Warioba Anamdhalilisha Nyerere!

Warioba Anamdhalilisha Nyerere!

Mkuu haya ni mawazo yako,yaheshimiwe,pia nawe yaheshimu mawazo ya mzee Walioba na wenzake.
Kusema alichokisema siyo kumdhalilisha Mwalimu.hebu tuangalie mwalimu alipokuwa hai,alipinga kuvunjwa kwa azio la Arusha,alipinga kuuzwa kwa benki ya taifa ya biashara (NBC),lakini yalifanyika mbele ya macho yake na siyo mbele ya kaburi lake,je hapo hakuvunjiwa heshima? Leo hii tumeshuhudia Walioba na wenzake wa tume ya katiba wakipendekeza maadili ya viongozi kama sehemu ya kurejesha nidhamu ktk uongozi ambalo ni mojawapo ya mambo muhimu ktkt azimio la Arusha,mbona hapo hujawapongeza?
Ikumbukwe kwamba Tume ya katiba wamejaribu kutatua tatizo la kero za muungano,kero hizo haziko kwa wazanzibar peke yao ni pamoja na kwa wabara,kuona jina la nchi yao linamezwa na muungano huku nchi ya zanzibar ikiendelea kutajwa kwenye katiba ya muungano.
Kama tujuavyo nchi za Tanganyika na Zanzibr ziliungana kuzaa TANZAN-IA
TAN-Tanganyika
ZAN-Zanzibar
I-Iqbar-Jina la aliyetunga jina la Tanzania
A-Ahamadiya-Dini yake
Kwenye ufafanuzi wa serikali mbili kuna tanzania bara na Zanzibar,ni lini iliwahi kuwepo nchi inayoitwa Tanzania bara
hasa ukiangalia majina yaliyotajwa hapo juu.
Mwalimu Nyerere aliwahi kusema "ktk serikali yangu nilifanya mambo mazuri na mambo ya kijinga,nashanga wanafuta mazuri wanashika ya kijinga"
Mimi nadhani mojawapo ya mambo ya kijinga aliyoyasema ni hili la Tanganyika kuitwa tanzania bara na tunalipigania hili la kijinga tunaacha jema la maadili ya viongozi lililodidimiza utu wa mtanzania.
Naipongeza tume ya katiba kwa kufuta ya kijinga tuliyoyashika muda mrefu na kurejesha mambo mema kwa faida ya watanzania wote.

-ia | Define -ia at Dictionary.com
[h=2]-ia[/h]
a noun suffix having restricted application in various fields, as in names of diseases ( malaria; anemia ), place names ( Italia; Romania ), names of Roman feasts ( Lupercalia ), Latin or Latinizing plurals ( Amphibia; insignia; Reptilia ), and in other loanwords from Latin ( militia ).



Origin:
< Neo-Latin, Latin, Greek, equivalent to -i- (formative or connective) or -&#299;- ( Greek -ei- ) + -a, feminine singular or neuter plural noun or adj. ending
 
viongozi si viongozi wa kufikiria kufanya mambo magumu, mi nilitegemea mchakatonwa katiba ungekuwa ndio mwanzonwa kuivunja zanzibar tupate muungano wa kweli yani Tanzania, ndio kwanza nikasikia mapendekezo ya serikali tatu, kweli uzee na mvi si busara, tunahitaji watu wenye fikra ngumu na maamuzi magumu, warioba na wenzake wamechagua njia rahisi ki mtazamo lakini kiuhalisia ni ngumu sana,
kuundwa kwa serikali moja ya muungano ndio suluhisho pekee la matatizo hapa tanzania, tunapaswa kuusahau uzanzibar na utanganyika, watanganyika wanapaswa kupongezwa kwa uvumilivu kwa miaka mingi, zanzibar ubinafsi ndio unaoleta shida katika muungano, wao ndio wangepaswa kuwa wakwanza kutetea kuundwa kwa serikali moja, sikuzote wamekuwa wakipiga kelele bila kuwa na mwelekeo watu wa kulalamika bila kujua
 
K-Boko Badilika usipokuwa makini uatalaumu kila kitu kuwa Mwalimu alisema hivi na vile,hata matatizo ya ndoa kati ya babako na mamako utasingizia Mwalimu alisema!!
 
