Waraka wangu maalum kwa Watanzania wote

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
41,539
2,000
ANGALIZO

Waraka huu nautoa kama GENTAMYCINE na siyo GENTAMYCINE mwana CCM au Mpinzani na Mtani Mkuu wa CHADEMA ( anavyojulikana na wengi humu ) na nautoa huku nikimtanguliza Kwanza Mwenyezi Mungu mbele, Unafiki pembeni na nikiiweka Mama Tanzania mbele yangu ili tuendelee kuifurahia Tanzania yetu.

 1. Nawaomba Wanasiasa wa Tanzania wasameheane upesi kama siyo haraka sana
 2. Nawaomba Wanasiasa wa Tanzania wakatubu yale yote mabaya waliyosababisha
 3. Nawaomba Wanasiasa wa Tanzania waache chuki ambazo naona zinatupeleka kubaya
 4. Nawaomba wana CCM muonyeshe mfano wa Siasa bora na zenye Utu pamoja na Upendo
 5. Nawaomba wana CHADEMA muonyeshe Uungwana na Ukomavu wenu wa Kidemokrasia
 6. Naviomba Vyombo vyote vya Ulinzi na Usalama Tanzania vitende haki
 7. Nawaomba Wanasiasa wote mfutane makovu ya Hasira na Vinyongo
 8. Nawaomba Viongozi wote Wastaafu waingilie kati afya ya wasiwasi ya Kidemokrasia nchini
 9. Naviomba Vyombo vyote vya Habari nchini vidumishe Upendo na Amani daima
 10. Namwomba Rais Dr. Magufuli aige busara na hekima za Yesu Kristo / Mtume Mohammed
 11. Naomba Watanzania wote tusali sana, tupendane na tugange yajayo kwa matendo mema
Moyo wangu una wasiwasi sana kwa jinsi hali ya Kisiasa ilivyo sasa Tanzania. Haiwezekani kila siku ni kukamata kamata tu, kujibizana vibaya, kutishana, Kukomoana, Kuviziana pasipo sababu wakati wote Sisi ni Watanzania wale wale ambao tunahitajiana Kimaisha pengine hata kuliko hizi Siasa zetu za ' Maji Taka ' ambazo hazina ' Tija ' sana kwa Maendeleo tunayoyakusudia. Mungu tusaidie huku ukitufanya tuchukuliane, tuvumiliane na tudumishe umoja wetu wa Kitaifa tulioachiwa na Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere na Abeid Aman Karume!

Nawasilisha.
 

Haya_Land

JF-Expert Member
Dec 26, 2017
5,258
2,000
Tumeshawazoea hizo sifa unatafuta upandishwe Mshahara!!!!
Ila nikwambie tuu maguful hana rafiki kutokana na roho yake ya JIWE,unaweza fukuzwa Muda wowote!!Uongozi wa Kiki kutwa mnashindana na vyombo vya habari Ili zirushe habari zenu za kimbuzi wakati KITAA kigumu mlo mmoja.
 

Spectator

JF-Expert Member
Aug 26, 2017
225
500
Mkuu ajifunze, maandamano sio siasa chafu!

Siasa chafu;
1. Mabao ya mikono
2. Kuubambikizia kesi wapinzani (mbona hajawahi fungwa wala kushtakiwa mpinzani yoyote kuhusu kupanga njama wala kuratibu vurugu!)
3. Utekaji wa wanaoikosoa serikali.
4. Kununua wapinzani nk

Hayo hayapo kwenye katiba. ILA MAANDAMANO YAMEHALALISHWA NA KATIBA!! HIYO NI SIASA SAFI.
 

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
41,539
2,000
Aige hekima za KRISTO, hapana aanze kwanza kuiga hekima za Uhuru Kenyatta.....

Hata Uhuru Kenyatta alianza Kwanza Kuiga za Kristo. Labda unataka kutuaminisha kwamba Uhuru Kenyatta ni zaidi ya Yesu Kristo wa Nazareth.
 

MIXOLOGIST

JF-Expert Member
Mar 1, 2016
5,269
2,000
AMEN na INSHAALLAH Mkuu.

Huwezi amini moyo wangu unaniuma sana kila nionapo haya yanayoendelea sasa na ambayo naona kama vile sasa yanaanza kuzoeleka. Mungu atusaidie!
Hakika Mkuu, mambo hayako sawa au kwa uhakika hayako kama zamani. Tuombe Mungu atufanyie wepesi atuepushe na kila shari.
 

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
41,539
2,000
Hakika hili ni juma takatifu!

Naam Mkuu. Nina wasiwasi sana tunakoelekea siko kabisa na tusipojitafakari haraka kuna uwezekano mkubwa katika ' mioyo ' ya Watanzania wengi kukajaa ' Sumu ' kali ya Chuki, Visasi na Kukomoana.

Naomba huu ' Waraka ' wangu upokelewe kwa nguvu zote na tusaidiane kutimiza hayo niliyoyaorodhesha kwa afya njema kabisa ya Siasa na Demokrasia ya Tanzania kwa sasa na baadae.

Nisiwe mwongo wala mnafiki ukweli ni kwamba kwa sasa hatuendi vizuri na nanusa hatari.
 

Mwanzi1

JF-Expert Member
Sep 19, 2016
5,977
2,000
Haya yana anza na wanachi kabla ya wanasiasa, wanasiasa watabadilika kama wanachi wakibadili mienedo yao. Tatizo kubwa ni Instagram haisadi kubadili mienendo ya watu.
 

themanhimself176

JF-Expert Member
Dec 28, 2016
1,757
2,000
NimependA namba 6 japo yote yako sahihi

Tukiishi kma ulivyosema mbona inakuwa raha

Allah atufanyie wepesi katika kipindi ichi ambacho nchi yetu inapitia mengi yasiyo ya haki wala kupendeza
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom