Warioba Anamdhalilisha Nyerere!

Warioba Anamdhalilisha Nyerere!

Mkuu haya ni mawazo yako,yaheshimiwe,pia nawe yaheshimu mawazo ya mzee Walioba na wenzake.
Kusema alichokisema siyo kumdhalilisha Mwalimu.hebu tuangalie mwalimu alipokuwa hai,alipinga kuvunjwa kwa azio la Arusha,alipinga kuuzwa kwa benki ya taifa ya biashara (NBC),lakini yalifanyika mbele ya macho yake na siyo mbele ya kaburi lake,je hapo hakuvunjiwa heshima? Leo hii tumeshuhudia Walioba na wenzake wa tume ya katiba wakipendekeza maadili ya viongozi kama sehemu ya kurejesha nidhamu ktk uongozi ambalo ni mojawapo ya mambo muhimu ktkt azimio la Arusha,mbona hapo hujawapongeza?
Ikumbukwe kwamba Tume ya katiba wamejaribu kutatua tatizo la kero za muungano,kero hizo haziko kwa wazanzibar peke yao ni pamoja na kwa wabara,kuona jina la nchi yao linamezwa na muungano huku nchi ya zanzibar ikiendelea kutajwa kwenye katiba ya muungano.
Kama tujuavyo nchi za Tanganyika na Zanzibr ziliungana kuzaa TANZAN-IA
TAN-Tanganyika
ZAN-Zanzibar
I-Iqbar-Jina la aliyetunga jina la Tanzania
A-Ahamadiya-Dini yake
Kwenye ufafanuzi wa serikali mbili kuna tanzania bara na Zanzibar,ni lini iliwahi kuwepo nchi inayoitwa Tanzania bara
hasa ukiangalia majina yaliyotajwa hapo juu.
Mwalimu Nyerere aliwahi kusema "ktk serikali yangu nilifanya mambo mazuri na mambo ya kijinga,nashanga wanafuta mazuri wanashika ya kijinga"
Mimi nadhani mojawapo ya mambo ya kijinga aliyoyasema ni hili la Tanganyika kuitwa tanzania bara na tunalipigania hili la kijinga tunaacha jema la maadili ya viongozi lililodidimiza utu wa mtanzania.
Naipongeza tume ya katiba kwa kufuta ya kijinga tuliyoyashika muda mrefu na kurejesha mambo mema kwa faida ya watanzania wote.
 
Mleta mada umepatia sana. Mungu akubariki. Jaji warioba nampenda, lakini kwa serikali tatu kaweka utashi wake. Njelu kasaka, muumini wa serikali tatu hakubaliani naye. Stay tune! Tanzania yangu maskini inakufa
. Tutaipigania hadi mwisho.
Mkuu, amepatia au amekufarahisha tusubiri kura ya maoni watakae amua kama kuzikubali serikali tatu au kuzikataa.
 
Manyerere tusonge mbele, achana na akina Njelu kasaka, mawazo yako yatakua wapi? Njelu alishindwa baada ya kupewa ulaji...........nadhani tuje na hoja nzito zenye uchambuzi jadidifu kwa kuangalia uchambuzi, matakwa ya wengi na hali halisi ya sasa badala ya kuegemea wazee
Mleta mada umepatia sana. Mungu akubariki. Jaji warioba nampenda, lakini kwa serikali tatu kaweka utashi wake. Njelu kasaka, muumini wa serikali tatu hakubaliani naye. Stay tune! Tanzania yangu maskini inakufa
. Tutaipigania hadi mwisho.
 
Endapo utaona vyema message yangu, nimeunga mkono la kuchezewa kwa katiba iliyopo--na hasa upande wa Zanzibar--ila kama ilivyokuwa kwa Mwalimu--siamini kabisa kwamba solution ni serikali tatu. Mbona suala hilo liliibuliwa wakati Mwalimu akiwa hai, tena kwa hoja hizo hizo za kuchezewa kwa katiba, hasa upande wa Zanzibar na kwa kutumia uwezo wake kama Jeshi la Mtu Mmoja akaiua hoja ya serikali tatu iliyokuwa ikiasisiwa na akina Njelu Kasaka na kundi lao la watu 45? Tuzungumze tatizo halisi hapa badala ya kulikwepa! Kama viongozi wetu wameshindwa kumfunga paka kengele, naamini Watanzania wa kweli watamfunga katika kura ya maoni ijayo!! Na pia naamini iko siku ataibuka kiongozi Mtanzania atakayemdhibiti vyema 'paka' asiichezee katiba ya TANZANIA.
Mzee warioba unataka tuamini kwamba tiba ya kuchezea katiba ni kuanzisha serikali tatu na unadhani hiyo ndiyo sababu ya kuwa na serikali tatu. Je na hiyo pia ikisiginwa kama ulivyo sema suluu itakuwa serikali ngapi wazo zaifu kwa hoja nzito.
 
Hakuna sehemu yoyote niliyosema ww ni ccm bali nimesema wanaopinga serikali 3 ni ccm, na kwa jibu lako hapa huna haja ya kusema ww ni mtanzania wala mtanganyika bali ni ccm damu na kuwa ccm sio dhambi mkuu bali mmedumazwa na mfumo hamfikirii nje ya box.
Tume ya jaji warioba ilitumia kodi zetu kuzunguka karibia tz nzima na huo ndiyo msimamo wa watanzania wote bila kujali itikadi zetu,so hatuna budi kuyapokea mawazo ya watanzania wengi,na kama ilivyo ada wengi wasikilize wachche wape,mkicheza karata zenu vzr mnaweza fanikiwa hizo serikali 2

Mtoa mada ana hoja. Umesema CCM ndio inapinga serikali tatu? Ukasema serikali tatu ni msimamo wa watanzania walio wengi? Wangapi, 300,000 waliotoa maoni? Kama uhalali ni namba, na kama unakubali kuwa msimamo wa serikali 2 ni wa wana CCM basi CCM inawakilisha mawazo ya watanzania waliowengi kwa kuwa CCM ina zaidi ya wanachama milioni tano. Hata hivyo nakubaliana na wanaosema Muungano wetu ungeimarika zaidi tukielekea serikali moja japo kwa uhalisia wa siasa zetu za sasa kusema hivyo ni sawa na kuzungumzia Azimio la Arusha.
 
wewe jaribu sana kutumia akiri zako za kuzaliwa kuliko kumfanya Nyerere kama mungu wako. jiulize kwa nini Nyerere alipounganisha Tanu na Afro Shiraz hakuuiacha afro shiraz iwe huru visiwani. Ila alipounganisha Tanganyika na Zanzibar aliiacha zanzibar ijitawale? Muungano wa serikali tatu au mbili zote ni hisia za kipuuzi tupu. Muungano ni serikali moja tuu na raisi mmoja kwisha kazi.

Jaribu kujifunza kumkosoa nyerere ili uijenge nchi! usimfanye Nyerere ni mungu wetu wala eti fikira zake ni bora kupita watanganyika wote.

Kajifunze Kiswahili kwanza ndipo ujitokeze katika majukwaa kama haya--hakuna neno "akiri" kwa maana ya neno, kama ulivyolitumia hapo!! Kwangu mimi, kosa hili linaua hoja zako za msingi ndugu!
 
Mkuu haya ni mawazo yako,yaheshimiwe,pia nawe yaheshimu mawazo ya mzee Walioba na wenzake.
Kusema alichokisema siyo kumdhalilisha Mwalimu.hebu tuangalie mwalimu alipokuwa hai,alipinga kuvunjwa kwa azio la Arusha,alipinga kuuzwa kwa benki ya taifa ya biashara (NBC),lakini yalifanyika mbele ya macho yake na siyo mbele ya kaburi lake,je hapo hakuvunjiwa heshima? Leo hii tumeshuhudia Walioba na wenzake wa tume ya katiba wakipendekeza maadili ya viongozi kama sehemu ya kurejesha nidhamu ktk uongozi ambalo ni mojawapo ya mambo muhimu ktkt azimio la Arusha,mbona hapo hujawapongeza?
Ikumbukwe kwamba Tume ya katiba wamejaribu kutatua tatizo la kero za muungano,kero hizo haziko kwa wazanzibar peke yao ni pamoja na kwa wabara,kuona jina la nchi yao linamezwa na muungano huku nchi ya zanzibar ikiendelea kutajwa kwenye katiba ya muungano.
Kama tujuavyo nchi za Tanganyika na Zanzibr ziliungana kuzaa TANZAN-IA
TAN-Tanganyika
ZAN-Zanzibar
I-Iqbar-Jina la aliyetunga jina la Tanzania
A-Ahamadiya-Dini yake
Kwenye ufafanuzi wa serikali mbili kuna tanzania bara na Zanzibar,ni lini iliwahi kuwepo nchi inayoitwa Tanzania bara
hasa ukiangalia majina yaliyotajwa hapo juu.
Mwalimu Nyerere aliwahi kusema "ktk serikali yangu nilifanya mambo mazuri na mambo ya kijinga,nashanga wanafuta mazuri wanashika ya kijinga"
Mimi nadhani mojawapo ya mambo ya kijinga aliyoyasema ni hili la Tanganyika kuitwa tanzania bara na tunalipigania hili la kijinga tunaacha jema la maadili ya viongozi lililodidimiza utu wa mtanzania.
Naipongeza tume ya katiba kwa kufuta ya kijinga tuliyoyashika muda mrefu na kurejesha mambo mema kwa faida ya watanzania wote.
Kama kila hawamu itakayo chezea katiba ambayo ilihapa kuilinda suluisho litakuwa serikali tatu mimi nadhani ni wazo zaifu kwa hoja nzito.suluisho la kusiginwa kwa katiba ni kuwafikisha mahakani walio hapa kuilinda na siiwazo zaifu la mzee warioba.nyerere ilikuwa mashine ilikuwa aibahatishi jambo subili matokeo ya huo ujinga utakuwa ujanja.
 