Heshimu/pitia majority opinions ya washirika wa muungano na watu wake kuhusu mchakato wa katiba mpya! b4 hujaibuka na jazba na mtazamo wa kibnafsi!
mwenyekiti(warioba)kaongea hilo kwa kutazama alama za nyakati na kufanya obvious reasoning with due respect to the ancestors of TANZANIA!
kiukweli kuna mizengwe mingi imegubikwa kuhusu muungano and so behond reasonable doubt Nyerere angeng'amua!
welevu+nyerere+warioba tulishaona mbali(RIP Abood Jumbe+ Osca Kambona) na ndo maana inatubidi kuwatendea haki washirika wa muungano na watu wake kama walivyoamua.
Tunahtaj serikali tatu ila nyie wenye fikra potofu mtavuja povu jingi sana kuendana na alama za nyakati!
Tunahtaj serkal tatu ili washirika watumie raslimali zao independently but very effectively!
 
Okay, lakini wasiibuke watu kwa kuwa Nyerere amefariki dunia, kudai kuwa Nyerere hakuwa na mawazo mgando, kwa maana ya kutaka kuhalalisha kuwa eti labda Nyerere angeliunga mkono wazo la serikali tatu! Hilo nalipinga hadi kaburini--msimamo wa Nyerere katika muungano hakuwa na mswalie mtume! Angeweza kukubali jambo lolote jingine libadilishwe kama alivyorelax katika suala la kubehuliwa kwa Ujamaa na mengine kadhaa (hata Azimio la Arusha) lakini sio katika muungano huu uliopo--hakutaka mchezo nalo kabisa akiamini kuwa ni suala la Msingi wa Taifa. Ninaposema hivyo sina maana kwamba ni dhambi kumkosoa Nyerere (coz hakuwa malaika), lakini ni dhambi kumpachika msimamo ambao aliupinga hadi mwisho wa maisha yake!! Baadhi yetu tulipata bahati ya kumfahamu vyema Mwalimu, tusidanganyane mchana kweupe!!


Ukweli ni huu muungano ulianzishwa na kuendeshwa kimagumashi na matokeo ya kufanya mambo kimagumashi ndio tunayashudia leo.
 
Katika hiyo hotuba alioitoa kwenye bunge la Afrika Kusini mwaka 1997, Mwalimu alikuwa anajenga hoja juu ya Umajumui wa Afrika ( Pan Africanism) kwa kuwaambia kama wazungu wanatuona sisi kama waafrika kwa nini sisi tuone fahari kwa kujitambulisha na viinchi vilivyotengenezwa na wakoloni kwa kubuni michoro katika ramani ya Afrika, na yeye kama unavyosema akatengeneza moja ( Tanzania). Kwa Nyerere aliyekuwa muumini wa Umajumui wa Afrika asingekubali kuona Tanzania ikifa kwa jina la serikali tatu.

Huwezi kutabiri Nyerere angesema nini leo kwa sababu hata alipokuwa hai ilibidi umsikilize kwa makini kumuelewa.

Na katika hili la kuvunja muungano, huwezi kujua angekuja na paradigm shift gani ambayo inaweza kuonekana counterintuitive ukiiangalia kwa juu, lakini yeye angeitetea kwa akili zake.

Kujifanya tunamjua mtu complex kama yule kiasi cha kuproject angesema nini leo, baada ya kufa miaka yote hiyo, ndiko kumdhalilisha kwenyewe.

Mnamfanya kwamba mawazo yake yalikuwa hafifu kiasi kwamba anatabirika ataenda wapi na kufanya nini.

Nimetoa mfano wa kusema "CCM si Mama yangu".

Kama aliweza kusema "CCM si mama yangu" hakuna ambaye anaweza kubisha kwamba siku moja angeweza kusema "Tanzania si mama yangu".

Vyote viwili aliviasisi.

Kama kuna uzuri au ubaya wa kudumisha au kuvunja muungano au serikali tatu, tuuseme tu. Kama kuna aliyofanya au kutenda Nyerere kabla hajafa, tuseme alitenda hili na kusema hivi.

