na mawazo mgando, na kwa maana yake, anataka kuhalalisha kuwa kama angekuwepo, Mwalimu angeunga mkono mawazo yao ya kuibuka na serikali tatu.

Amedai kuwa endapo angekuwepo Mwalimu leo angekuwa amekasirika mno kutokana na Katiba iliyopo ilivyochezewa. Naweza kumuunga mkono kwa hilo lakini ni ukweli ulio wazi Mwalimu asingeunga mkono muungano wa serikali tatu kamwe!

Ni udhalilishaji mkubwa wa mtazamo wa Mwalimu kudai kuwa Mwalimu angeunga mkono serikali tatu!! Sote tulikuwa hai wakati Mwalimu alipoingilia kati, tena kwa nguvu zake zote, na kuziua juhudi za kikundi cha 45 cha kuanzisha harakati za kuunda muungano wa serikali tatu, harakati zilizokuwa tayari zimeshaungwa mkono na Mzee Malecela akiwa Waziri Mkuu na Makamu wa Kwanza wa Rais chini ya utawala wa Mzee Mwinyi na aliyekuwa Katibu Mkuu wa CCM, marehemu Horace Kolimba.

Huu anaoutangaza hivi sasa Warioba ni udhalilishaji mkubwa wa mawazo na msimamo wa Mwalimu kuhusu muungano. Ukweli ni kwamba muungano chini ya serikali tatu sio muungano.

Hauna mashiko na ni rahiusi mno kuuvunja akitokea kiongozi mkorofi kutoka upande wa Tanganyika au Zanzibar kuliko muungano katika mtindo uliopo sasa.

Na Warioba pamoja na heshima zake, asiwadhalilishe wananchi wanaopinga mawazo ya kuwa na serikali tatu kwa kuwaita ni "wenye mawazo mgando"--kama anavyoupigia yeye debe muungano wa serikali tatu pia hao wana haki ya msingi na ya kikatiba kuupinga muungano wa serikali tatu.

Akae akijua sio suala la gharama tu linalopigiwa kelele, ila ni suala la mashiko katika muungano wenyewe. Kwa mtazamo wangu anayeupigia upatu muungano wa serikali tatu, hautaki muungano!

Ukweli ni kwamba pamoja na juhudi zote hizo za kuutetea muungano wa serikali tatu, lakini Warioba hayuko wazi kuhusu ni wananchi wangapi wanaoutaka muungano huo.

In fact, katika wananchi wapatao laki 3 waliohojiwa na tume yake kutoka bara na Visiwani, ni watu wapatao 19,000 tu waliounga mkono muungano wa serikali tatu--hakuna uhalali wowote wa kimahesabu na kimantiki unaoweza kusema kwa kujiamini kuwa Watanzania sasa wanaulilia muungano wa serikali tatu.

Kwa kuanzisha muungano wa serikali tatu, ni wazi kabisa tutadhoofisha mno uzalendo wa Utanzania, ambao miaka ya hivi karibuni umeanza kuimarika sana ndani na nje ya nchi.

Hivi sasa bendera ya Tanzania inapepea...