Kukurekebisha ww mzee wa kucopy vibaya na kupaste lile kundi ni G 55 acha hiyo tabia kila jambo la nyerere kwako ww la kuiga wakati yeye mwenyewe alishawai kusema wamefanya mema na wamefanya ya kijinga moja wapo la kijinga hlo kutu ulia tanganyika yetu mwingereza alimkabidhi nchi inayoitwa tanganyika yeye akaiua wake up wewe.
 
Siku zote kikwete hafanani na hao ccm katika maamuzi yake siunakumbuka ya serikali ya umoja wa kitaifa, kwa hili serikali tatu ndio litapita lakini naomba unijuze kwanini sisi wabara tunaing'an'gania zanzibar? Tunafaidika na nini na tuna the best army na strategic areas za kuweka kambi za jeshi

Which best army are talking about? Does Tanganyika have an army? You think building an air force and the navy to secure our coast is less costly than the cost of maintaining the union? Siamini!
 
nasema hivi..

SERIKALI 3=KUVUNJA MUUNGANO..
sasa kwanin wasiuvunje moja kwa moja had waanze kuptia huko.?
 
Kajifunze Kiswahili kwanza ndipo ujitokeze katika majukwaa kama haya--hakuna neno "akiri" kwa maana ya neno, kama ulivyolitumia hapo!! Kwangu mimi, kosa hili linaua hoja zako za msingi ndugu!
Ukitaka mtu akuheshimu nawe heshimu watu wanae muheshimu ukimzalau watu wanae muheshimu hapo ndipo utajuwa nguvu ya wale wengi wanaomuheshimu.kudhani kwamba kupinga mawazo ya mtu kunathibitisha ubola wako sii kweli.nyumba ya chini na ya gorofa kimtizamo zote nyumba tu kivipimo gorofa ni gorofa tu.nyerere ni nyerere tu itabaki kuwa hivyo.fikta zake ni gorofa sii nyumba ya chini.
 
Mara yoyote unaposikia mtu anadai anajua marehemu angefanya nini kama angekuwepo, hususan kama marehemu amefariki kitambo na ni mtu complex kama Nyerere, chunguza sana hiyo kauli.

I mean unajuaje jinsi mambo yooote yaliyotokea baada ya kufariki Nyerere yangemu influence vipi Nyerere na mawazo yake?

Kusema unamjua mtu kiasi hicho ni kumfanya awe an automaton. Kwamba alikuwa anafikiri katika namna ambayo inaweza kutabirika.

Warioba mzee wangu, lakini, kwa kusema Nyerere hakuwa na mawazo mgando na angekuwepo leo angefikiri hivi, ukiangalia kiundani ni kusema kwamba Nyerere alikuwa na mawazo mgando kiasi kwamba hata baada ya kututoka miaka yote hii, tunaweza kuchukua a few factors, tukazichanganya katika a simulated head of Nyerere, na tukajua angewaza nini.

Kama hoja ina nguvu, tuitetee tu, nguvu ya hoja itaonekana.

Nyerere hatunaye, na wala si haki kutaka tuwe naye na kuanza kujiuliza angefikiri nini, hatutamtendea haki.
 
nasema hivi..