Habari za kujitia ubashiri wa kusema tunajua leo angekuwepo angesemaje ni kumdhalilisha kwamba alikuwa formulaic, unimaginative, wooden, mechanic na asiyeweza kubadilika kutokana na nyakati.
 
Tanzania haitakufa kwa sababu ya serikali tatu. Inauwawa na mafisadi wa ccm. Nyerere lilipenda sn Azimio la Arusha maccm wakalinyongelea mbali kule Znzibr. Leo wanageuka eti wanamwonea huruma mwalimu kudhalilishw na Warioba. aSi kweli wnatka kutumia jina la mwalimu vibaya. Kwanza mujibu Nyere alkufa au mlimuua? Acheni unafiki bwana. Safari hii hilo mnlo na mtazaa nalo lazima.
 
Sasa tatizo hapa ni lipi?.

Huhitaji kuchimba zaidi siasa kufahamu kama Mw. Nyerere kweli hakuwa na mawazo mgando, na nitashangaa sana kama kuna kiongozi wa kisiasa anayeheshimika au aliyeheshika kwa kiwango kikubwa lakini ana mawazo mgando.

Na ifahamike kuwa Mwanasiasa mwenye mawazo mgando ni vigumu sana au haiwezekani kufahamu kesho atakuwa na mawazo na mtazamo upi kisiasa.

Hii dhana ya kusema Mwl. Nyerere kama angekuwa hai angefanya hivi au asingefanya hivi ni kujivika unajimu usio na mashiko kwa watu wenye mawazo na fikra pana. Niseme tu kuwa, hakuna anayefahamu Mwl. Nyerere angekuwa na mtazamo gani kwa sasa kuhusiana na Muungano.

Tusijenge hoja kwa kutumia mgongo wa watu ambao wameishamaliza kazi zao hapa duniani. Kwangu mimi ninaziona hizi ni spinning tu ambazo hazina mashiko yanayojisimamia zenyewe.

Jengeni hoja zenu na zijisimamie zenyewe ili wananchi wazichambue kama ni mchele au ni pumba.
 
Ninachomshangaaga Mzee Waryoba ni kuwa yeye kama Mwenyekiti wa kukusanya maoni ya wananchi hakutarajiwa kuwa na msimamo wa upande mmoja. Ni kama kocha wa mpira anatakiwa asionekane anaunga timu mmoja, alitakiwa kuwa 'neutral'. Ajifunze hata kwa raisi wetu JK anavyojitahidi kuonyesha hana upande mmoja ingawa ni Mwenyekiti wa CCM. Kwanza Tume ya Waryoba baada ya kuwakilisha rasimu ya pili ilisha kufa (ceased to exist) kwa mjibu wa sheria, sasa hizo kampeni anazozidi kuzifanya kuhusu serikali tatu si ni kukiuka sheria na taratibu? Kwanza tume yake ilihoji less than 0.1% ya Watanzania, wahojiwa hawakuzidi 40,000 na wote walikuwa wa mijini tu. Hivyo ku extrapolate kuwa Watanzania wengi wanataka serikali 3 ni ujuha wa hesabu za statistics! The sample was biased and was not representative, the sample size was too small to be statistically analysed. Tume ilichotakiwa (kabla ya kutoa rasimu ya katiba) ni kupendekeza kura ya maoni ya nchi nzima (national referrendum) kwa maswali yafuatayo kuhusu muungano: 1. Jee unataka muungano uwepo? 2. Kama jibu ni ndiyo unataka uwe wa namna gani (chagua moja): serikali moja, serikali mbili, serikali tatu. Matokeo ya kura hizo ndiyo yangetupa jibu la Watanzania wengi wanataka nini. Hata hivyo uamuzi wa mwisho si lazima uwe wa 'majority' kama tulivyofanya kwenye demokrasia ya vyama vingi ambapo kura za 'minority' ndizo zilishinda na mpaka sasa nadhani hatujajutia kama ambavyo tungafuata kura za 'majority' ambao walitaka demokrasia ya chama kimoja. Mzee Waryoba angenyamaza sasa na kuacha mchakato uendelee bila bias ya Tume ambayo imeshakufa. Kero za Muungano haziwezi kupunguzwa na serikali tatu, sana sana zitaongezeka na kuua muungano. Muungano ukifa hayo majeshi ya serikali ya muungano sijui tutayagawana vipi. Kero za muungano zitapungua tu kwa kupunguza mambo ya muungano na kubakiza machache yale ya msingi hasa ya ulinzi/usalama na utaifa (mambo ya nje). Mambo ya kuwa na ikulu 3, bendela na ngao za taifa 3, nyimbo za taifa 3 n.k. haitatusaidia cho chote. Halafu nani kamwambia Waryoba kuwa muungano utakapokufa sisi wabara tunalitaka tena hilo jina la tanga-nyika tulilopewa na Muzungu? Tutachagua jina tutakalopenda kama vile The Republic of East Africa.
 