SIJUI NIFANYEJE WATU Waelewe juu ya Ubaya wa Serikali tatu hasa sie wa Bara, Gharama za kuihudumia hiyo serikali ya 3 Zanz wanauwezo?Nani mwenye nguvu zaidi kwenye Serikali hizo, Tanganyika au Tanzania? Bunge la Tanganyika nalo litaundwa je tupo tayari kubeba gharama? Gharama tena za Katiba ya Tanganyika tupo tayari kuzibeba? Maraisi kibao na viongozi wastaafu kuhudumiwa hadi kufa tupo tayari? Je, tupo tayari kulipa kodi MARA 3 ili kujenga nchi kwa nguvu zetu chininya serikali hizo? Nani mwenye mamlaka ikiwa kuna tatizo upande wa muungano mmoja hasa Tanganyika.Je Zanzibar wakigawanyika na ndipo wanachotaka kuwa Pemba na Zanz tumejiandaa kuwa na SERIKALI NNE?Tunajiunga kuwa jumuia ya EAC, ambapo tunaelekea kuwa na sarafu moja na Rais mmoja, je Kuigawa nchi tutaingia Muungano huu kwa nguvu.MIMI NAWAASA WATANZANIA WOTE...TUSIPOTOSHWE TUSIWAPE NAFASI MTU KUJITENGENEZEA SIFA KUTUMIA LEGACY YA NYERERE, KUONYESHA YA NYERERE ILISHINDWA.TANZANIA NI MOJA WOTE NI WAMOJA NA SERIKALI NI MBILI ILI ZANZIBA WAJUE KUWA WAPO HURU KWA MASWALA FULANI..TUWE WAZALENDO SIO KUFIKIRIA...NITAPATAJE URAIS...KUPITIA CHAMA CHANGU..HASA UPINZANI...HILI SWALA TULIJADILI KWA NGUVU ZOTE, KWA kina.

Huu ni ujanja ujanja uliyopitwa na wakati.Mbona kwenye serekali ya maridhiano kati ya CUF na CCM hizo gharama hazikusemwa.Katika maridhiano hayo walikubaliana kuwa kuwepo na nafasi ya makamu wa Rais wa Zanzibar nafasi ambayo haikuwepo hapo awali na hiyo nafasi ilitakiwa wapewe watu wa CUF.CCM walipo kugunduwa kuwa hiyo nafasi wao hawatakuwemo ili na wao wawemo kwenye nafasi hiyo walilweza kulazamisha kuwepo makamu 2 wa Rais wa kwanza na wapili ili mradi tu na wao wawemo kwenye nafasi hiyo kitu ambacho ilikuwa ni kuongeza gharama kwa kuwa hudumia makamu 2 wa Rais.Gharama zinakuja kuibuka na kusemwa linapokuja swala la serekali 3 na uwepo wa Tanganyika Kitu ambacho si kweli kwamba uwepo wa serekali 3 pamoja na Tanganyika eti vitasababisha gharama za uendeshaji wakati hakuna kitu kikubwa ambacho kitaongezwa kwenye serekali.Kwani kitu ambacho kinaweza kurudishwa ni Tanganyika ambayo ili kuwepo hapo awali Rais wa Tanganyika ambae alikuwepo hapo awali ikishindikana serekali ya Tanganyika inaweza kuongozwa na wazri mkuu ambae mpaka sasa tunaye.Wizara za Tanganyika ni zile ambazo haziko chini ya muungano pamoja na mawaziri wake.Gharama zitakazotumika ni zilezile zinazotumika kugharamia wizara zisizo za muungano na mawazri wake.Wabunge wote waliyopo bara watakuwa wabunge wa Tanganyika na watashughulika na wizara zote ambazo siyo za muungano kwa kutumia gharama zilezile zinazotumika hivi sasa pasipo kuongeza hata senti tano.Wizara zote ambazo siyo za muungano zitaendelea kuwepo chini ya Rais wa Jamhuri ya muungano kama ilivyo hivi sasa.wizara za muungano zitaendelea kuwa zilezile na mawaziri idadi ileile ya kulingana na wizara zilizopo na gharama ndiyo zilezile zinazotumika kwenye wizara hizo hivi sasa.Wabunge wa Zanzibar watakuja kuungana na wenzao wa Tanganyika siku ya kuja kujadili mambo yanayo husu muungano na wizara zake na si vinginevyo.
 
Mkuu hongera sana kwa kuwapa za uso. Mawaziri na Wizara ambazo siyo za Muungano automatically zitakua chini ya serikali ya Tanganyika. Serikali ya Muungano itaendelea kutekeleza majukumu yake kwa mambo ya Muungano. Hata Bunge la Jamhuri ya Muungano litakua ni dogo!