SERIKALI 3=KUVUNJA MUUNGANO..
sasa kwanin wasiuvunje moja kwa moja had waanze kuptia huko.?

Uko sahihi. Nilisema juzi nilipokuwa najadili Katiba Mpya TBC, serikali tatu ni njia ya kuvunja Muungano kistaarabu. Hizi siasa za kuviziana kila upande kukwepa lawama hazina maana.
 
Mara yoyote unaposikia mtu anadai anajua marehemu angefanya nini kama angekuwepo, hususan kama marehemu amefariki kitambo na ni mtu complex kama Nyerere, chunguza sana hiyo kauli.

I mean unajuaje jinsi mambo yooote yaliyotokea baada ya kufariki Nyerere yangemu influence vipi Nyerere na mawazo yake?

Kusema unamjua mtu kiasi hicho ni kumfanya awe an automaton. Kwamba alikuwa anafikiri katika namna ambayo inaweza kutabirika.

Warioba mzee wangu, lakini, kwa kusema Nyerere hakuwa na mawazo mgando na angekuwepo leo angefikiri hivi, ukiangalia kiundani ni kusema kwamba Nyerere alikuwa na mawazo mgando kiasi kwamba hata baada ya kututoka miaka yote hii, tunaweza kuchukua a few factors, tukazichanganya katika a simulated head of Nyerere, na tukajua angewaza nini.

Kama hoja ina nguvu, tuitetee tu, nguvu ya hoja itaonekana.

Nyerere hatunaye, na wala si haki kutaka tuwe naye na kuanza kujiuliza angefikiri nini, hatutamtendea haki.

Nyerere asingeweza kugeuka mnara wa chumvi! Mwalimu alikuwa wazi na mawazo yake aliandika kwenye kitabu chake cha Uongozi wetu na Hatima ya Tanzania. Tusome. Tumuache apumzike wala tusifanye maamuzi mabovu kisha tuyahalalishe kwa kumhusisha marehemu.
 
Ukweli ni kwamba huo ndio msimamo wa Watanzania wengi, mimi nikiwemo. Ila sote twajua kuwa hilo halikuwepo tangu day one ya kuundwa kwa muungano na limeendelea kupingwa, hasa na Wazanzibar kwa kuogopa kumezwa. Muungano wa serikali mbili tumekuwa nao kwa miaka 50 na wengi wetu tumezaliwa Watanzania na tumeishi ndani ya Tanzania kwa miaka yote hiyo 50--waswahili wanasema heri zimwi likujualo! hatupingi kubadili au kuandika katiba mpya, lakini tunapinga mabadiliko for the sake of mabadiliko--tunataka mabadiliko yenye tija sio yatakayovunja nchi tuliyozaliwa na kuipigania kwa miaka 50!!

Ndugu utapata pressure bure kushikilia kuitwa Mtanzania wakati moja ya mshirika hataki kuendelea kuwemo ktk muungano. Anza taratibu kujizoeza kuitwa Mtanganyika. Sisi siyo wa kwanza na hatutakua wa mwisho kutengana na kuishi kama mataifa mawili rafiki.

Sitarajii utafurahia wazalendo wa nchi ya Zanzibar kwa kutambua kwamba hawawezi pigana vita ya moja kwa moja na sisi,wataanzisha hujuma za kihalifu kwa kujilipua na kuua Watanganyika kwa sababu ya kutafuta uhuru wa pili wa taifa lao!!

Hakuna sababu ya kuwalazimisha ktk muungano wa serikali moja,serikali mbili bado hawazitaki licha ya kufaidika kwa kiasi kikubwa na ajira,elimu,ardhi,uchumi na biashara. Njia iliyobaki ni serikali 3. Kama hawataki watimue.
 
Uko right kabisa mkuu,kikwete kapigana na mawazo mengi sana ya wanaccm wenzake,tutamkumbuka kwa machache yake.
Navyojua mimi tanganyika inajitosheleza kwa kila kitu na sababu kubwa za kuing'ang'ania zanzibar ni sababu za kiusalama tu plus uwepo wa gesi na mafuta ila tofauti na hapo hatuna tunachokipata wala kufaidika na zenji,labda wakuu wa nchi wanasababu zao za msingi ambazo wananchi wa kawaida hatuzijui.