Okay, lakini wasiibuke watu kwa kuwa Nyerere amefariki dunia, kudai kuwa Nyerere hakuwa na mawazo mgando, kwa maana ya kutaka kuhalalisha kuwa eti labda Nyerere angeliunga mkono wazo la serikali tatu! Hilo nalipinga hadi kaburini--msimamo wa Nyerere katika muungano hakuwa na mswalie mtume! Angeweza kukubali jambo lolote jingine libadilishwe kama alivyorelax katika suala la kubehuliwa kwa Ujamaa na mengine kadhaa (hata Azimio la Arusha) lakini sio katika muungano huu uliopo--hakutaka mchezo nalo kabisa akiamini kuwa ni suala la Msingi wa Taifa. Ninaposema hivyo sina maana kwamba ni dhambi kumkosoa Nyerere (coz hakuwa malaika), lakini ni dhambi kumpachika msimamo ambao aliupinga hadi mwisho wa maisha yake!! Baadhi yetu tulipata bahati ya kumfahamu vyema Mwalimu, tusidanganyane mchana kweupe!!

Kwa hiyo unataka kusema kuwa Nyerere ni mtu ambae alikuwa haendi na wakati wala ni mtu ambae alikuwa hashauliki atakacho kisema ndiyo hichohicho hakuna mtu yeyote anaeweza kufanya mabadiliko wa kile alicho kifanya au alichokisema kwa maana nyingine unachotaka kuaminisha hapa ni kwamba Nyerere alikuwa ni dikteta.Mbona Nyerere alipokuwa ana anza harakati zake za kisiasa alikuta kuna mfumo wa vyama vingi vya kisiasa kabla hajaupiga marufuku mfumo huo.Nyerere alidriki hata kuwaweka kizuwizini wale waliyothubutu kudai mfumo wa vyama vingi lakini ni Nyerere yule yule alie kuja kugeuka na kuunga mkono uanzishwaji wa vyama vingi vya kisiasa kwa vile mfumo wa kuwa na chama kimoja cha kisiasa ulikuwa umepitwa na wakati.Kama Nyerere aliweza kwenda na wakati kwa baadhi ya mambo aliyo kuwa ana yapinga kufa na kupona kwanini ashindwe kwenda na wakati kwa kuukubali muungano wenye serekali 3 ambayo ni maoni ya wtz waliyo wengi ukizingatia kuwa wa Tanganyika hawa kutendewa haki kwa kufutiwa nchi ya Tanganyika pamoja na serekali yao ya Tanganyika.
 
Mtoa hoja unapaswa kutazama pande zote mbili hoja yako imejikita zaidi kwenye kupinga serikali tatu, Sema faida na hasara za kila mfumo wa serikali halafu fanya hitimisho
 
Mleta mada umepatia sana. Mungu akubariki. Jaji warioba nampenda, lakini kwa serikali tatu kaweka utashi wake. Njelu kasaka, muumini wa serikali tatu hakubaliani naye. Stay tune! Tanzania yangu maskini inakufa
. Tutaipigania hadi mwisho.

Kaka Manyerere kuanzia sasa narudisha heshima yangu kwako maana Kuna wakati niliiondoa kwasababu ulikuwa unashabikia Fisadi Lowassa, Kwahili la serikali mbili tuko pamoja.
 
Sasa wewe mwenyewe una uhakika gani kama Mwalimu asingeunga mkono serikali tatu?ina maana Mwalimu yeye asingekuwa mtu wa kwenda na wakati?
 