Jiulize ni gharama kiasi gani kwa mwaka tunatumia kuwahudumia wabunge toka Zanzibar waliopo ktk Bunge la JMT ambao kwa kipindi kirefu hawana hoja za kuchangia kwasababu shughuli nyingi za Bunge zinahusu maendeleo na wizara za Watanganyika!!

Kiasi gani tunatumia kuhudumia Viti Maalumu wakati tija yake ni ndogo sana!! Gharama kiasi gani Tanganyika kws kivuli cha JMT inabeba kuwahudumia na kuwalea hawa walalamishi? Watajifunza kujitegemea baada ya Tanganyika kuwepo!
 
Huu ni ujanja ujanja uliyopitwa na wakati.Mbona kwenye serekali ya maridhiano kati ya CUF na CCM hizo gharama hazikusemwa.Katika maridhiano hayo walikubaliana kuwa kuwepo na nafasi ya makamu wa Rais wa Zanzibar nafasi ambayo haikuwepo hapo awali na hiyo nafasi ilitakiwa wapewe watu wa CUF.CCM walipo kugunduwa kuwa hiyo nafasi wao hawatakuwemo ili na wao wawemo kwenye nafasi hiyo walilweza kulazamisha kuwepo makamu 2 wa Rais wa kwanza na wapili ili mradi tu na wao wawemo kwenye nafasi hiyo kitu ambacho ilikuwa ni kuongeza gharama kwa kuwa hudumia makamu 2 wa Rais.Gharama zinakuja kuibuka na kusemwa linapokuja swala la serekali 3 na uwepo wa Tanganyika Kitu ambacho si kweli .................
Mkuu, tena iligeuzwa kuwa makamu wa pili wa Rais ndio atakuwa msimamizi wa shughuri zote za Baraza la Wawakilishi badala ya Waziri Kiongozi kwa kuwa huyu na Rais ni wa CCM.
 
Wadanganyika mmekuwa mnapiga makelele sana lakini hamfahamiki,hizi ni nchi 2 huru,hamuwezi kuifuta zanzibr kwa koti la muungano hata nyerere imemshinda,zanzibar bado inapumua na itaendelea kupumua,kama mliifuta tanganyika ni kwa uzembe wenu,wenyewe kama hamuitaki tanganyika yenu ndio sisi tunakuja kuchukua ardhi,ajira na rasilimali,kama muungano mnaupenda kaunganeni na congo,zanzibar kwanza.
 
Nyerere asingeweza kugeuka mnara wa chumvi! Mwalimu alikuwa wazi na mawazo yake aliandika kwenye kitabu chake cha Uongozi wetu na Hatima ya Tanzania. Tusome. Tumuache apumzike wala tusifanye maamuzi mabovu kisha tuyahalalishe kwa kumhusisha marehemu.
Hii ni kwa ufahamisho tu kwa malimbukeni wasivyojua historia ya nchi hii kama wewe Alex Manonga...hebu nipe jibu moja tu. Bila shaka unajua kuwa ni Mwalimu ndiye kwa nguvu ya hoja alipinga mfumo wa vyama vingi na kuanzisha mfumo wa chama kimoja na chama kushika hatamu...je unajua kuwa ni Mwalimu huyo huyo alikuja kupingana na msimamo wa CCM kuhusu kuanzishwa tena kwa mfumo wa vyama vingi miaka thelathini baadaye? Wakati Raisi Ali Hasan Mwinyi na Waziri Mkuu John Samwel Malecela wakiwa wamejizatiti kuupinga upepo wa mageuzi ni Mwalimu Nyerere alieyewakemea akisema ni lazima tujifunze kwenda na wakati. Je hapo Mwalimu alimdhalilisha Mwalimu? Aligeuka mnara wa chumvi? Acheni kukurupuka na madai ya kipuuzi, Mwalimu alienda na wakati.
 
Nawewe ni miongoni mwa wenye mawazo mgando,serikali tatu ni lazima hata kama Nyerere angekuwepo .Mbona alikubali vyama vingi

Back
Top Bottom