You people are misunderstanding the president. Kama rais Kikwete anasimamia huu mchakato kwa msimamo wa kitaifa, hakutaka imani ya chama chake ibebe mawazo ya watanzania-which is the best democratic practice. Akirudi kwenye chama kama mwenyekiti bado atasimama kwa mtizamo wa chama unless CCM kama taasisi kibadili sera.
 
Nyerere asingeweza kugeuka mnara wa chumvi! Mwalimu alikuwa wazi na mawazo yake aliandika kwenye kitabu chake cha Uongozi wetu na Hatima ya Tanzania. Tusome. Tumuache apumzike wala tusifanye maamuzi mabovu kisha tuyahalalishe kwa kumhusisha marehemu.

Nyerere mwenyewe kashasema kwamba yeye anabadilika kutokana na mazingira, kwa hiyo kusema "asingeweza kugeuka mnara wa chumvi" kwa maana ya kubadili msimamo ni kutomjua Nyerere.

Nyerere alikuwa muasisi wa TANU na CCM, na kama angefariki kabla ya kusema "CCM si mama yangu" kwa kumaanisha kwamba siku moja CCM inaweza kuchemka sana akaihama, mtu yeyote angeniambia kwamba Nyerere angekuja kusema hivyo ningemuona anamzushia mzee wa watu.

Lakini ina speech of unpredictable courage, alijisemea mwenyewe kwamba yeye ana principles zake za msingi kabisa, na moja ya principle hizi ni kuweza kubadilika na nyakati. Kiasi kwamba, inawezekana kabisa siku moja CCM ikabadilika kwenda asikokutaka, akarudisha kadi.

Huyu si mtu ambaye unaweza kusema kirahisirahisi tu, baada ya miaka yote hii kufariki, baada ya siasa za nchi yetu na za dunia kubadilika sana, kwamba angewaza hivi au vile leo hii.

Hiyo itakuwa ni speculation tu.

Unaweza kuniambia Nyerere alisema na kufanya nini 1999 na nyuma, lakini unapojaribu kutaka kuniambia Nyerere angesema nini leo unaniambia kwamba huelewi jinsi Nyerere alivyokuwa complex, multifaceted na nuanced.

Respect the man for a min, and don't ride on his coattail for political currency.It is low and unworthy of the services he rendered this nation, not to say that he was flawless or anything, but still.

Kaangalie speech ya Nyerere aliyoitoa mara ya pili bunge la Africa kusini, mzee anakuchota kwanza kwa kuponda kwa nini akienda ulaya wazungu wanamuuliza matatizo ya Rwanda na Burundi wakati yeye si mtu wa huko, kwamba mbona wanataka kuifanya Afrika kama nchi moja? Hawaheshimu sovereign states? He has an argument there. Amepigania uhuru Tanganyika na na kuiunda Tanzania.

Halafu anapiga 180 turn na kusema it's OK, kwani hivi vi nchi vya Kiafrika ni creatiojns za jana tu, hata yeye katengeneza moja, so the underlying Pan African appearance cannot be uderrated.

Watu weeee.

I mean this is not a simple guy kwamba useme unajua chochote anachotaka kusema hata enzi zile alivyokuwepo hai.

Iweje leozaidi ya miaka 13 tangu afe watu fulani wajifanye wanajua angetaka kusema nini?

Pengine mwenzenu angeenda kwenye paradigm shift nyingine kabisa inayo reject totally the entire Westphallian model that has wrecked havoc on this planet even since the Europen princelings embarked on "The Thirty Years War"!
 
Si haki kumshutumu Warioba mkuu kwa sababu kuu mbili: Kwanza yeye amewakilisha kazi iliyofanywa na tume nzima kwa niaba ya wenzake kama Mwenyekiti, pili hayo anayoyasema si ya kwake wala ya tume bali ni mapendekezo ya watanzania zaidi ya 64% hivyo alivyosema hata hatati Nyerere angeafiki ana maana kwamba asingepinga mawazo ya watanzania wengi kwani si ndiyo demakrasia ambayo Nyerere alikuwa muumimi wake?? Ni sawa na kuwaambia wananchi wapige kura kumchagua rais wao wanayemkubali then akipatikana useme huyu hapana!! Pia ufahamu kwamba wanaopinga serikali 3, kama wewe wapo ila hawakuwashinda wale wanaotaka serikali 3 na demokrasia inasema wengi wape.
 