Serikali tatu siyo suluhisho hata kidogo!! Warioba kalazimisha tu matakwa yake!! Suluhisho ni serikali moja tu!!

Halafu mwache mambo ya Nyerere, kwani yeye alikuwa Mungu hadi kila kitu atukuzwe nacho?? cc faiza Foxy
 
Last edited by a moderator:
Mwalimu alikuwa mpenda mabadiliko. Hilo halina ubishi. Mwalimu angeweza kuzikubali Serikali Tatu, lakini asingekubali kuona hizo Serikali zinauua Muungano. Kwake Muungano kilikuwa kitu cha maana zaidi kuliko hawa wanaohoji mara Tanzania Bara, mara Tanganyika! Dunia inaungana, lakini huku kwetu watu wanashabikia kutengana. Dhambi hii inabebwa na kina Mzee Mkapa waliohakikisha wanakwenda kusimamia Sudan igawanyike! Wamefanikiwa, ndiyo maana hapa husikii maoni yao ya kuitetea Tanzania! Haitashangaza baada ya kuipata Tanganyika, zikawa Makonde Land, Kanda ya Ziwa, Sukuma Land, nk. Nasisitiza tena na tena, jamani someni kitabu cha Mwalimu cha Uongozi Wetu na Hatima ya Tanzania. Haki ya Mungu kile kitabu sidhani hata kama hawa wakubwa wanakisoma. Watu wazima kama kina Kardinali Pengo wameona hatari inayolikabili Taifa!
 
Kaka Manyerere kuanzia sasa narudisha heshima yangu kwako maana Kuna wakati niliiondoa kwasababu ulikuwa unashabikia Fisadi Lowassa, Kwahili la serikali mbili tuko pamoja.

Chuki, asili ya kazi yangu inanifanya niwe karibu na watu wa aina zote. Kamwe sijawahi kumchukia Lowassa, Membe, Mbowe, Lipumba, Mtikila au mwanasiasa yeyote. Kwanza kwa imani yangu nazuiwa kuwa na chuki dhidi ya mtu mwingine. Pili, siwezi kuwa na chuki na mtu kwa maneno ya kusikia tu. Wote mmeingia kuimba na kucheza wimbo wa ufisadi wakati hamuujui. Vita ya wakubwa unapaswa kuingia kwa akili sana. Sipo tayari kuburuzwa kwa kuaminishwa kuwa fulani ni fisadi, basi nikafuata mkumbo. Nikijiridhisha kuwa fulani ana jambo lisilo la manufaa kwa nchi yangu sitomchukia, lakini nitakuwa mbali naye.
 
Hivi unaweza kweli kumdhalilisha marehemu aliyetangulia mbele ya haki miaka zaidi ya kumi iliyopita? Mimi nilizaliwa Tanzania lakini nina hamu kubwa ya kuiona Tanganyika ili niwe najitambulisha kwa uasili wa taifa langu kama wenzetu wazanzibari. Kwa sasa naona kama huu unaoitwa utanzania umekaa kiusanii sana. Yaani ndani ya utanzania kuna watu ni watanzania pekee na kuna wengine ni watanzania na wazanzibar kwa wakati huo huo.
 
Kati ya viongozi wa ccm waliofanya mambo kwa kuona mbali zaidi ya leo ni Nyerere.na hakuna anayeweza toa jibu sahihi kwa nini nyerere aliinyoshea kidole ccm. Pengine ni kwa kuipuza katiba,kama aliyaona hayo hata leo asigesita kuyapokea mabadiliko.
 
Hujasema wewe mtazamo wako ni upi kila mtu anahaki ya kutoa mawazo yake we unautaka muungano upi.
 
Ni kwel mwl hakuwa na mawazo mgando,wengi wetu ndio tuna mawazo mgando.
Mwl alifariki 1998 leo 2014 isiwe Nyerere awe mwisho wa upeo wetu kufikiri na kujadli mustakabali wa Taifa letu.
Muungano uliozaa Tanzania ni kt ya Tanganyika na Zanzibar iwaje tukatae nchi yetu ya asili,huu ni utumwa.
Yatubidi tubadilike,kuhusu gharama kwa sasa ni kumbwa kuliko kukiwa na hizo serikali tatu.
 
Back
Top Bottom