Nyerere mwenyewe kashasema kwamba yeye anabadilika kutokana na mazingira, kwa hiyo kusema "asingeweza kugeuka mnara wa chumvi" kwa maana ya kubadili msimamo ni kutomjua Nyerere.

Nyerere alikuwa muasisi wa TANU na CCM, na kama angefariki kabla ya kusema "CCM si mama yangu" kwa kumaanisha kwamba siku moja CCM inaweza kuchemka sana akaihama, mtu yeyote angeniambia kwamba Nyerere angekuja kusema hivyo ningemuona anamzushia mzee wa watu.

Lakini ina speech of unpredictable courage, alijisemea mwenyewe kwamba yeye ana principles zake za msingi kabisa, na moja ya principle hizi ni kuweza kubadilika na nyakati. Kiasi kwamba, inawezekana kabisa siku moja CCM ikabadilika kwenda asikokutaka, akarudisha kadi.

Huyu si mtu ambaye unaweza kusema kirahisirahisi tu, baada ya miaka yote hii kufariki, baada ya siasa za nchi yetu na za dunia kubadilika sana, kwamba angewaza hivi au vile leo hii.

Hiyo itakuwa ni speculation tu.

Unaweza kuniambia Nyerere alisema na kufanya nini 1999 na nyuma, lakini unapojaribu kutaka kuniambia Nyerere angesema nini leo unaniambia kwamba huelewi jinsi Nyerere alivyokuwa complex, multifaceted na nuanced.

Respect the man for a min, and don't ride on his coattail for political currency.It is low and unworthy of the services he rendered this nation, not to say that he was flawless or anything, but still.

Kaangalie speech ya Nyerere aliyoitoa mara ya pili bunge la Africa kusini, mzee anakuchota kwanza kwa kuponda kwa nini akienda ulaya wazungu wanamuuliza matatizo ya Rwanda na Burundi wakati yeye si mtu wa huko, kwamba mbona wanataka kuifanya Afrika kama nchi moja? Hawaheshimu sovereign states? He has an argument there. Amepigania uhuru Tanganyika na na kuiunda Tanzania.

Halafu anapiga 180 turn na kusema it's OK, kwani hivi vi nchi vya Kiafrika ni creatiojns za jana tu, hata yeye katengeneza moja, so the underlying Pan African appearance cannot be uderrated.

Watu weeee.

I mean this is not a simple guy kwamba useme unajua chochote anachotaka kusema hata enzi zile alivyokuwepo hai.

Iweje leozaidi ya miaka 13 tangu afe watu fulani wajifanye wanajua angetaka kusema nini?

Pengine mwenzenu angeenda kwenye paradigm shift nyingine kabisa inayo reject totally the entire Westphallian model that has wrecked havoc on this planet even since the Europen princelings embarked on "The Thirty Years War"!

Katika hiyo hotuba alioitoa kwenye bunge la Afrika Kusini mwaka 1997, Mwalimu alikuwa anajenga hoja juu ya Umajumui wa Afrika ( Pan Africanism) kwa kuwaambia kama wazungu wanatuona sisi kama waafrika kwa nini sisi tuone fahari kwa kujitambulisha na viinchi vilivyotengenezwa na wakoloni kwa kubuni michoro katika ramani ya Afrika, na yeye kama unavyosema akatengeneza moja ( Tanzania). Kwa Nyerere aliyekuwa muumini wa Umajumui wa Afrika asingekubali kuona Tanzania ikifa kwa jina la serikali tatu.
 
Hata mimi namshangaa Warioba kazi yake amemaliza kama anaamini hayo waliyoandika kwenye rasimu ya katiba kwanini anahangaika kuyatetea halafu Nyerere asingeunga mkono serikali tatu bali angehakikisha wale wote waliovunja katiba wanachukuliwa hatua kwa mtindo huu wa kuangaliana bila kuchukua hatua ni wazi hata hiyo katiba tunayoandaa haitakuwa na maana amezungumzia gharama za kuendesha serikali ya muungano kijuu juu yeye anakula mafao yake ya uwaziri mkuu hatachangia popote ila wanaochangia ndio wataumia
Mwisho kama kweli alitaka wananchi wafanye maamuzi angewaacha wachague aina ya muungano wanaoutaka kama serikali moja,serikali mbili,serikali tatu,serikali nne,mkataba au wananchi hawataki kabisa muungano na sio kulazimisha mawazo yake kuwa ndio sahihi na wengine wanaopinga hawako sahihi
 
Back
Top Bottom